STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 18, 2014

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kuanza Mei 10

LIGI ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) itakayochezwa kwa ligi ya mkondo mmoja katika vituo vitatu vya timu tisa kila kimoja inatarajia kuanza Mei 10 mwaka huu.
Timu ya kwanza kutoka katika kila kituo ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015. Kwa vile ligi hii haina mdhamini, hivyo timu zitajigharamia kwa kila kitu.
Vituo vitakavyotumika kwa ajili ya RCL, kanuni pamoja na ratiba vitatangazwa kabla ya kuanza kwa ligi hiyo. Pia kituo kitakachoteuliwa kwa ajili ya ligi hiyo, timu yake haitapangwa katika kituo husika ikiwa ni moja ya njia ya kuhakikisha kanuni ya mchezo wa kiungwana (fair play) inazingatiwa

Ronaldo kuivaa Bayern Munich

Ronaldo
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ana matumaini ya kurejea Jumanne dhidi ya Bayern Munich katika mechi yao ya kwanza ya nusu fainali. "Nina furaha sana. Nilitaka kucheza na kuisaidia timu (dhidi ya Barcelona) lakini wachezaji wenzangu walifanya kazi nzuri. Nazidi kuwa fiti sasa, sisikii maumivu yoyote. Huenda nikarejea dhidi ya Bayern au katika mechi ya marudiano nao."
Mwanasoka Bora huyo wa FIFA, alikosa michezo kadhaa ikiwamo wa Fainali ya Kombe la Mfalme wakati Real Madrid ikiizamisha Barcelona kwa kuifunga mabao 2-1, huku yeye akiwa jukwaani kabla ya kujumuika pamoja klushangilia taji hilo.

Dominic Nyamisana kuzihukumu Simba, Yanga kesho Taifa

Yanga

Simba
MWAMUZI Dominic Nyamisana kutoka mkoani Dodoma ndiye anayetarajiwa kuchezesha mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga wakati wakifunga msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga itashuka uwanjani ikiwa imeshakata tiketi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika yatakayofanyika mapema mwakani.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Nyamisana atasaidiwa na John Kanyenye kutoka Mbeya na Jesse Erasmo wa Morogoro.
Mbali na klabu hizo kongwe, pia timu nyingine 14 zinazoshiriki ligi hiyo  zitashuka kwenye viwanja tofauti hapa nchini kusaka pointi tatu muhimu.
Mabingwa wapya wa ligi hiyo, Azam ya jijini yenyewe itashuka kwenye Uwanja wa nyumbani Azam Complex kuwakaribisha JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani.
Timu ya Rhino Rangers kutoka mkoani Tabora tayari imeshashuka daraja huku mchezo kati Ashanti United na Prisons ya Mbeya zitakazocheza mechi yao kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, ukitarajiwa kuamua timu itakayoshuka daraja.
Prisons inahitaji sare yoyote ili kubaki Ligi Kuu, wakati Ashanti ushindi pekee ukiwa ndiyo tiketi yake ya kuonekana tena katika ligi hiyo msimu ujao.

