STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 13, 2014

Van Gaal afichua siri ya kumuuza Welbeck kwa Arsenal

Danny Welbeck
Danny Welbeck
WAKATI nyota wa zamani wa Manchester United na hata mashabiki wakishindwa kuamini kama Kocha Luis Van Gaal amemuuza Danny WElbeck kwa mahasimu wao Arsenal, meneja huyo amefichua siri ya kumtema mshambuliaji huyo.
Van Gaal amesema Welbeck aliachwa kwa sababu hakufunga mabao ya kutosha huku akidai kuwa atawapa nafasi wachezaji ndani. 
Akiongeza wakati wa kuwatambulisha wachezaji wawili waliosajili mwishoni Radamel Falcao na Daley Blind, Van Gaal alifafanua kwanini Welbeck, 23 aliuzwa kwa Arsenal kwa kitita cha paundi milioni 16. 
Van Gaal amesema Welbeck amecheza misimu mitatu akiwa na kikosi cha kwanza lakini hajafikia rekodi ya Robin van Persie au Wayne Rooney katika ufungaji. 
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa hiyo ndio sababu iliyomfanya auzwe kwasababu ya Falcao na pia kutoa nafasi kwa wachezaji chipukizi nao kupata nafasi.
Tangu Welbeck auzwe nyota wa zamani wa Old Trafford akiwamo David Beckham wamekuwa wakilaumu kitendo hicho kwa kuamini kuwa mshambuliaji huyo bado alistahili kubakishwa kwa Mashetani Wekundu hao kwa umahiri wake.

No comments:

Post a Comment