STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 31, 2014

INATISHA! VIKONGE 38 WAUWAWA SHINYANGA

Jumla ya vikongwe 38 wameuawa  mkoani Shinyanga katika matukio tofauti, yakiwamo ya kuhusishwa na uchawi na ushirikina na wengine kudaiwa kutowapa urithi watoto wao matokeo yake watoto kuua wazee wao
Akizungumza na waandishi wa habari juzi kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga SACP Justus Kamugisha,alisema vikongwe wamekuwa wakiuawa, bila ya kuwa na hatia kutokana na kuhisiwa kuwa ni wachawi.
Alisema mbali na imani za kishirikina vikongwe wengine wamekuwa wakiuawa kikatili wakidaiwa kung’ang’ania mali na kutowagawia watoto wao hivyo watoto hao kuamua kutekeleza mauaji hayo.
Kamugisha alifafanua katika kipindi cha mwezi Januari hadi Desemba mwaka jana (2013), jumla ya vikongwe 27 wameuawa yaani katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini vikongwe 11, Kahama 9 na   Kishapu 7.
Aliongeza kuwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Julai mwaka huu (2014),vikongwe 11 wameuawa,ikiwa katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini vikongwe 6,  Kahama 4, Kishapu mmoja.
“Jumla kuu ya vikongwe waliouawa katika kipindi cha mwaka jana hadi Julai  mwaka huu wa 2014,ni 38”,alisema kamanda Kamugisha
Kufuatia mauaji hayo kamanda Kamugisha aliwataka wakazi wa mkoa wa Shinyanga kuacha kuendekeza imani za kishirikina,ambazo zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa mauaji hayo ya vikongwe, huku akiwataka vijana kushighulisha ili kujipatia kipato na kuacha dhana tegemezi ya mirathi.
Kamugisha alisema katika msimu wa mwaka huu wa mwaka 2014/2015, atahakikisha anakomesha uhalifu mkoani Shinyanga, pamoja na kutokomeza mauaji hayo ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). 
Aidha aliwataka wananchi likiwamo na jeshi la jadi sungu sungu kushirikiana kwa pamoja na  kuhakikisha, wanawakamata wahalifu, ili kuwafikisha katika vyombo vya dola, na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili liwefundisho kwa watu wengine.
Aliongeza kuwa hivi sasa anatarajia kusambaza polisi kata, kwa kila kata kwani baadhi ya kata hazina polisi hao, hali ambayo itasaidia kushirikiana kwa ukaribu na wananchi katika kuhakikisha anawatia nguvuni waharifu.

No comments:

Post a Comment