Diamond ateuliwa kuwania tuzo 2 MTV

Diamond
NYOTA wa muziki wa Bongofleva, Diamond Platnumz ameendelea kuchana anga la Afrika katika muziki baada ya kutajwa kuwania tuzo mbili za MTV ikiwamo kubwa zaidi ya Msanii Bora wa Kiume Afrika.
Katika majina ya wanaowania tuzo hizo za MTV Africa Music Awards (MAMA) yaliyotangazwa juzi, Diamond anawania tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika na pia tuzo ya Wimbo Bora wa Ushirikiano (Number One remix) alioufanya na Davido wa Nigeria.
Katika tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika, Diamond anachuana na mshirika wake Davido, pamoja na Anselmo Ralph (Angola), Donald (Afrika Kusini) na Wizkid wa Nigeria.
Diamond na Amani wa Kenya wamekuwa wasanii pekee wa kujitegemea kutoka Afrika Mashariki na Kati kuingia kuwania tuzo hizo, wakati Sauti Sol kutoka Kenya wameingia kuwania tuzo ya Kundi Bora Afrika.
Mafikizolo na Uhuru kutoka Afrika Kusini wanaongoza kuwania tuzo nyingi (4) sawa na Davido, ambaye anawania pia wimbo bora wa Mwaka, Msanii Bora wa Mwaka na Wimbo wa Ushirikiano.
Katika tuzo ya Wimbo Bora wa Ushirikiano, Diamond na Davido wanachuana na Amani ft Radio & Weasel – ‘Kiboko Changu’ (Kenya/Uganda, Mafikizolo ft May D – ‘Happiness’ (Afrika Kusini/Nigeria), R2bees ft Wizkid – ‘Slow Down’ (Ghana/Nigeria) na
Uhuru ft DJ Buckz, Oskido, Professor, Yuri Da Cunha – ‘Y-tjukutja’ (Afrika Kusini/Angola).
Nyota wa timu ya soka ya Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure anawania tuzo isiyohusiana na muziki ya 'Personality of the Year' akichuana na muigizaji Mkenya aliyeshinda tuzo ya Oscar, Lupita Nyong’o na muigizaji Mnigeria Omotola Jalade
Upigaji wa kura za kuwachagua washindi ulianza Jumatano hadi Juni 4, 2014 usiku kupitia www.mtvbase.com.
Diamond amewashuruku mashabiki wake na kuwaomba wampigie kura ili ailetee heshima Tanzania.

Thursday, April 17, 2014

Hawa ndiyo wana Hip Hop wenye mkwanja mnene 2014

JARIDA maarufu la Forbes imetoa orodha ya wasanii wasanii watano wa Hip Hop matajiri zaidi 2014. 
Sean 'Diddy' Combs (P Diddy) ndiye anayeongoza katika orodha hiyo kwa kuwa msanii tajiri zaidi wa Hip Hop 2014 kwa mujibu wa Forbes.

Utajiri wa Diddy unakadiriwa kuwa dola milioni 700, ikiwa imeongezeka dola milioni 120 kutoka mwaka jana huku vyanzo vya utajiri wake vikitajwa kuwa ni Revolt TV/Diageo’s Ciroc.
Anayefuatia katika nafasi ya pili ni producer Andre Young aka Dr. Dre ambaye ana utajiri unaofikia dola milioni 550. 

Utajiri wake umetokana na mauzo ya headphones za Beats by Dr. Dre.
Hawa ndio wasanii Matajiri wa5 wa Hip Hop kwa mwaka 2014
Nafasi ya tatu imeshikwa na Shawan Carter aka Jay Z, kwa utajiri wa dola milioni 520 huku vyanzo vya utajiri huo vikitajwa kuwa Rocawear Sale/Live Nation/Roc Nation.
Nafasi ya nne imekamatwa na Bryan Williams aka Birdman, huku utajiri wake ukitokana na Cash Money/YMCMB/GT Vodka.
Wa mwisho katika orodha hiyo aliyeshika nafasi ya tano ni Curtis Jackson aka 50 Cent, mwenye utajiri wa dola miliono 140, vyanzo vyake vikitajwa kuwa ni Vitamin Water/SMS Audio/SK Energy.
 
The Forbes Five: Hip-Hop’s Wealthiest Artists 2014
1.Sean “Diddy” Combs | $700 Million | Revolt TV/Diageo’s Ciroc
2.Andre “Dr. Dre” Young” | $550 Million | Beats by Dr. Dre Headphones
3.Shawn “Jay Z” Carter | $ 520 Million | Rocawear Sale/Live Nation/Roc Nation
4.Bryan “Birdman” Williams | Cash Money/YMCMB/GT Vodka
5.Story kamili ya orodha hii itatoka katika toleo la May la jarida la Forbes.

