STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 31, 2014

Jaydee afunguka tuhuma za kutoka dogodogo

http://1.bp.blogspot.com/-weW6cZWZj7Y/UJqGqZJf4nI/AAAAAAAAALM/AB-sQhv5jF8/s400/DSC05503.JPGNYOTA wa muziki na mmoja wa wasanii wenye mafanikio makubwa nchini lakini asiye na makeke, Judith Wambura Mbibo 'Lady Jaydee' a.k.a Anaconda ameamua kujibu habari iliyoandikwa katika gazeti moja la udaku kuhusu kuwa na uhusiano na aliyewahi kuwa mtuma salamu maarufu kwenye redio, Meddy Ahmed aka ‘Mtoto wa Vitoto’.
Kwenye habari hiyo, gazeti hilo linalotoka mara mbili kwa wiki lilidai kuwa Jaydee ambaye anadaiwa kuachana na mume wake Gadner G Habash ameonekana mara kadhaa na Mtoto wa Vitoto na kwamba amewahi kuonekana akiwa na gari lake.
Kupitia Instagram, Jaydee ameandika:
"Kuna habari za kuniudhi Ila hii imenichekesha. Kwahiyo mtoto wa vitoto ndio bwana angu???? Basi sawa nashukuru naona mmenianzia tena sasa picha za February Na nilizi post mwenyewe humu insta leo ndio mmeziona? Ukweli mnaujua mmeamua tu kuzingua ,,, wangapi wameshapiga picha na hiyo Range? Duuuh! !!!!! Shkamoooni Moyo wangu chuma. Pigeni mawe mpk mchoke Kama ambavyo mmekuwa mkifanya miaka yote na bado nipo hapa hapa.

No comments:

Post a Comment