STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 13, 2014

Ni shidaa leo England, Arsenal uso kwa uso na watetezi Man City


KIVUMBI cha Ligi Kuu ya England, kinatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii baada ya kupisha michezo ya Kimataifa wiki mbili zilizopita ambapo leo Jumamosi Arsenal itavaana na watetezi Manchester City.
Mwezi uliopita, Arsenal iliichapa Man City Bao 3-0 Uwanjani Wembley kwenye Mechi ya kufungua pazia Msimu mpya kugombea Ngao ya Hisani lakini kwenye Ligi Arsenal wameshinda Mechi moja na kutoka Sare Mechi 2 zilizopita.
Nao Man City walianza kwa ushindi katika Mechi mbili za kwanza lakini kwenye Mechi yao ya mwisho Uwanjani kwao Etihad walitandikwa 1-0 na Stoke City.
Mbali ya Mechi hii, Chelsea, ambao wanaongoza Ligi kwa kushinda Mechi zao zote 3, watakuwa kwao Stamford Bridge kucheza na Swansea City ambao ndio wamefungana nao kileleni na ambao pia wameshinda Mechi zao zote 3.
Lakini Chelsea huenda wakamkosa Straika wao Diego Costa mwenye  mabao manne na aliyeshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti kutokana na kuwa majeruhi.

RATIBA kamili ipo hivi:
Leo Jumamosi
14:45 Arsenal v Man City
17:00 Chelsea v Swansea
17:00 Crystal Palace v Burnley
17:00 Southampton v Newcastle
17:00 Stoke v Leicester
17:00 Sunderland v Tottenham
17:00 West Brom v Everton
19:30 Liverpool v Aston Villa
Kesho Jumapili
18:00 Man United v QPR
Jumatatu
22:00 Hull v West Ham

No comments:

Post a Comment