16 kambi ya Maboresho waula Taifa Stars

Na Mwandishi Wetu, Mbeya
JUMLA ya wachezaji 16 wa kikosi cha Maboresho ya Timu ya Taifa(Taifa Stars) wamechaguliwa kujiunga na timu ya Taifa kwa ajili ya mechi za kirafiki kutoka kambi ya wachezaji 34 iliyokuwa Chuo cha Ualimu Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Kikosi hicho  kimetangazwa leo na Kocha Msaidizi, Salum Mayanga, aliyekuwa na timu hiyo katika Mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hill View iliyopo jijini Mbeya.
Mayanga aliwataja wachezaji hao kuwa ni Mlinda mlango Benedict Mlekwa kutoka Mara, Walinzi wa kati ni Emma Simwanda kutoka Temeke na Joram  Mgeveja kutoka Iringa.
Walinzi wa pembeni ni Omari Kindamba wa Temeke, Edward Mayunga wa Kaskazini Pemba na Shirazy Sozigwa wa Ilala, viungo ni Yusufu Mlipili, Said Juma Ally kutoka Mjini Magharibi, Abubakar Mohamed wa Kusini Unguja na Hashimu Magona kutoka Shinyanga.
Viungo wa pembeni ni Omari Nyenje wa Mtwara na Chunga Zito kutoka Manyara.
Washambuliaji ni Mohammed Said kutoka Kusini Pemba, Ayubu Lipati wa Ilala, Abdurahman Othman  kutoka Mjini Magharibi na Paul Bundara kutoka Ilala.
Aliongeza, katika kikosi hicho pia wamejumuishwa wachezaji wawili waliojiunga na Timu ya Taifa ya vijana  U20; Mbwana Mshindo kutoka Tanga na Bayaga Fabian kutoka Mbeya.
Manyanga alisema wachezaji wengine walioachwa wataendelea kuwa kwenye uangalizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) kwa sababu mpango wa maboresho ya timu ya Taifa ni endelevu.
Alisema Kambi ya timu hiyo iliyoanza Machi 22, imehitimishwa leo Aprili 17 kwa awamu ya kwanza ambapo wachezaji hao watajiunga na kikosi cha Stars mechi ya Kirafiki kisha watarudi tena wilayani Rungwe kwa ajili ya Kambi ya awamu ya Pili.

Mzee Edwin Mteu amlaani Lissu kumtusi Nyerere


Nilimsikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu. 
 
Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972. 
 
Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.
 
Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke: 
 
Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao. 
 
Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!
With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.
Edwin Mtei

PAPARAZI

SHIVIWATA yamlilia Mzee Gurumo

Gurumo (kati) enzi za uhai wake
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)Umepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mkongwe wa muziki wa dansi nchini na aliyekuwa kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma,Muhidin Maalim Gurumo "Kamanda"aliyefariki Jumapili katika hospitali ya Muhimbili.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana kuwa wamepokea kwa majonzi makubwa na kusema kuwa pengo lake haliwezi kuzibika haraka kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao wa kutunga, kuimba na kuongoza wanamuziki wenzake.

Alisema marehemu Gurumo hakuwa mtu wa kukata tamaa kuendeleza muziki wa dansi kwani aliwahi kuwafundisha wanamuzi wanaotamba katika bendi mbalimbali ikiwemo Msondo Ngoma..

"Kutoka miaka ya sitini Gurumo alikonga nyoyo za mashabiki wa muziki akiwa na NUTA, JUWATA,Safari Sound,Sikinde na Msondo ambayo aliastaafu kabla ya kifo chake"alisema Taalib.


Wakati wa uhai wake, Gurumo alikuwa mwanachama wa SHIWATA na alikuwa kiunganishi cha wanamuziki wa Msondo Ngoma kushiriki kuunda kijiji cha wasanii Mkuranga mkoa wa Pwani na kubariki jitihada za kuwakomboa wasanii wa fani mbalimbali kujikomboa kiuchumi..

Marehemu Gurumo alizikwa Jumanne nyumbani kwao Masaki wilaya Kisarawe mkoa wa Pwani.