STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 2, 2013

Tangulia Tabu Ley Rochereau, tutakukumbuka daima

Tabu :ley akiwa na Mbilia Bel
BRUSSELS, Ubelgiji
MWANAMUZIKI mkongwe wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Pascal Tabu Ley Rochereau, amefariki katika hospitali moja ya mjini Brussels.

Tabu Ley, alifariki juzi saa mbili usiku baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi. Alianza kuugua ugonjwa huo tangu 2008.

Meneja wa zamani wa mwanamuziki huyo, Mekansi Modero, ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani, amethibitisha taarifa za kifo cha Tabu Ley, baada ya kuthibitishiwa na ndugu wa karibu wa mkongwe huyo.

Mwanamuziki Nyboma Mwandido, anayeishi mjini Paris, Ufaransa pia amethibitisha taarifa za kifo cha mwanamuziki huyo mkongwe.

Tabu Ley alikuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa huo kwa muda mrefu na alikuwa akitembea kwa kutumia baiskeli maalumu kutokana na kushindwa kutembea kwa miguu.

Kifo cha Tabu Ley kimewapa simanzi kubwa mashabiki wa muziki barani Afrika, kutokana na kuwa mmoja wa watu mahiri, ambaye nyimbo zake zilikuwa na mvuto wa aina yake.

Katika miaka ya hivi karibuni, Tabu Ley aliamua kuachana na muziki na kujitosa katika masuala ya siasa, baada ya kuteuliwa kuwa waziri katika serikali ya Rais wa zamani wa DRC, Laurent Kabila mwaka 1997

Awali, Tabu Ley alilazimika kuikimbia DRC na kwenda kuishi uhamishoni nchini Ubelgiji kutokana na kutoelewana na rais wa zamani wa nchi hiyo, marehemu Mobutu Sese Seko.

Kabla ya kwenda Ubelgiji, Tabu Ley aliishi kwa muda nchini Ufaransa akipatiwa matibabu ya ugonjwa huo. Baada ya hali kuanza kuwa mbaya, alihamishiwa Ubelgiji kwa ajili ya kupatiwa matibabu maalumu.

Enza za uhai wake, Tabu Ley alikuwa akichuana vikali na wakati nyota wa DRC wa wakati huo kama vile Joseph Kabasele, Nicolas Kasanda na Rwambo Lwanzo Makiadi 'Franco'.

Alianza kujihusisha na muziki 1959 akiwa mtunzi, mwimbaji na mcheza shoo akiwa katika bendi ya African azz, iliyokuwa ikiongozwa na Kabasele. Mkongwe huyo amerekodi na kuimba nyimbo zaidi ya 2,000 na kutoa albamu 250.

Alizaliwa 1940 katika mji wa Bandundu nchini DRC. Alianza maisha akiitwa Pascal Tabu. Akiwa na umri wa miaka 14, aliandika wimbo wake wa kwanza Bessama Muchacha,  ambao aliurekodi na kundi maarufu la African Jazz, lililokuwa chini ya Kasebele, (asichanganywe na Pepe Kalle).

Aliendelea na shule na hatimae alipomaliza sekondari 1959, ndipo alipojiunga rasmi na African Jazz.

Alikuwa mmoja wa wanamuziki walioimba wimbo Independence Cha Cha, wa Grande Kalle, uliotikisa anga la Afrika miaka ya 1960. Wimbo huo ukawa rasmi wa kusherehekea uhuru wa DRC.

Baada ya miaka minne, alijiengua katika kundi la African Jazz. Akiwa na mpiga gita mahiri, Nicholaus Kassanda, wakaanzisha kundi la African Fiesta, ambalo alidumu nalo hadi 1965.

Wakati DRC ikiwaka moto kimuziki na ushindani kuwa mkali, aliamua kuachana na  Nico na kuanzisha kundi lake la African Fiesta National au mara nyingine ikiitwa Africa Fiesta Flash na kurekodi kibao maarufu cha Afrika Mokili Mobimba, ambacho kilivuka mauzo ya nakala milioni moja miaka ya 1970 na kuiingiza bendi hiyo kuwa kati ya bendi zilizopata mafanikio ya juu katika Afrika kwa wakati huo.

Wanamuziki kama Papa Wemba na Sam Mangwana ni miongoni mwa wakongwe waliowahi kupitia katika kundi hili tishio.

Mwaka 1970, Tabu Ley alianzisha bendi ya Orchestre Afrisa International. Wakati huo Afrisa na TPOK Jazz, ndizo zilizokuwa bendi maarufu zaidi Afrika. Afrisa waliteremsha vibao kama Sorozo, Kaful Mayay, Aon Aon na Mose Konzo.

Kutokana na umahiri wake, Tabu Ley aliweza kupata tuzo kutoka serikali za nchi kama Chad, iliyompa heshima ya 'Officer of The National Order' wakati Senegal ilimpa heshima ya 'Knight of Senegal' na akawa sasa anaitwa Siegneur Rochereau.

