STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 31, 2014

Spurs, Liverpool ni vita tupu, Arsenal kujiuliza ugenini

http://screaming-eagles.com/wordpress/wp-content/uploads/2013/12/Tottenham-vs-Liverpool.jpghttp://337sports.net/wp-content/uploads/2014/08/Leicester-City-vs-Arsenal.jpg
WAKATI jinamizi baya likiendelea kuiandama Machester United baada ya kulazimishwa suluhu na timu iliyopanda daraja Burnley, huku majirani zao Machester City wakibamizwa nyumbani na Stoke City, leo ni zamu za Tottenham Hotspur na Liverpool kuonyeshana kazi katika Ligi Kuu ya England.
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu itapigwa kwenye uwanja wa White Hart Lane, London ya Kaskazini Spurs ikitaka kuendeleza maajabu yake ya kupata ushindi mfululizo katika ligi pia wakitaka kurejea kileleni baada ya kuenguliwa na Chelsea iliyoifumua Everton ikiwa uwanja wa ugenini mabao 6-3.
Mbali na mechi hiyo leo pia katika ligi hiyo kutakuwa na mechi nyingine mbili Arsenal ikiwa ugenini itavaana na Leicester City na Aston Villa kuikaribisha Hull City.
Liverpool ambayo ilimnyakua mshambuliaji mpya toka AC MIlan, Mario Balotelli imetamba kuwa itaanza kumtumia mchezaji huyo katika mechi hiyo, ikiamini atashirikiana na wenzake kurejesha heshima baada ya wiki iliyoipita kufumuliwa mabao 3-1 na mabingwa watetezi Manchester City.
Vijana hao wa Branden Rodgers wanahitaji ushindi katika mechi hiyo ya ugenini ili kuwatuliza mashabiki wao ambao wanaamini pengo la Luis Suarez aliyewapa raha msimu uliopita bado halijapata wa kuliziba labda baada ya ujio wa 'mtukutu' Mario Balotelli aliyerejea katika ligi ya England baada ya miezi kadhaa.
Mbali na mashabiki wa kandanda kuwa na hamu ya kutaka kuona Supr Mario atafanya kitu gani leo mbele ya Spurs inayotambia nyota kadhaa akiwamo Emmanuel Adebayor na ambayo haijaruhusu wavu wake kuguswa tangu ligi hiyo ilipoanza Agosti 16.
Katika pambano la Arsenal iliyoanza kwa ushindi kabla ya kuponea chupuchupu kipigo toka kwa Everton wiki ijayo itakuwa na hamu ya ushindi ili kuendeleza furaha yao ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa 17 mfululizo baada ya kuilaza Besiktas ya Uturuki katikati ya wiki.
Baoa la nyota wake mpya kutoka Chile, Alexis Sanchez lilitosha kumtuliza Arsene WEnger ambaye amekuwa akimkingia kifua mashambuliaji huyo baada ya kuanza ligi bila kuonyesha vitu vyake vilivyomfanya Arsenal wamsajili baada ya Kombe la Dunia la nchini Brazili akitokea Barcelona.
Je, ni Spurs itakayoendeleza wimbi la ushindi au LIverpool itakayofufukia mikononi mwa Super Mario au ni Arsenal kupata ushindi ugenini leo? Tusubiri!

No comments:

Post a Comment