STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 5, 2014

Waziri Mkuu afutwa kazi Senegal, kisa...!

 
WAZIRI mkuu nchini Senegal Aminata 'The Iron Lady' Toure ameachishwa kazi baada ya chama tawala kushindwa katika uchaguzi mkuu.
Maafisa wanasema kuwa Rais Macky Sall alimtaka Mwanamama huyo kujiuzulu baada ya kuhudumu chini ya kipindi cha mwaka mmoja.
Waandishi wanasema kuwa kutorodhika kwa wanachi kuhusu sera za uchumi za serikali hiyo ndio sababu kuu ya chama hicho kushindwa katika uchaguzi huo.
Waziri Mkuu huyo alikuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo nchini humo tangu Mame Madior Boye kuweka rekodi alipochaguliwa mwaka 2001 na kudumu kwa kipindi kifupi chini ya utawala wa Abdoulaye Wade.
BBC

Wambura aibua 'zengwe' jingine Msimbazi, amshangaa Aveva

Michael Wambura
Rais Mpya wa Simba, Evance Aveva (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Hassan Dalali
ALIYEKUWA Mgombea wa Urais wa Uchaguzi Mkuu wa Simba, Michael Wambura ameibuka tena na kumshangaa Rais mpya wa klabu hiyo,  Evans Aveva na kamati yake ya utendaji kwa kufanya maamuzi ya kulipeleka suala lake kwenye mkutano mkuu wa agosti 3 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Wambura amesema hakuna haja ya kupeleka suala lake kwenye mkutano huo kwasababu sakata lake lilimalizwa na kamati ya Rufani ya uchaguzi ya TFF chini ya mwenyekiti wake,  Jaji Julius Mutabazi Lugaziya.
Wambura ameyasema hayo ikiwa ni siku moja baada ya Aveva alitangaza kuwasimamishwa wanachama 69 kwa kosa la kwenda mahakama ya kawaida kujaribu kuzuia uchaguzi huo wa Simba na kudai suala lao litajadiliwa kwenye mkutano mkuu wa mwezi agosti, sawia na suala linalomhusu Wambura aliyewahi kuipeleka Simba mahakamani katika uchaguzi wa mwaka 2010 kosa lililomfanya ajikute matatani Msimbazi.
Hata hivyo Wambura amekuja juu na kusema yeye alishasafishwa na kamati ya Lugaziya na kitendo cha Aveva kuwapiga `Stop` wanachama ni kuendelea kuchochea migogoro isiyokuwa ya lazima.
“Mimi nilisafishwa kwenye kamati  ya Rufani ya Lugaziya na ndio maana nilirudishwa kwenye mchakato wa uchaguzi, na niliondolewa kwa kosa la kupiga kampeni kabla ya muda, hivyo sina haja na mkutano huo”. Alisema Wambura.
Wambura aligusia Ibara ya 41(d) ya klabu ya Simba ambapo alifafanua kuwa kuwanyima wanachama fursa ya kujitetea na kusikilizwa kabla ya kuchukua hatua ni uvunjifu wa haki za msingi za binadamu.
Aidha,  Wambura alisema wanachama waliokwenda mahakamani wasipuuzwe kwasababu wana hoja za msingi.
“Wangekuwa hawana hoja, hata mahakama kuu isingewapa haki ya kufungua shauri lao. Wasipuuzwe, wapewe fursa ya kujitetea na kusikilizwa”. Aliongeza Wambura.
Alisisitiza kuwa Ibara ya 54(3) ya klabu ya Simba inafafanua kuwa uamuzi wowote wa kufukuza wanachama lazima upigiwe kura za siri na wajumbe theluthi mbili waunge mkono, huku akitolea mfano wa Hassani Dalali alipofanya jaribio la kumpinuda Mwina Kaduguda, lakini alikwama kwasababu wanachama walikataa pendekezo lake.
Aliongeza kuwa uongozi wa Aveva hauwezi kupambana na wanachama zaidi ya 500 na kama utaendelea kufanya hivyo basi utaingia katika mgogoro mkubwa, lakini akashauri uongozi utafute suluhusho la mapema.
Wambura alisema ushauri wake atauwasilisha kwa maandishi kwa uongozi wa Simba sc kama sehemu kutunza kumbukumbu kuwa aliyaongea hayo.

Stars majaribuni tena leo Bostwana

BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 4-2 toka kwa wenyeji wao Botswana, timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo inatarajiwa kujiuliza tena wakati itakapovaana na Lesotho katika mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa mjini Gaborone.
Stars ipo Botswana kujiandaa na mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili dhidi ya Mamba ya Msumbiji kuwania kucheza Fainali za Afrika za mwakani zitakazochezwa nchini Morocco.
Timu hiyo inayonolewa na kocha Mart Nooij, inashuka dimbani kuivaa na Lesotho ikiwa ni siku chache tangu inyukwe mabao 4-2 na Botswana katika moja ya mechi zake za kujiwinda na pambano la Mamba litakalochezwa Julai 20 jijini Dar es Salaam.
Hiyo ni mechi ya kwanza kwa timu hizo kukutana na mara baada ya mchezo huo Stars itarejea nchini kuendelea na kambi wakati wapinzani wao watakuwa wakijiandaa na mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya wenyeji wao Botswana kabla ya kuwasubiri Kenya katika mechi ya kuwania fainali za Afrika 2015.