STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 11, 2014

Wigan yaichimba mkwara Arsenal

MABINGWA watetezi wa Kombe la FA, Wigan Athletic wamesema hawatakuwa tayari kuona kombe hilo likitoweka mikononi mwao hususan watakapocheza mechi ya nusu fainali dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Wembley Jumamosi.
Wigan iliutwaa ubingwa huo msimu uliopita baada ya kuifunga Manchester City katika mechi ya fainali.
Hull City, ambayo haijawahi kufika nusu fainali, huku ikitinga hatua hiyo baada ya miaka 85 iliyopita, itacheza nusu fainali nyingine dhidi ya Sheffield United Jumapili.
Arsenal itavaana na watetezi hao wa FA wakiwa wanauguza kipigo cha aibu walichopewa na Everton katika pambano lao la mwisho la Ligi Kuu ya England dhidi ya Everton waliowatambia kwa kuwalaza mabao 4-0

Rooney katuponza kwa Bayern-MOyes

Wayne Rooney
KOCHA David Moyes amekiri kwamba alifanya makosa makubwa kumharakisha Wayne Rooney kurejea uwanjani katika kikosi cha Manchester United kilicholala 3-1 dhidi ya Bayern Munich katika mechi yao ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya England, ambaye aliumia wiki iliyopita, alipasishwa kuchukua namba yake katika kikosi cha kwanza cha Man U, lakini hakuweza kuwasaidia Mashetani Wekundu wasikumbane na kipigo hicho kwenye Uwanja wa Allianz Arena.
"Kuna wakati nilihisi kwamba anashindwa hata kupiga mpira lakini yeye ni mchezaji muhimu sana kwetu," Moyes aliwaambia waandishi wa habari. "Sikujiwa na fikra kwamba tumeshatoka mchezoni, daima niliamini kwamba tulikuwa na nafasi ya kusonga mbele.
"Ilipokuwa 2-1 tulihitaji kufunga moja ili tuwe 2-2, lakini mambo hayakutuendea vyema. Nadhani ilikuwa ni kukosa bahati kulikotufanya tukafungwa bao lile la tatu.”

Ruvu Star sasa wana Kioo na Facebook

Rogart Hegga 'Katapila' mmoja wa viongozi na waimbaji wa Ruvu Star
BENDI ya muziki wa dansi ya Ruvu Stars ya Mlandizi Pwani wapo studio kwa ajili ya kumalizia nyimbo zao tatu za mwisho kukamilisha albamu ya kwanza.
Mmoja wa viongozi wa bendi hiyo, Rogart Hegga 'Katapila' alisema nyimbo hizo zimetungwa na waimbaji watatu tofauti ukiwamo unaitwa 'Kioo' ambao ni utunzi wa kiongozi mkuu wao, Khamis Kayumbu 'Amigolas'.
Alizitaja nyimbo mbili za mwisho kuwa ni 'Chewa Original' wa Seleman Muhumba na 'Facebook' wa Mkuu wa Jukwaa, Victor Mkambi ambaye pia ni mpapasa kinanda mahiri nchini.
"Tunamalizia nyimbo zetu tatu za mwisho kukamilisha albamu kabla ya kuanza maandalizi ya uzinduzi wa bendi na albamu hiyo, pia tumesaini mkataba na kampuni ya kurekodi video ya albamu hiyo."
Aliongeza, video hiyo inatarajiwa kuanza kurekodiwa wiki ijayo kwa  nyimbo tatu za awali ambazo ni; 'Spirit' alioutunga yeye (Hegga), 'Network ya Mapenzi' wa Toto Tundu na 'Jua Kali' wa Kuziwa Kalala.
"Video hiyo itaanza na nyimbo za awali tulizotambulisha kwa mashabiki na tukimalizia hizi tunazorekodi tutahimisha albamu na ndipo mipango ya uzinduzi," alisema.
Alisema bendi yao ipo hatua ya mwisho kabla ya kuanika ratiba ya maonyesho yao kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka itakayoptangazwa muda wowote kuanzia leo ili mashabiki wao wakae tayari kuwapokea.