STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 13, 2014

Halima Mdee aibuka kidedea CHADEMA, asema la moyoni

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/09/HalimaMdee.jpg
MWANASIASA machachari ambaye pia ni Mbunge wa Kawe Halima Mdee CHADEMA amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la wanawake wa Chama hicho (BAVICHA) unaoendelea katika ukumbi wa Mlimani City.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Mdee aliwaasa wanawake kwa wanawake kuwa wamoja badala ya kupigana vijembe wao kwa wao ili maendeleo ya mwanamke yaweze kupatina na na kuondokana na mfumo dume
“Nimezoea kuona watu wanaotukashifu ni wa upande wa pili kutokana na mfumo dume uliojengeka na sio wanawake wenyewe kukashifiana,” alisema.
Alisema mwanamke ana nguvu ya kuleta mabadiliko na kueleza kuwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kipo madarakani kwa sababu kinawatumia wanawake na kutaka nao kuungana na kuwa kitu kimoja.
“Mwanamke ana nguvu ya kuleta mabadiliko, bila kuwatumia  hakuna ushindi na wanawake siku zote wanamsimamo na sio wasaliti hata kidogo,” alisema Mdee.
Aidha aliwataka wanawake wakafanye kazi majimboni kwa umoja licha ya kufahamu wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa fedha.
“Harakati zetu sio za starehe na hata ikiwezekana pindi mnapokuwa majimboni bila kujali mnalala wapi, mnatumia choo cha ‘pasipoti size’ ili mradi ushindi unapatikana,” alisema.
Akitangaza matokeo hayo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana, Arcado Ntagazwa, alisema Mdee alipata kura 165 akifuatiwa na Janeth Rithe 35, Sophia Mwakagenda 18, Chiku Abwao 15, Lilian Wassira 11 na Rebecca Magwishe kura 4.
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti upande wa Bara, alitangazwa Hawa Mwaifunga aliyejinyakulia kura 136 akifuatiwa na Victoria Benedict kura 99.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar ilichukuliwa na Hamida Abdalah Huewishi aliyepata kura 194 akifuatiwa na Mariamu Msabaha kura 36.

No comments:

Post a Comment