Bondia Djamel Dahou wa Algeria aliyempiga Yazidu kwa KO ya raundi ya kwanza |
Alibaba (kulia) akatika mazoezi kabla ya kushinda jana dhidi ya Mmalawi |
Hata hivyo watanzania walijifariji baada ya bondia Ali Ramadhani 'Alibaba' kumshinda kwa pointi Mmalawi Alick Mwenda na kutwaa mkanda wa UBO Afrika katika pambano jingine la kimataifa.
Yazidi mmoja wa mabondia wakongwe waliowahi kujijengea jina siku za nyuma, alishindwa kuhimili vishindo vya mpinzani wake na kujikuta akishindwa kumaliza raundi ya kwanza kwa kuchakazwa na Dahou.
Mtanzania huyo alijikuta akisalimu amri kwa mpinzani wake katika dakika ya pili sekunde ya saba na kuuacha mkanda huo wa Dunia ukiondoka katika ardhi ya Tanzania.
Kabla ya pambano hilo lililokuwa la raundi 12, Ali Ramadhani maarufu kama Alibaba wa Tanzania aliweza kupambana vilivyo na kumshinda mpinzani wake kutoka Malawi, Alick Mwenda kwa pointi 100-99 katika pambano la kuwania ubingwa wa Afrika unaotambuliwa na UBO.
Katika pambano hilo la raundi 10 mabondia wote walionyesha ujuzi wao kwa kutupiana makonde kiufundi na ndipo majaji walipotoa matokeo yaliyompa Alibaba ushindi huo wa pointi dhidi ya Mmalawi.
Michezo hiyo na minmgine ya utangulizi iliandaliwa na kampuni ya Green Hill Promotion chini ya usimamizi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST).
No comments:
Post a Comment