STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 31, 2014

Chelsea yazidi kujiimarisha, Kagawa arejea Dortmund

KLABU ya Chelsea imezidi kujiimarisha baada ya kukamilisha uhamisho wa Loic Remy kwa dau la Pauni Milioni 8 kutokaq QPR, huku Mjapan Shinji Kagawa wa Manchester United akirejea klabu yake ya zamani ya Borrusia Dortmund.
Remy aliyekuwa anatakiwa pia na Arsenal, anakwenda kuziba nafasi ya Fernando Torres aliyehamia AC Milan kwa mkopo wa muda mrefu.
Uhamisho huu ni faraja kwa Remy ambaye sasa anakwenda kujiunga na klabu inayocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kocha Mreno, Jose Mourinho alihitaji mshambuliaji baada ya kumtoa kwa mkopo Torres.
Katika kuelekea mwisho wa kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya, Shinji Kagawa ambaye hakuwa akipewa nafasi kubwa ndani ya Mashetani WEkundu amerejea Ujerumani kuichezea Dortmund.
Kiungo huyo amerejea Dortmund kwa dau la Pauni Milioni 6.3, miaka miwili tu tangu aondoke klabu hiyo ya Ujerumani.
Kagawa atasaini Mkataba wa miaka minne na Dortmund, ambayo ilimuuza Mjapani huyo United mwaka 2012 kwa Pauni Milioni 12.
Shinji Kagawa akikabidhiwa uzi wake mpya wa Dortmund baada ya kuondoka Manchester Utd

Remy: 'When I heard Chelsea wanted me I said "let's go" because they are one of the best clubs in the world.'
Remy akisaini mkataba wa kujiunga na Chelsea
Akionyesha uzi mpya wa klabu yake ya Chelsea

No comments:

Post a Comment