STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 13, 2014

TFF kutoa mafunzo ya Tiketi za Elektroniki

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/08/Wambura1.jpg
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo Jumamosi kuanzia saa 4 asubuhi litaendesha mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki kwa wadau wa mpira wa miguu Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura, mafunzo hayo Uwanja wa Taifa, yatashirikisha wasimamizi wa mechi, viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na makatibu na maofisa habari wa klabu za Azam na Yanga.
Washiriki wengine wa mafunzo hayo ni Meneja wa Uwanja wa Taifa na msaidizi wake, wasimamizi wa milangoni (stewards), waandishi wa habari wa Dar es Salaam maofisa usalama wa TFF.
Mafunzo hayo yatahitimishwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) kwa mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga kuanzia saa 10 kamili jioni. Tiketi zimeanza kuuzwa jana (Alhamisi) kupitia M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka ya Fahari Huduma.

No comments:

Post a Comment