STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 24, 2014

Maajabu! Maiti iliyozikwa miaka 700 yakutwa bado wamo!

Maiti hiyo ikiwa imetolewa nje ya jeneza
Ama kweli ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni....Maiti ya mwanamke iliyozikwa miaka 700 iliyopita yagunduliwa China ikiwa haijaoza. Ipo katika hali nzuri kiasi kwamba bado ina nyusi. Inasemekana alihifadhiwa vizuri na inaonyesha alikuwa ni mtu kutoka katika familia ya ufalme. 
Maiti hiyo iligunduliwa na wafanyakazi wa barabara (wakandarasi) huko China mashariki walipopewa kazi ya kupanua barabara katika mji wa Taizhou, Mkoani wa Jiangsu. Wakandarasi hao walitakiwa kuchimba kwenda chini kiasi cha futi 6 ili kumaliza mwinuko uliokuwa katikati ya bara bara ndipo wakakutana kitu wasichotarajia kukikuta.
Walipokuwa wakichimba walikuta kitu kigumu  na baada ya kufanya utafiti wao kidogo ndipo waligundua kuwa kulikuwa kuna kaburi alilozikwa mtu na ndipo wakawaita wataalamu ili kuchunguza zaidi, baada ya hapo wakaamua kuweka wazi juu ya tukio hilo kuwa waligundua kwamba kaburi hilo lilikuwa na umri wa miaka 700. Tazama picha zaidi la sakata hilo hapa chini...
Mkandarasi akijaribu kuvunja zege lililozunguka sanduku lakini kabla hawajajua kuwa kuna maiti
Baada ya kuvunja sanduku hilo la zege
Wakihamaki baada ya kuona kitu ndani ya sanduku
Wakianza kufunua matambara yaliyo ndani ya sanduku yaliyozunguka maiti

Noma! Raia wa UK agundulika kuambulizwa Ebola


Daktari wa Ebola nchini Liberia
Raia mmoja wa Uingereza anayeishi nchini Sierra leone ameambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola.
Idara ya afya imethibitisha kisa hicho.
Tangu mwezi machi zaidi ya watu 1400 wameripotiwa kufariki magharibi mwa Afrika.
Idara ya afya imesema kuwa raia wa kwanza mwingereza kuambukizwa ugonjwa huo alikuwa anaishi Sierra Leone.
Taifa hilo ni miongoni mwa mataifa ambayo yameathiriwa vibaya na ugonjwa huo.
Mwathiriwa wa Ebola aliyepona
Iwapo atapewa matibabu nchini Uingereza mgonjwa huyo ana uwezekano mkubwa wa kupata nafuu kwa sababu hospitali za Sierra Leone zimejaa waathiriwa wa ugonjwa huo hatari ambao unaendelea kuenea kwa kasi.
Eneo la kuwatenga wagonjwa tayari limebuniwa katika hospitali ya Royal free mjini London.
Kufikia sasa hakuna tiba ya ugonjwa wa ebola,ijapokuwa dawa ya majaribio iliwasaidia raia wawili wa Marekani kupona huku maafisa watatu wa afya pia wakionyesha dalili za kupata nafuu walipoitumia dawa hiyo nchini Liberia.
Katika mataifa ya afrika magharibi wakaazi wengi wamekuwa wakiogopa kuwatoa ndugu zao wanaoathiriwa na ebola kwa hofu ya kutowaona tena.
BBC SWAHILI

