Msemaji wa klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga |
STRIKA

USILIKOSE

Tuesday, March 19, 2013
Mabondia nusura wazichape kavukavu kasi...!
Mabondia Immanuel “Prince” Naidjala wa Namibia na Lesley Sekotswe wa Botswana
wamekutana leo katika mkutano wa waandishi wa habari. Kukutana kwao nusura
kulete balaa kubwa baada ya mabondia wenyewe kuingia midadi na kutaka kuzipiga
kavu kavu mbele ya vyombo vya habari
Immanuel "Prince" Naidjala
Mkutano huo ulifanyika
katika hotel ya Windhoek Country Club Resort ambayo ni moja ya Casino kubwa
katika nchi ya Namibia. Vyombo mbalimbakl vya habari kutoka nchi za Afrika na
Ulaya zilishiriki katika mkutano huo ambao wawili hao walitambiana kupeana
mkongoto wa uhakika watakapokutana siku ya jumatano tarehe 20.
Mabondia hao wanakutana
tena kesho tarehe 19 katika hoteli hii katika zoezi la kupima uzito
kabla ya mpambano wao siku ya Jumatano ambayo ni siku ya Uhurru wa nchi ya
Namibia. Viongozi wakuu wa serikali ya Namibia watahudhuria mpambano huo ambao ni mkubwa kuwahi
kufanyika katika nchi hii yenye wakazi milioni mbili na ushee!
Naye Rais wa IBF katika
bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi amewasili
jijini Windhoek leo akitokea nchini Ghana kulisimamia pambano hili la ubingwa
wa “IBF International Title”
Rais Ngowi ametokea jijini Accra, Ghana ambapo
alishughudia mabondia Richard Commey na Bilal Mohammed wakitoana jasho ambako
Richard Commey aliibuka kuwa bingwa wa uzito mwepesi katika bara la Afrika.
Promota wa mpambano huo Nestor Tobias wa kampuni
maarufu ya Sunshine Boxing Promotions ana uhakika wa mpambano huu kuvunja
rekodi ya kuingiza watu wengi zaidi ya mapambano yote yaliyowahi kufanyika
nchini Namibia.
Pambano hili litawakutanisha pia baadhi ya mabondia
kadhaa katika mapambano ya awali ambako bondia Martin Haikali wa Namibia
atakutana na Nelson Banda wa Zambia katika mpambano wa raundi 8.
TAIFA STARS YAENDELEA KUJIFUA KUISUBIRI MOROCCO
Kocha wa makipa, Juma Pondamali akimnoa Cassilas |
Nazuia hivi! |
Kim Poulsen (kushoto) akiwashuhudia vijana nwake wanavyojifua |
Mwinyi Kazimoto akichuana na mwenzake |
Makipa Juma Kaseja na Hussein Sharrif 'Cassilas' wakijifua |
Salum Abubakar akimiliki mpira huku akichungwa na mabeki wakiwa mazoezini |
Wachezaji waliowasili ni wa Yanga, Simba, Mtibwa na Azam ambao walifungiwa kwa tuhuma za kuhujumu timu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba.
Timu hii ipo kambini kujianda na mchezo dhidi ya Morocco utakaochezwa Jumapili kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen amesema mazoezi yanaendelea vizuri na wachezaji wana ari hivyo anaamini watashinda mchezo wao dhidi ya Morocco.
Pia amesema wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu watawasili kesho alfajiri tayari kujiunga wenzao kwa mazoez.
Stars inahitaji ushindi katika mechi hiyo ili kuendelea kuifukuzia Ivory Coast wanaoongoza kundi lao la C kwa pointi 4 ambapo mwishoni mwa wiki nao watakuwa uwanjani kuumana na Gambia.
Tanzania ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 3 kutokana na kucheza mechi mbili ikipoteza moja na nyingine kuilaza Gambia, hukui Morocco wakiwafuata nyuma wakiwa na pointi 2 iliyopata kwa sare mbili, huku Gambi wakishikilia mkia na pointi yao moja japo nayo imecheza mechi mbili.
Rage awashtaki waliofanya 'mapinduzi' Simba
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage |
Na Boniface Wambura
UONGOZI wa klabu ya soka ya Simba umewapeleka kwa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wanachama wake waliotangaza mapinduzi klabu hayo katika mkutano walioitisha juzi jijini Dar es Salaam.
Uongozi huo wa Simba chini ya Mwenyekiti wake wameamua kupelekea mashtaka hayo TFF kuonyesha kutokubaliana na maamuzi yaliyofanywa na wanachama hao waliotangaza kuung'oa uongozi wote wa Simba na kuunda kamati maalum.
TFF imethibitisha kupokea barua kutoka uongozi wa
Simba ikielezea kutotambua mkutano ulioandaliwa na wanaodaiwa kuwa
wanachama wake na kufanyika jana ukumbi wa Starlight, Dar es Salaam.
Vilevile
katika barua hiyo uongozi wa Simba umeahidi kuitisha mkutano wa
wanachama wake. Mkutano huo utaitishwa na Mwenyekiti wa Simba kwa mujibu
wa katiba ya klabu hiyo.
Kutokana
na hali hiyo, TFF imeitisha mara moja kikao cha Kamati ya Sheria,
Maadili na Hadhi za Wachezaji kinachoongozwa na Wakili Alex Mgongolwa
kwa ajili ya kutoa mwongozo kwa matukio ya aina hiyo.
Hata
hivyo, TFF tunasisitiza kwa wanachama wetu ikiwemo Simba kuwa wanachama
wanapotaka kufanya uamuzi wowote ule wanatakiwa kuzingatia katiba na
kanuni zilizopo.
Subscribe to:
Posts (Atom)