STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 13, 2014

Jennifer Mgendi amrudia Shelina

http://www.jennifermgendi.com/images/gallery/1361182868.jpg

MUIMBAJI nyota wa muziki wa Injili, Jennifer Mgendi amesema ataingia mzigoni kutengeneza filamu yake mpya iitwayo 'Shelina' baada ya awali kuisitisha kupisha kazi nyingine anayojiandaa kuitoa hadharani.
Jennifer alipanga kuitengeneza filamu hiyo ya Shelina mapema mwaka huu, lakini aliahirisha ili kurekodia 'Mama Mkwe' ambayo imeshakamilika na itaachiwa wiki ijayo.
Akizungumza na MICHARAZO, alisema hakuona kama ni busara kuzitengeneza filamu hizo mbili kwa wakati mmoja, ndiyo maana ataisitisha 'Shelina' ili kuimalizia 'Mama Mkwe' na baada ya hapo ndipo akirudie 'kiporo' chake ambacho atawashirikisha wasanii mbalimbali nyota wa muziki wa Injili na wale wa Bongo Movie.
Miongoni mwa wasanii wanaotarajiwa kushiriki filamu hiyo kwa mujibu wa Jennifer ni; Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Christina Matai na Bi Esther.
"Nilisitisha kuendelea na Shelina ili kupisha filamu ya 'Mama Mkwe' ambayo nitaiachia Sept 22, baada ya hapo kazi itaanza mara moja," alisema.
Jennifer Mgendi anayetamba na albamu kadhaa za nyimbo za Injili ikiwamo ya 'Hongera Yesu' iliyopo sokoni kwa sasa, amewahi kukimbiza na filamu kama 'Joto la Roho', 'Pigo la Faraja', 'Teke la Mama' na 'Chai ya Moto'.

No comments:

Post a Comment