| Skauti walioongoza maandamano wa kuingia kwenye eneo la tukio |
| Ni wakakamavu kudhihirisha ni mashujaa wa kesho |
| Kwa mwendo wa pole mbele tembeaaaaaa! |
| Matarumbeta yalikuwapo kusapoti sherehe hizo |
| Wahitimu wakielekea kwenye eneo la tukio |
| Maandamano fulani ya kuonyesha furaha yao ya kuhitimu Darasa la Saba |
| Mkuu wa Shule ya Msingi, Neville Marandu akizungumza machache, huku Mkuu wa Shule za Brain Trust, Irene Makinda (pembeni yake kulia) akiwa bize |
| Hawa nao walikuwapo kushuhudia kila kitu kwa umakini zaidi |
| Baadhi ya wazazi na walezi waliohudhuria sherehe hizo jana Yombo Vituka |
| Wazazi na walezi wakiwa makini kufuatilia kila tukio katika mahafali hayo |
| Hakuna aliyetaka kupitwa na jambo au asimuliwe na mtu |
| Gift Marandu akisoma shairi mbele ya hadhira kwa umahiri mkubwa |
| Kama Mwanamalenga katika ughani mashairi |
| Dada zao wa Sekondari nao walikuwapo kuwapa mkono wa kwaheri |
| Kwa herini wadogo zetu, heri twawatakia, makini muwapo makwenu.... |
| Dada zao wa Sekondari wakiendelea kuwaburudisha kwa kuwaimbia ngonjera na nyimbo |
| Ikawa zamu ya wahitimu wenyewe kuingia kilingeni kuonyesha umahiri wao |
| Kwa kujiamini wahitimu wakiingia uwanjani kuangusha burudani la mwisho mwisho |
| Kazi ikaanza kwa kuimba wimbo |
| Wakaangusha na ngonjera |
| Mashairi pia yalikuwapo |
| Wahitimu wa Elimu ya msingi wa Shule ya Brain Trust wakiendeleza kutoa burudani |
| Samuel Robert (kulia) akawaongoza wenzake kuangusha njongera |
| Dogo achana naye ana kipaji cha kughani acha bhana! |
| Kwa mbwembwe ndiyo kabisaaaaa |
| Ikawa zamu ya mwanadada naye kuonyesha makeke yake |
| Skauti nao wakaingia uwanjani kuonyesha umahiri wao katika sanaa hiyo |
| Hayaaaa twende |
| Ni nyuma geuka, kulia geuka kwa ukakamavu kama maafande |
| Ikaja zamu ya mwnafunzi huyo wa Chekechea Mereciana Ronald ambaye aliangusha burudani ya kufa mtu |
| Anacheza kwa pozi taratibu kama hataki |
| Kadri mzuka ulivyokuwa ukimpanda ndivyo alivyoongeza makeke kwa kunengua muziki |
| Akachanganya kasi we kama Aisha Madinda |
| Hapo chachaaaa! Yebaaaa |
| Mkuu wa Shule ya Msingi Brain Trust, Neville Marandu akisoma wasifu wa shule |
| Mgeni rasmi ikafika zamu yake kutoa nasaha zake ni Richard Mngomo wa Tanzania Printers |
| Msiridhike na kumaliza kwenu la Saba bado mna kazi kubwa mbele yenu, ndivyo alivyowanasihi wahitimu |
| Wahitimu wakaanza kukabidhiwa vyeti vyao |
| Immaculata Justine Limonga, naye alitunukiwa cheti na mgeni rasmi wa mahafali hayo |
| Ilikuwa furaha kwa wahitimu baada ya kukabidhiwa vyeti vyao |
| Immaculata Justine akiwa katika picha mbalimbali na familia yake baada ya kukabidhiwa cheti cha kuhitimu darasa la saba katika shule ya Brain Trust |
| Anafanyiwa surprise |
| Pokea keki ya zawadi mwanangu |
| Mdogo mtu anampokea keki ya zawadi |
| Daa nitaifaidije hiii |
| Akifurahia zawadi ya Mwanafunzi Mwenye Nidhamu na Msafi kuliko wote Brain Trust School |
No comments:
Post a Comment