STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, March 19, 2013

Simba yawananga wanaoikejeli haina fedha

Msemaji wa klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga
KLABU ya soka ya Simba imetoa ufafanuzi juu ya tuhuma zilizotolewa na baadhi ya wanachama kwamba Simba haina fedha ndiyo maana wameamua kuzunguka mikoani kucheza wakati wakielekea Kagera kuuamana na wenyeji wao, Kagera Sugar.
Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga aliandika katika wall yake ya Facebook, akifafanua tuhuma hizo na kueleza namna uongozi wa Simba unavyowahudumia wachezaji wao tofauti na kejeli zinazotolewa.
Kamwaga alianza kwa kuandika; Nauli ya bei nafuu kabisa kutoka Dar-Luanda-Dar ni dola 1000 kwa kichwa. Simba imekwenda Angola pasipo kutembeza bakuli kwa mtu. 
Na wote waliosafiri wakalipwa posho kwa USD (si kwa fedha za madafu). Fedha hizo ni mara kumi ya zile ambazo wachezaji walikuwa wakilipwa miaka minne hadi sita iliyopita wakiwa safarini na Simba.... Leo inazushwa kwamba eti Simba haina fedha za kwenda Kagera ndiyo maana inapita Dodoma, Tabora, Shinyanga kucheza ndondo!!!!!! Inachekesha. 
Gharama ya mafuta, kwa sababu Simba ina basi lake, haifikii hata nauli ya mtu mmoja kwenda Angola... Sasa vije leo isemwe eti Simba haina fedha za kwenda Mwanza? Yaani za kwenda Angola zipo ila za Mwanza hakuna? Kuna sababu kubwa mbili kwanini timu inakwenda Kagera TARATIBU. 
Mosi, zaidi ya nusu ya wachezaji waliosafiri wanatoka TIMU B na wengine hawajawahi kufundishwa na Patrick Liewig. Benchi la ufundi liliona ni vema hawa wapate nafasi ya kujaribiwa katika mechi ya kirafiki ili wajue kocha anahitaji nini na kocha awafahamu zaidi wachezaji wake. 
Ikumbukwe pia, kiufundi, Simba haikutakiwa kuwa na mechi kwa wiki zaidi ya mbili kutokana na ratiba iliyozingatia ushiriki wake kwenye Ligi ya MABINGWA. Hiyo ni sababu ya kiufundi. Kuna sababu ya 2 ambayo ni ya kimantiki. Kwamba Simba ni klabu ya Watanzania wote na si wale walioko Dar es Salaam na mikoa yenye timu za Ligi Kuu. 
Kuna mikoa kama Tabora ambayo Simba haijacheza kwa takribani miaka 10 lakini wapo Wana Simba ambao wangependa kuiona. Vivyo hivyo kwa Shinyanga ambapo tulipata sapoti kubwa sana tulipokwenda mwaka jana. Tunahitaji kuwafurahisha wapenzi wetu wa kona zote. 
Tunahitaji pia kutengeneza fan base kubwa zaidi hata kwa watoto ambao wataiona Simba ikicheza Tabora.... Mwaka jana tulipeleka Kombe letu katika baadhi ya mikoa. Mara baada ya kumalizika kwa ligi msimu huu, tuna mpango wa kwenda kwenye mikoa ambayo Simba haijakwenda kwa miaka mingi... 
Mikoa kama vile Rukwa, Kigoma, Singida, Mara, Iringa n.k... Jamani huko kote kuna washabiki wa Simba na watafurahi kuiona ikicheza mbele ya macho yao. TUNASUBIRI KWA HAMU pia tuambiwe tunaenda kucheza ndondo wakati huo ! 
Watu wanafikiri Man United inakwenda China kufanya mazoezi pekee!!!! Hapana, inakwenda kutangaza brand yake ili wapate pa kuuza merchandise yao... Tutakwenda kote itakakowezekana, INSHALLAH... 
Ili mradi Simba ikianza kufanya biashara huko tuendako, na wakati huo utafika tu, tusianze kuulizana tulimtumia MGANGA gani kufanya biashara ya merchandise yetu vizuri.... Hiki ndicho kile rafiki yangu John Shibuda huwa anakiita kwa maneno mawili tu; FIKRA MCHAKATO....

Mabondia nusura wazichape kavukavu kasi...!

Mabondia Immanuel “Prince” Naidjala  wa Namibia na Lesley Sekotswe wa Botswana wamekutana leo katika mkutano wa waandishi wa habari. Kukutana kwao nusura kulete balaa kubwa baada ya mabondia wenyewe kuingia midadi na kutaka kuzipiga kavu kavu mbele ya vyombo vya habari
                          Immanuel "Prince" Naidjala
 
Mkutano huo ulifanyika katika hotel ya Windhoek Country Club Resort ambayo ni moja ya Casino kubwa katika nchi ya Namibia. Vyombo mbalimbakl vya habari kutoka nchi za Afrika na Ulaya zilishiriki katika mkutano huo ambao wawili hao walitambiana kupeana mkongoto wa uhakika watakapokutana siku ya jumatano tarehe 20.


