STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 29, 2013

Bale, Ronaldo, Messi kuchuana tuzo ya FIFA's Ballon d'Or

Bale na Ronaldo
Zlatan Ibrahimovic

MCHEZAJI ghali kwa sasa Gareth Bale, ni miongoni mwa wachezaji 23 akiwamo Cristiano Ronaldo na Lionel Messi watakaowania Tuzo ya FIFA cha Mchezaji Bora Duniani  (FIFA's Ballon d'Or).
Aidha kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, Jose Morinho wa Chelsea na Alex Ferguson ni kati ya makocha watakaowania tuzo ya Kocha Bora wa Dunia wa FIFA.
Winga huyo (23) amejumuisha katika orodha ya awali ya watakaowania tuoz hiyo inayotolewa kila mwaka ambayo kwa sasa inashikiliwa na Messi.
Mkali huyo aliteua Real Madrid msimu huu akitokea Tottenham Hotspur, alivunja rekodi ya kuwa mchezaji mwenye uhamisho ghali akipiku rekodi ya Ronaldo kwa kunyakuliwa na Madrid atapigana kumbo na Mchezaji Bora wa Ulaya, Franck Ribery.
Orodha kamili iliyotangazwa na FIFA kuwania tuzo hiyo ni kama ifuatavyo;
Gareth Bale (Real Madrid), Edinson Cavani (Paris Saint-Germain), Radamel Falcao (Monaco), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Paris Saint-Germain), Andres Iniesta (Barcelona), Philipp Lahm (Bayern Munich), Robert Lewandowski (Borussia Dortmund), Lionel Messi (Barcelona), Thomas Muller (Bayern Munich), Manuel Neuer, (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Mesut Ozil (Arsenal), Andrea Pirlo (Juventus), Franck Ribery (Bayern Munich), Arjen Robben (Bayern Munich), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich), Luis Suarez (Liverpool), Thiago Silva (Paris Saint-Germain), Yaya Toure (Manchester City), Robin Van Persie (Manchester United), Xavi (Barcelona).
Orodha kamili ya makocha watakaochuana katika tuzo hizo za FIFA ni pamoja na  Carlo Ancelotti (Paris Saint-Germain), Rafael Benitez (Napoli), Antonio Conte (Juventus), Vicente del Bosque (Spain), Alex Ferguson (formerly Manchester United), Jupp Heynckes (formerly Bayern Munich), Jurgen Klopp (Borussia Dortmund), Jose Mourinho (Chelsea), Luiz Felipe Scolari (Brazil), Arsene Wenger (Arsenal)