Katikati ya miaka ya 1980, Tabu Ley aligundua kipaji cha mwanamama aliyekuja kutikisa anga za Afrika, Mbilia Bel. Baadae Tabu Ley alimuoa Mbilia, wakapata mtoto mmoja.

Nyimbo kama Nadina, Nakei Nairobi zinaonyesha kipaji gani alikuwa nacho mwanamama huyo, aliyekuwa mzuri kwa sura, aliyejua pia kucheza na kutawala jukwaa vizuri.

Mwaka 1988, Tabu Ley akagundua kipaji cha mwimbaji mwingine wa kike, Faya Tess. Hapo Mbilia akaacha bendi na kuendelea na maisha yake ya muziki peke yake. Katika kipindi hicho, mtindo wa Soukus uliokuwa na mapigo yenye mwendokasi zaidi ya ile ya rumba ya Afrisa na TP OK Jazz, ulianza kuzishika nyoyo za vijana, bendi hizi kubwa zikaanza kufifia.

Mwanzoni mwa miaka ya 1990, Tabu Ley, alihamia Marekani, akawa anaishi Kusini mwa California na kubadili  muziki wake katika kujaribu kujikita zaidi katika soko la kimataifa.Akatunga nyimbo kama Muzina, Exil Ley na Babeti Soukous.

Mwaka 1996, Tabu Ley, alishiriki katika album ya kundi la Africando, akiimba wimbo wa Paquita, ambao aliurekodi miaka ya 1960, akiwa na African Fiesta.

Tabu Ley alipata cheo cha uwaziri katika utawala wa Kabila baada ya kuondolewa kwa Mobutu. Hata baada ya kifo cha Kabila, 2005, alipewa cheo cha gavana.

Mwaka 2006,  Tabu Ley,  alishirikiana na rafiki yake wa  muda mrefu, Maika Munah na kurekodi album yake ya mwisho, iliyoitwa Tempelo. Katika albumu hiyo, binti yake, Melodie aliimba nyimbo kadhaa.

Inaelezwa kuwa mkongwe huyo ameacha zaidi 54 kutoka kwa wanawake 36 aliozaa nao kwa nyakati tofauti.

Dk Kitila majanga matupu, avuliwa cheo kingine kisa...!



KUNA taarifa zinasema kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) umemvua kwa muda Mhadhiwa Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo madaraka ya kuongoza Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam (DUCE).

Hatua hiyo inatajwa kuchukuliwa baada ya uongozi wa UDSM kupata taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa Dk Kitila Mkumbo alikuwa kiongozi wa chama cha siasa, CHADEMA wakati angali ni mtumishi wa umma, jambo ambalo Uongozi wa chuo hicho umekariri kuwa ni kinyume cha sheria ya nchi na Serikali kwa mfanyakazi wa umma kushika wadhifa katika chama cha siasa.

Kutokana na uamuzi wa chuo hicho, Dk Kitila aliandikiwa na kukabidhiwa barua ya kusimamishwa kwake wadhifa huo.

Dk Kitila bado ataendelea kuwa Mhadhiri Mwandamizi kwenye kitivo hicho.

Wanawake wawili wanaswa na 'Unga' uwanja wa KIA

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz
Jeshi la Polisi  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), linawashikilia wanawake wawili ambao ni wafanyabiashara wa kigeni kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha kilo 12.7 za dawa za kulevya maarufu kama 'unga'.

Hilo ni tukio la pili katika muda usiozidi siku saba kwa raia wa kigeni kukamatwa na dawa hizo katika uwanja huo, ikiwa ni wiki mbili  tangu Waziri wa Uchukuzi, Dk.

Harrison Mwakyembe, atishie kuwafukuza kazi maofisa wa idara za usalama watakaobainika kujihusisha na biashara hiyo  kupitishwa katika uwanja huo.

Watuhumiwa hao waliokamatwa ni jana alfajiri katika uwanja huo ni Josiane Dede Creppy (25), raia wa Togo na Grace Teta (34), raia wa Liberia ambao kwa nyakati tofauti, mmoja akijiandaa kuelekea jijini Accra, Ghana na mwingine nchini Afrika Kusini.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, aliiambia NIPASHE jana kwamba mtuhumiwa  Grace alikamatwa akiwa na kilo 10.5 za dawa hizo wakati  akisafiri kwa ndege ya Shirika la Precision Air kutoka KIA kwenda Captown nchini Afrika Kusini kupitia Nairobi, Kenya.

“Huyu alikamatwa na unga unaoaminika kuwa ni dawa za kulevya alfajiri ya saa 10:45 akitumia hati ya kusafiria yenye namba 1039080 ikimuonyesha ni mfanyabiashara na raia wa Liberia. Josiane    alikamatwa saa 8:50 alfajiri akiwa na kilo 2.2 za dawa hiyo akiwa anataka kuondoka na ndege ya Shirika la Ethiopia kelekea Ghana,” alisema Kamanda Boaz.