Mabondia hao wanakutana tena kesho tarehe 19 katika hoteli hii katika zoezi la kupima uzito kabla ya mpambano wao siku ya Jumatano ambayo ni siku ya Uhurru wa nchi ya Namibia. Viongozi wakuu wa serikali ya Namibia watahudhuria mpambano huo ambao ni mkubwa kuwahi kufanyika katika nchi hii yenye wakazi milioni mbili na ushee!

Naye Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi amewasili jijini Windhoek leo akitokea nchini Ghana kulisimamia pambano hili la ubingwa wa “IBF International Title”

Rais Ngowi ametokea jijini Accra, Ghana ambapo alishughudia mabondia Richard Commey na Bilal Mohammed wakitoana jasho ambako Richard Commey aliibuka kuwa bingwa wa uzito mwepesi katika bara la Afrika.

Promota wa mpambano huo Nestor Tobias wa kampuni maarufu ya Sunshine Boxing Promotions ana uhakika wa mpambano huu kuvunja rekodi ya kuingiza watu wengi zaidi ya mapambano yote yaliyowahi kufanyika nchini Namibia.

Pambano hili litawakutanisha pia baadhi ya mabondia kadhaa katika mapambano ya awali ambako bondia Martin Haikali wa Namibia atakutana na Nelson Banda wa Zambia katika mpambano wa raundi 8.

TAIFA STARS YAENDELEA KUJIFUA KUISUBIRI MOROCCO

Kocha wa makipa, Juma Pondamali akimnoa Cassilas

Nazuia hivi!

Kim Poulsen (kushoto) akiwashuhudia vijana nwake wanavyojifua

Mwinyi Kazimoto akichuana na mwenzake

Makipa Juma Kaseja na Hussein Sharrif 'Cassilas' wakijifua

Salum Abubakar akimiliki mpira huku akichungwa na mabeki  wakiwa mazoezini
JUMLA ya wachezaji 17 wa Taifa Stars wamewasili kambini  na kuanza mazoezi kwenyeuwanja wa Karume jijin Dar es Salaam.
Wachezaji waliowasili ni wa Yanga, Simba, Mtibwa na Azam ambao walifungiwa kwa tuhuma za kuhujumu timu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba.
Timu hii ipo kambini kujianda na mchezo dhidi  ya Morocco utakaochezwa Jumapili kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen amesema mazoezi yanaendelea vizuri na wachezaji wana ari hivyo anaamini watashinda mchezo wao dhidi ya Morocco.
Pia amesema wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu watawasili kesho alfajiri tayari kujiunga wenzao kwa mazoez.
Stars inahitaji ushindi katika mechi hiyo ili kuendelea kuifukuzia Ivory Coast wanaoongoza kundi lao la C kwa pointi 4 ambapo mwishoni mwa wiki nao watakuwa uwanjani kuumana na Gambia.
Tanzania ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 3 kutokana na kucheza mechi mbili ikipoteza moja na nyingine kuilaza Gambia, hukui Morocco wakiwafuata nyuma wakiwa na pointi 2 iliyopata kwa sare mbili, huku Gambi wakishikilia mkia na pointi yao moja japo nayo imecheza mechi mbili.

Rage awashtaki waliofanya 'mapinduzi' Simba

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage

Na Boniface Wambura
UONGOZI wa klabu ya soka ya Simba umewapeleka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wanachama wake waliotangaza mapinduzi klabu hayo katika mkutano walioitisha juzi jijini Dar es Salaam.
Uongozi huo wa Simba chini ya Mwenyekiti wake wameamua kupelekea mashtaka hayo TFF kuonyesha kutokubaliana na maamuzi yaliyofanywa na wanachama hao waliotangaza kuung'oa uongozi wote wa Simba na kuunda kamati maalum.
TFF imethibitisha kupokea barua kutoka uongozi wa Simba ikielezea kutotambua mkutano ulioandaliwa na wanaodaiwa kuwa wanachama wake na kufanyika jana ukumbi wa Starlight, Dar es Salaam.
Vilevile katika barua hiyo uongozi wa Simba umeahidi kuitisha mkutano wa wanachama wake. Mkutano huo utaitishwa na Mwenyekiti wa Simba kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.
Kutokana na hali hiyo, TFF imeitisha mara moja kikao cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kinachoongozwa na Wakili Alex Mgongolwa kwa ajili ya kutoa mwongozo kwa matukio ya aina hiyo.
Hata hivyo, TFF tunasisitiza kwa wanachama wetu ikiwemo Simba kuwa wanachama wanapotaka kufanya uamuzi wowote ule wanatakiwa kuzingatia katiba na kanuni zilizopo.