Yanga kuvuna nini kwa Mgambo JKT, kazi ipo jijini Mbeya


WAKATI watani wao wa jadi Simba ikipokea kipigo cha kwanza kwa msimu huu mbele ya Azam, mabingwa watetezi Yanga jioni ya leo inatarajiwa kuvaana na Mgambo JKT katika mfululizo wa Ligi Kuu.
Yanga yenye pointi 19 itahitaji ushindi kwa Mgambo ili kujiweka pazuri katika msimamo wa ligi hiyo baada ya jana wapinzani wao wa jadi kuboronga na kuruhusu kipigo cha kwanza, lakini bado itakuwa ikiiombea Mbeya City isiendeleze wimbi la ushindi itakapoumana na Prisons kwenye uwanja wa Sokoine-Mbeya.
Ushindi wowote wa Mbeya City utamaanishja Yanga itasalia kwenye nafasi ya tatu ikiiengua Simba tu ambayo kwa sasa ipo nafasi ya pili.
Mbeya City ina pointi 20 sawa na Simba ila inazidiwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufunga na ushindi mbele ya Prisons iutaifanya walingane na Azam na kuendelea kukaa kileleni wakati Yanga ikishinda itafikisha pointi 22.
Hata hivyo Yanga tayari imetangaza wazi kuwa inachohitaji kwa sasa ni ushindi kwa mechi zake zilizosalia bila kujali kama itamaliza duru hilo katika nafasi ipi.
Mabingwa watetezi hao iliyosaliwa na mechi zake zote dhidi ya maafande wa JKT, ilikatishwa wimbi lake la ushindi Okti\oba 20 baada ya kulazimishwa sare ya mabao 3-3 na Simba.
Yanga pengine itataka kupata ushindi mnono kama ilivyofanya mtani wake wealipoitandika maafande hao mabao 6-0 huku Amissi Tambwe akitiupia kambani mabao manne pekee yake.
Ingawa kocha wa Mgambo, Mohammed Kampira alisema leo watashuka dimbani kwa nia ya kuidhibiti Yanga akiwategemea vijana wake wa U20.
Ukiondoa pambano la Dar, macho na masikio ya mashabiki wa soka yanaelekezwa jijini Mbeya kwenye pambano la kukata na nmundu baina ya wenyeji wa mkoa huo Mbeya City na Prisons.
Mbeya City iliyopanda daraja msimu huu inaonekana ndiyo kipenzi cha mashabiki wengi wa jiji hilo, huku Prisons ambao ni wazoefu wa ligi 'wakisuswa' kwa kile kinachoelezwa kuwa imezidi kulowea Dar, kitu ambacho leo inatarajiwa upinzani mkali baina ya timu hiyo na mgawanyo wa mashabiki.
Hiyo ni moja ya mechi tatu zinazochezwa leo nyingine ikiwa ni zile za maafande wa JKT Ruvu itakayokuwa ugenini dhidi ya Rhino Rangers kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Baada ya matokeo ya mechi za jana zilizoshuhudia Mtibwa Sugar wakikandamizwa mabaop 3-0 na Coastal Uinon, Ruvu Shooting na Kagera Sugar zikitoshana nguvuya kufungana bao 1-1 na Ashanti United kudinda ugenini dhidi ya Oljoro JKT, kuna mabadiliko katika msimamo huo kama inavyoonekana hapo chini.
Pia Kipre Tchetche aliyekuwa mfungaji wa mabao yote ya Azam jana wakati wakiizamisha Simba amekwea hadi nafasi ya tatu ya wafungaji bora akiwa na mabao sita, mawili pungufu na ya kinara aliyedhibitiwa, Amissi Tambwe.
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014    
                                   P    W   D   L    F    A   GD   PTS
01. Azam                    11   6    5   0   17   7    10    23
02. Simba                   11   5    5   1   21   10  11   20
03. Mbeya City          10   5    5    0   13   7   6     20
04. Yanga                   10   5    4    1   21  11  10   19
05. Ruvu Shooting      11   4    4    3    13  10  3    16
06. Kagera Sugar       11   4    4    3    11   8   3    16
07. Mtibwa Sugar       11   4    4    3   16  15  1    16
08. Coastal Union       11    3    6    2   10   6    4   15
09. JKT Ruvu             10    4    0    6     9   11 -2   12
10.Ashanti                  11    2    4    5    10  19 -9   10
11.Prisons                  10    1    5    4     5    12 -7    8
12.Rhino Rangers       10    1    4    5     8   15 -7     7
13.Oljoro                    11    1    4    6     8    16 -8    7
14.Mgambo                10    1    2    7     3    18 -15  5

Wafungaji:

8- Tambwe Amisi (Simba)
7- Elias Maguri (Ruvu Shooting), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Hamis Kiiza (Yanga)
6- Kipre Tchetche (Azam)
5- Tumba Sued (Ashanti Utd), Themi Felix (Kagera)
4- Didier Kavumbagu (Yanga), Peter Michael (Prisons), Jerry Santo (Coastal Union)
3- Jerry Tegete, Mrisho Ngassa (Yanga), Haruna Chanongo, Jonas Mkude (Simba), Bakar Kondo (JKT Ruvu), Themi Felix (Kagera), Paul Nonga (Mbeya City), Salum Machaku (JKT Ruvu), Jerry Santo (Coastal Union),
2- Haruna Moshi, Crispian Odulla (Coastal Union), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Mwagani Yeya, Jeremiah John (Mbeya City), Godfrey Wambura (Kagera Sugar), Shaibu Nayopa, Amir Omary (JKT Oljoro), Khamis Mcha (Azam), Shaaban Nditti (Mtibwa Sugar), Betram Mombeki, Ramadhani Singano (Simba), Said Dilunga (Ruvu Shooting)
1- Abdi Banda, Danny Lyanga (Coastal Union), Henry Joseph, Joseph Owino, Gilbert Kazze (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Frank Dumayo (Yanga), Iman Joel, Salum Majid, Mwalimu Musuku, Kamana Salum, Hussein Abdallah (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah,  Aggrey Morris,  John Bocco, Joseph Kimwaga, Faridi Maliki, Hamphrey Mieno, Salum Abubakar, Erasto Nyoni (Azam), Steven Mazanda, Richard Peter, Peter Mapunda, (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Shaaban Susan, Jerome Lembeli, Cosmas Ader  (Ruvu Shooting), Masoud Ally, Shaaban Kisiga (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma, Anthony Matangalu, Paul Maono(OG), John Matei, Mwinyi Ally (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga, Hamis Msafiri (Mgambo JKT), Seleman Kibuta, Daud Jumanne, Maregesi Marwa, Clement Douglas (Kagera Sugar), Paul Malipesa, Expedito Kidulo, Nurdin Mohammed, Fikiri Mohammed (Oljoro JKT)

