STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 13, 2014

Yanga wakubali yaishe kwa Twite yawaita Fc Lupopo mezani

http://api.ning.com/files/3I-9LvQkoOSAPbzeGPW5yP6OSfiIe*zDKxvTvEruLBnPGhxkE3j8HJX2IRwtbIWsugVPQAhAda5j3SU7tPM2CI5dsqk6mOCF/MBUYUTWITESALAMAJAMANIPIXNO5.jpg
Mbuyu Twite
UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema umeshangazwa na wenzao wa timu ya a FC Lupopo ya JK Kongo kudai Mbuyi Twite alijiunga nao kwa mkopo, hata hivyo wameamua kuwaita mezani kumaliza mambo kiutu uzima tofautis na tisho la Lupopo kutaka kukimbilia FIFA kushtaki.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Beno Njovu, alisema Yanga haikumsajili Twite kwa mkopo.
Akifafanua zaidi, Njovu, alisema Lupopo inataka ilipwe fedha zaidi mara baada ya Yanga kumuongezea mkataba Twite baada ya ule wa awali kumalizika.
"Mbali na malalamiko mengine ya wenzetu, pia wanataka walipwe pesa baada ya Twite kuongezewa mkataba.. lakini kwenye mkataba hakuna makubaliano kama hayo wakati tunamchukua Twite," alisema Njovu.
Aidha, alisema kuwa ili kuweka mambo sawa, Yanga imewasiliana na viongozi wa Lupopo ambao siku yoyote kuanzia leo watawasili nchini kwa ajili ya mazungumzo.
"Tumewapigia simu hao jamaa na watawasili nchini kuanzia kesho, tutakaa kuwaelewesha na naamini tutaelewana..., ila nataka muelewe kuwa hatukumchukua Twite kwa mkopo," aliongezea kusema Njovu.

No comments:

Post a Comment