STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 15, 2013

Maiti yafukuliwa kaburini na kukatwa kichwa Geita

Picha hii haihusiani na kaburi lililofukuliwa Geita




WATU wasiofahamika huko Geita wamelifukua kaburi na mwanaume mmoja kisha kukata kichwa cha maiti yake na kutowekwa na kichwa hicho kusikojulikana.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia MICHARAZO, zinasema kuwa watu hao wanadaiwa kuyfanya unyama huo usiku wa kuamkia jana majira ya usiku kwa kulifukua kaburi la mtu huyo ambaye hakuweza kufahamika kisha kupasua sanduku alilozikiwa na kukata kichwa cha maiti hiyo na kutoweka na kichwa hicho.
Mashuhuda wanasema tukio hilo liligundulika jana wakati wachimba makuburi walipoenda katika makaburi hayo na kukuta kaburi hilo likiwa limefukuliwa na huku jeneza likiwa lipo juu yake likiwa limepasuliwa na walipoangalia ndani wakashangazwa kukutwa mwili huo ukiwa hauna kichwa.
Inaelezwa maiti hiyo ilizikwa miezi mitatu iliyopita na baadhi ya watu wamehusisha na vitendo vya kishirikina kwani silo jambo la kawaida maiti kufukuliwa kisha kukatwa kichwa hivi hivi tu.
Jeshi la Polisi mkoani Geita limethibitisha juu ya tukio hilo na kwamba wanafanya upelelezi juu ya watu waliohusika kufanya unyama huo.

Abdallah Juma haamini kafunga hat trick, apewa mpira tofauti na Tambwe

Abdallah Juma (kulia) alipokuwa Simba. Hii ni mechi moja wapo kati ta mbili anazodai alizitumikia katika Ligi ya msimu uliopita akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi.
MSHAMBULIAJI wa Mtibwa Sugar, Abdallah Juma, amesema bado haamini kama ni yeye aliyefunga 'hat-trick' juzi Jumapili hasa baada ya kutoka katika kipindi kigumu cha kutothaminiwa na klabu ya Simba, huku akibainisha kwamba alikabidhiwa uwanjani mpira wake baada ya kufunga magoli hayo matatu.
Mchezaji huyo alifunga mabao matatu wakati Mtibwa ilipoisambaratisha Oljoro JKT kwa magoli 5-2 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani na kuwa mchezaji wa kwanza mzawa kufanya hivyo tangu msimu wa 2010-2011.
Katika msimu huo, aliyekuwa mshambuliaji wa Polisi Dodoma, Juma Semsue alifunga mabao matatu na kuwa mchezaji pekee kufunga 'hat-trick' katika ligi kuu ya Bara kwa misimu miwili iliyopita.
Mrundi Amisi Tambwe wa Simba alizindua tukio hilo kwa kufunga mabao manne wakati walipoisambaratisha Mgambo JKT kwa magoli 6-0.
Juma alisema hadi sasa bado anashindwa kuamini kama ni kweli amefunga 'hat-trick' hiyo ya kwanza katika maisha yake ya soka kwa vile msimu uliopita alipokuwa na Simba hakupewa nafasi na alifikia kuanza kukata tamaa ya kucheza soka.
"Kwa kweli nimefurahishwa mno na pia najishangaa kama ndiye mimi yule yule ambaye nilipokuwa Simba sikuaminiwa na msimu mzima nilichezeshwa katika mechi mbili tu tena kwa muda usiozidi dakika 15," alisema. na kzuitamba mechi anazokumbuka aliichezeshwa ni ile dhidi ya African Lyon na JKT Ruvu.
Juma aliyewahi pia kung'ara na timu za AFC Arusha, Kagera Sugar na Ruvu Shooting, alisema kuaminiwa na kupewa nafasi na makocha wake ndiyo kulikomrejesha katika kiwango chake kilichowavutia Simba msimu mmoja uliopita.
"Kuaminiwa na makocha ndiyo siri ya kurejea kwa makali yangu, na huu ni mwanzo tu kwani kiu yangu ni kuendelea kufunga mabao ili nije kuitwa Taifa Stars," alisema.
Aliongeza kuwa tofauti na tukio la aibu la kunyimwa mpira lililomkumba Tambwe wa Simba baada ya kupiga 'hat-trick', yeye katika mechi yao ya juzi alikabidhiwa mpira wake uwanjani na mwamuzi mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo.
"Nashukuru mimi nilipewa mpira wangu," alisema.
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alitoa ufafanuzi wa tukio la Juma kupewa mpira wake uwanjani tofauti na ilivyokuwa kwa Tambwe akisema ilitokana na hekima ya mwamuzi wa mchezo huo.
"Tulishatoa ufafanuzi tangu mwanzo kwamba hakuna kanuni wala sheria ya jambo hilo zaidi ya kuwapa motisha wachezaji na hivyo alichokifanya mwamuzi huyo ni kwamba ametumia busara na inakubalika," alisema.

Safina wa Mizengwe aing'ata serikali sikio

Safina wa Mziengwe
MCHEKESHAJI mahiri wa kike anayetamba kupitia kipindi cha vichekesho cha Mizengwe, Jesca Kindole 'Safina' ameitaka serikali na wadau wa sanaa nchini kuongeza juhudi katika kudhibiti vitendo vya wizi wa kazi za wasanii ili kuwasaidia kunufaika na kazi zao.
Safina alisema mbali na sanaa kuwa moja ya ajira tegemeo kwa watu wengi, lakini kama ingetengenezewa mazingira mazuri ingeiwezesha serikali kuvuna pato la kutosha kuliko ilivyo sasa ambapo linaishia mikononi mwa wachache.
Msanii huyo alisema wasanii wengi wa Tanzania wanaishi kimaskini kutokana na kufanyiwa 'uharamia' na unyonyaji mkubwa, kitu ambacho imefika wakati serikali na wadau wanaosimamia fani hiyo kutoa makucha.
"Sanaa inalipa sana Bongo, ila wizi na unyonyaji uliopo unatufanya wasanii wengi kuishi maskini tofauti na jasho tunalolitoa, pia serikali inapoteza mapato mengi kupitia huko, sasa ni wajibu wao kuamka na kuikomalia," alisema.
Mchekeshaji huyo anayejiandaa kutoka na filamu ya 'Kijiji Chetu', alisema anaamini kama tasnia ya sanaa itatengenezewa mazingira mazuri, wasanii nchini wataishi maisha mazuri kama wa mataifa mengine.