Monday, October 28, 2013

Mwanajeshi mwingine wa Tanzania auwawa DR Congo, ashambuliwa na Waasi wa M23

Mwanajeshi anayedaiwa kuuwawa DR Congo
WATANZANIA wameendelea kupoteza ndugu zao wanaolinda amani katika mataifa ya nje baada ya taarifa za kwenye mtandao kueleza mwanajeshi aliyekuwa akihudumu katika Jeshi la Kulinda Amani MANUSCO huko DR Congo kuuwawa na waasi wa M23.
Taarifa hizo zinamtaja mwanajeshi huyo kuwa ni Rajab Ahmad Mlima aliyeshambuliwa kwa risasi wakati akijaribu kuwalinda wakazi wa mji wa Kiwanja na Ratshruru Kaskazini mwa mji wa Goma dhidi jeshi la  waasi hao wa M23.
Kifo cha mwanajeshi huyo kimekuja wakati watanzania wakiwa bado hawajasahau mashujaa wao waliouwawa Sudan Kusini na DR Congo hivi karibuni katika harakati za kulinda amani katika nchi hizo.
Mwenyezi Mung Ailaze mahali pema Peponi Roho ya mwanajeshi huyo. Ameen

Chelsea, Spurs zang'ara, Sunderland ikiona mwezi EPL

 
UZEMBE uliofanywa na kipa Joe Hart kutoka golini bila kuwasiliana na beki wake, Nastasic aliyekuwa akimrudishia mpira kwa kichwa, uliiwezesha Chelsea kupata bao lililowapa ushindi dakika ya lala salama na kukwea hadi nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya England.
Fernando Torres aliuwahi mpira uluioonekana kama unaelekea nje ya lango lililokuwa wazi la Man City na kuipatia timu yake bao muhimu na kushinda 2-1 kartika pambano lililokuwa kali lililochezwa uwanja wa Stamford Bridge.
Awali, Torres alitoa krosi nzuri kwa Schurrle aliyeifungia Chelsea bao la kuongoza katika dakika ya 32 lililodumu haidi mapumziko kabaal ya wageni kulirejesha dakika tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kupitia kwa Sergio 'kun' Aguero.
Katika mechi nyingine zilizochezwa jana, Tottenham iliendelea kufukuzia nafasi za juu baada ya kuinyuka 
Hull City kwa bao 1-0 lililofungwa na Roberto Saldado, nao wachovu wa ligi hiyo Sunderland waliwafunga wapinzani wao Newcastle United kwa mabao 2-1 ikiwa ndiyo ushindi wao wa kwanza msimu huu na timu za Swansea City na West Ham wakitoshana nguvu kwa kutoka 0-0.

Maskini Wema Sepetu! Afiwa na baba yake mzazi

STAA wa filamu na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amepatwa na msiba mzito baada ya baba yake mzazi Balozi Issac Abraham  Sepetu kufariki dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya TMJ Mikocheni jijini.
Inaelezwa kuwa, Balozi Sepetu alikuwa amelazwa katika hospital ya TMJ akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu sasa.
Hadi umauti unamkuta, Balozi Isaac Sepetu alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar na taarifa zilizopo ni kwamba anatarajiwa kuzikwa visiwani Zanzibar siku ya kesho.
Mtandao huu wa MICHARAZO MITUPU unaungana na Wema waombolezaji wote kumpa pole Wema Sepetu na familia nzima, ndugu na jamaa wa marehemu Balozi Zepetu na kuwaomba kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu kwa kukumbuka kuwa 'Sisi ni wa Mungu na kwake tutarejea. Mwenyezi Mungu, Aiweke Roho ya Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu, Mahala Pema Peponi. Ameen

Vitali Klitschko aitamani Ikulu ya Ukraine

BINGWA wa uzito wa juu wa WBC raia wa Ukraine, Vitali Klitschko anataka kufuata nyayo za bondia mwenzake, Manny Pacquiao wa Ufilipino kwa kujiingiza kwenye siasa, ila yeye anautaka Urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi wa 2015.
 
Manny Pacquiao pamoja na kuwa mbunge lakini pia anajishughulisha siasa ni mbunge wa Bunge la Ufilipino, hali ambayo imemvutia Klitschko ambaye mwezi Agosti alisema lengo kubwa ni kuifanya Ukraine kuwa nchi ya kisasa yenye maisha ya kiulaya.