Hata hivyo, alisema hadi sasa Polisi hawajatambua thamani halisi ya dawa hizo na aina ya dawa hizo kwa kuwa kazi hiyo iko chini ya Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya cha Jeshi la Polisi ambaye anazipeleka kwke kwa ajili ya uthamini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Kamishna Mwandamizi, Godfrey Nzowa, alisema polisi wanazifanyia uchunguzi dawa hizo ili kubaini aina yake na thamani halisi.

“Tunazifanyia uchunguzi hata zile zilizokamatwa hivi karibuni nazo bado tunazichunguza ili tujue ni aina gani, baada ya hapo tutawapa taarifa iliyokamilika,” alisema.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, raia wa Nigeria, Chubuzo John alikamatwa na kilo nne za dawa hizokatika uwanja huo,  wakati akitaka
kuondoka kwa ndege ya Shirika la Ethiopia kuelekea Roma nchini Italia.

Polisi imeahidi kumfikisha mtuhumiwa huyo mahakamani leo baada ya kupata jalada la mashtaka kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akiwa Kia katika ziara ya kushtukiza wiki mbili zilizopita, Dk. Mwakyembe aliwaonya maofisa wa idara za usalama pamoja na maofisa wengine uwanjani hapo, kutougeuza uwanja  huo kuwa uchochoro wa kupitisha dawa za kulevya huku akitishia kuwafukuza kazi maofisa uhamiaji watakaobainika kujihusisha na biashara hiyo haramu.

CHANZO: NIPASHE

Katibu Chama cha Madaktari ajiuzulu na kutua CHADEMA

Aliyekuwa Katibu Mkuu na baadaye President-Elect wa Chama cha Madaktari Tanzania, MAT, Dk Rodrick Kabangila ametangaza rasmi kujivua na kujiudhulu nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho cha kitaaluma, na kutangaza kujinga rasmi na chama cha siasa, CHADEMA.

Katika taarifa iliyooneshwa na runinga ya Star-Tv, Dk Kabangila amesema kuwa kwa mujibu wa sheria, imembidi kuamua kufanya lililo sahihi na sasa amejiunga rasmi ili kupata wigo mpana wa kupigania maslahi ya fani, madaktari na wananchi.

Chelsea yaendeleza mauaji England


CHELSEA imeendelea kugawa dozi kwa wapinzani wake katika Ligi Kuu ya England baada ya usiku wa jana kuinyoa Southampton anayochezea Mkenya, Victor Wanyama kwa kuilaza mabao 3-1. 
Chelsea ilitanguliwa kufungwa na wapinzani wao kabla ya kuamka na kurejesha mabao hayo na kuzidi kuikaribia Arsenal iliyopo kileleni ambayo msimu huu imekuwa moto wa kuotea mbali.  
Mabao yalifungwa na Cahil, John Terry na Demba Ba yalitosha kumfanya kocha Jose Mourinho kupata furaha.
Kutokana na ushindi huo Chelsea imekwea nafasi ya pili ikiipita Liverpool iliyoangushiwa kipigo jana chja mabao 3-1 toka kwaHull City







Bondia Chisora amkung'uta mtu KO

Mchezo umeisha! Bondia Ondrej Pala akiwa ameegemea kamba kujiepusha na kipigo zaidi kwa Dereck Chisora raundi ya tatu katika pambano la ngumi uzito wa juu lililofanyika kwenye ukumbi wa Copper Box Arena, London, Uingereza usiku wa kuamkia leo. Chisora alikuwa anatetea taji lake la WBO Intercontinental wakati taji la WBA International lilihusishwa pia.
Game opponent: Ondrej Pala was an ambitious challenger until the third-round stoppage came
Ondrej Pala wa Jamhuri ya Czech alipambana hadi raundi ya tatu aliposalimu amri kwa Knockout (KO), hilo linakuwa pambano la nne mwaka huu Chisora kushinda, likiwemo lile la ubingwa wa Ulaya alilotwaa September kwa kumpiga Edmund Gerber raundi ya pili.
Going toe-to-toe: Dereck Chisora's impressive chin again proved reliable against any big punches thrown
Dereck Chisora akimuadhibu mpinzani
Fighting back: But even in the earlier stages, it appeared Dereck Chisora's greater class would tell
Covering up: Dereck Chisora (right) also took several big shots from his Czech opponent
Dereck Chisora naye alipokea mikono kadhaa ya mpinzani kutoka Czech
All smiles: Dereck Chisora and promoter Frank Warren (right) know 2013 has been a good year for the fighter
Dereck Chisora na promota Frank Warren (kulia) wakifurahia mafanikio ya mwaka 2013