Anasema ataamua na watu wenye mtazamo mmoja, ndoto zinazofanana na kuingia kwenye siasa na kutokea ndani kufanya mabadiliko.

Bondia huyo mwenye elimu ya udaktari kwa kusomea ambapo ana masta yake  ambayo alichukua baada ya kupata elimu ya juu ua utabibu wa binadamu.

King Class Mawe alivyomnyuka mpinzani wake Dar

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hassani Bandani wakati wa mpambano wao usio na ubingwa uliofanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala Dar es salaam King Class Mawe alishina kwa pointi mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi 


Bonia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akimshambulia kwa makonde Hassani Bandani wakati wa mchezo wao usio na ubingwa uliofanyika katika ukumbi wa panandi panandi King Class Mawe alibuka na ushindi wa point mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi
Ibrahimu Class akioneshwa mshindi baada ya mpambano kumalizika mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi 
KING CLASS MAWE AKIWA NA MMOJA YA MASHABIKI WAKE BAADA YA KUSHUKA ULINGONI
KING CLASS MAWE KWENYE POZI
Bondia Chalo Issa kulia akipambana na Amour Mzungu wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa panandi panandi ilala bungoni Mzungu alishinda kwa pointi mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi 
Bondia Shabani Kaoneka kulia akioneshana umairi wa kutupiana makonde na Halid Makwega wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa panandi panandi Kaoneka alishinda kwa pointi mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi 

Bondia Shabani Kaoneka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Halidi Makwega wakati wa mpambano wao Kaoneka alishinda mpambano huo mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi 
REFARII AKIMUONESHA MKONO JUU BONDIA SHABANI KAONEKA BAADA YA KUMDUNDA HALIDI MAKWEGA KWA POINT WAKATI WA MPAMBANO ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA PANANDI PANANDI ILALA BUNGONI DAR ES SALAAAM

Jamal Malinzi amrithi Tenga TFF, ambwaga Myamlani

KATIBU Mkuu wa zamani wa Yanga, Jamal Emil Malinzi, usiku wa kuamkia leo ameshinda Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akimrithi uongozi Leodger Tenga baada ya kupata kura 72, dhidi ya 52 za mpinzani wake Athumani Jumanne Nyamlani.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam, Walace Karia alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu wa Rais kwa kupata kura 67 akiwashinda Nassib Ramadhani kura 52 na Imani Madega sita.
1_3cebe.jpg
Raia anayemaliza muda wake, Leogder Tenga aliwa na Rais Mpya Mteule, Jamal Malinzi
Kwenye kinyang'anyiro hicho upande wa nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13 ilienda kwa kiungo wa zamani wa Simba Wilfred Kidau aliyepata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said kura 50, Omar Abdulkadir kura 10 na Alex Kabuzelia kura nne.
Kanda 12; Khalid Mohamed Abdallah amepata kura 69 na kumshinda Davis Mosha aliyepata kura 54.

Kanda ya 11 Geoffrey Nyange 'Kaburu' amepata kura 78 na kuwashinda Riziki Majala kura tano, Twahir Njoki kura mbili, Juma Pinto kura 26 na Farid Mbaraka kura 14, Kanda ya 10 ameshinda Hussein Mwamba aliyepata kura 63, huku Charles Komba akipata nne na Stewart Nasima 58.
Kanda ya tisa Othman Kambi aliyepata kura 84 yeye amewashinda Francis Bulame kura 30, wakati James
Mhagama aliyepata 93 amemshinda Zafarani Damoda aliyepata kura 11 na Kanda ya nane, Ngube Kiondo amepata kura 73 amemshinda Ayoub Nyaulingo kura 52.

Kanda ya Tano, Ahmed Iddi Mgoyi aliyepata kura 92 amemshinda Yussuf Kitumbo aliyepata kura 34, wakati Kanda Omar Walii Ali amepata kura 53 dhidi ya 19 za Ally Mtumwa. Eley Mbise amepata kura 51 dhidi ya 53 kura 57 za Lamanda Swai.
Mbasha Matutu aliyepata kura 63, amembwaga Vesastis Ligano aliyepata kura 61, wakati Vedastus Lufano aliyepata kura 51, amewashinda Jumbe Odesa Magati kura 11, Mugisha Galibona kura 24 na Samuel Nyalla kura 39 na Kanda namba moja, Karilo Samson hakuwa na mpizani akapita moja kwa moja.