Shaaban Kisiga 'Marlone' anayeipa Simba ubingwa 2014-2015

WAPO baadhi ya mashabiki wa soka wanaishangaa Simba kwa kuamua kumrejesha kikosini kiungo wao wa zamani, Shaaban Kisiga 'Marlon' kwa kuamini kuwa ni 'zilipendwa'.
Hata hivyo kwa wanaotambua kipaji na uwezo mkubwa wa nyota huyo wa zamani wa Stars aliyetokea Mtibwa Sugar wanajua Simba itavuna nini kwa Kisiga.
Licha ya kuwepo dimbani kwa muda mrefu, bado uwezo wa Kisiga ni ule ule zaidi  umeongezeka kutokana na uzoefu alionao na jinsi anavyojitunza kama mwenyewe anavyosema.
"Kisiga ni yule yule, hajabadilika kitu sanasana ameongeza mzoefu zaidi. Nimerejea Simba baada ya miaka 9 ili kuirejeshea heshima," anasema.
Kisiga aliyefanya kazi na Phiri miaka 10 iliyopita anasema Mzambia huyo siyo bonge la kocha tu, bali ni baba mlezi anayejua kukaa na wachezaji na kuwafanya wafanye kazi zao kwa ufanisi dimbani.
"Binafsi nimefurahi kurejea Simba na kukutana tena na Phiri, Simba watarajie makubwa msimu huu chini ya kocha Phiri," anasema.
Kuhusu ushindani ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi, Kisiga anasema amejiandaa kupambana akitumia uzoefu alionao kuhakikisha anapata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.
"Ndani ya Simba kuna ushindani mkubwa kwani kuanzia namba 6-11 kuna vipaji vikubwa hivyo kufanya kila mchezaji kupambana  kujihakikishia namba jambo ambalo hata mimi nalifanya," anasema.
Nyota huyo aliyewahi kucheza soka la kulipwa Umangani, anasema ubinafsi na chuki ndivyo zinavyoua vipaji vingi vya soka nchini na kuikwamisha Tanzania kutamba kimataifa kwenye michuano ya kimataifa.
Anasema wapo wachezaji waliokatishwa tamaa na kuacha soka wangali wana uwezo mkubwa dimbani na kuwataka wadau wabadilike kama wanataka Tanzania ifanye vyema kimataifa.
"Leo vipaji vya akina Said Sued, Nurdin Bakar au Boban (Haruna Moshi) vimepotea kwa sababu ya chuki na ubinafsi, siyo kama soka lao limeisha. Hatuwezi kufika mbali kwa hali hii," anasema.
Anasema uteuzi na usajili wa kujuana na kubebana umekuwa ukifanya timu za Tanzania kuachwa mbali na mataifa hata yaliyokuwa nyuma.
Shabiki huyo wa Liverpool na asiyemhofia mchezaji yeyote dimbani anasema lazima viongozi na wadau wa soka waangalie kile ambacho mchezaji anachokifanya dimbani na siyo yale ya nje ya dimba.
"Wapo watu wanawahukumu wachezaji kwa matendo yao ya mitaani wakati uwezo wao dimbani ni msaada mkubwa kwa taifa, japo ni kweli nidhamu ni kitu cha muhimu katika kila jambo," anasema.
Anasema pia wadau wa soka wamekuwa wakiwabeza wachezaji wazoefu kwa kuwaita 'wazee' wakati Ryan Giggs na wakali wengine wa Ulaya wanazichezea klabu zao hadi wakiwa na miaka zaidi ya 40.
"Watanzania waache tabia hizi, mtu kucheza muda mrefu haina maana mtu ni mzee. Hata wale wanaonibeza sasa ndiyo hao hao watakaokuwa wakinishangilia dimbani kwa sababu soka nalijua na bado nina uwezo mkubwa," anasema.
Juu ya pambano asilosahau, Kisiga anasema ni lile la Nusu Fainali la Kombe la Kagame 2004 kati ya Simba na APR lililochezwa Kigali, Rwanda na Simba kung'olewa kionevu kwa kufungwa mabao 2-1.
"Nalikumbuka kwa jinsi tulivyopambana, lakini wenyeji walikuja kubebwa na kutuondosha mashindano kwa mabo 2-1," anasema.
Kisiga ambaye hana mpango kabisa wa kustaafu kwa sasa anasema anaamini ligi kuu ijayo itakuwa ngumu na yenye ushindani zaidi ya msimu uliopita kwa jinsi timu zinavyofanya maandalizi mazuri.
Hata hivyo anasisitiza kuwa msimu wa 2014-2015 ni wa Simba iwe isiwe kwa sababu wamefanya usajili mzuri chini ya uongozi makini na kocha bora hivyo siyo rahisi kulikosa taji linaloshikiliwa na Azam.
"Naamini ni zamu ya Simba safari hii, tutapambana kuirejeshea ubingwa na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, muhimu tushikamane na kuwa wamoja ndani ya Simba," anasema Kisiga.

Newz Alert! Ajali mbaya yatokea Mbeya, 10 wajeruhiwa


















TAARIFA KAMILI BAADAE
PICHA NA MBEYA YETU

Mshale wa Aisha Bui kutupwa wiki ijayo siyo kesho tena

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiXMubpSkoyEQuwMbeI-V_WEnpb2FZ55PnmSTksu9SQcbRJoiwNFcLnFxjnDHjjzi94I0uF5_h6NYkWE5ZClymhKjniWp9O0pMjTGLQRCQHBZRPqT21Lfx13uwenFVycRWQjPOaQzcETW0/s1600/DUI.jpg
Aisha Bui
FILAMU mpya ya muigizaji nyota wa filamu nchini, Aisha Fat'hi 'Aisha Bui' iitwayo 'Mshale wa Kifo' inatarajiwa kuingia sokoni wiki ijayo baada ya mipango ya kuitoa leo Jumatatu kushindikana.
Aidha mwanadada  ametamba kuwa filamu hiyo ni mwanzo wa uhondo ambao kampuni yake ya Bad Girl Film's imepanga kuwapa mashabiki wa filamu Tanzania.
Akizungumza na MICHARAZO, Aisha Bui alisema filamu hiyo aliyoigiza na wakali kama Mzee Chilo, Gabo wa Zagamba na wengine ilikuwa itolewe leo, lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake itaingia sokoni Septemba 4, huku ikijipanga kuandaa kazi nyingine kali zaidi na hiyo.
Aisha Bui, alisema japo filamu hiyo ni kazi yake ya kwanza kuiandaa, lakini kwa jinsi ilivyoandaliwa kwa umakini mkubwa ni wazi mashabiki watajua ujio wake mpya siyo wa kubahatisha.
"Naiachia filamu yangu mapema mwezi ujao badala ya Jumatatu (leo), nawaomba mashabiki waniunge mkono kwa kununua nakala halisi, ili kuiwezesha kampuni ya Bad Girl kuendelea kuwapa uhondo zaidi, kuna makubwa yapo njiani kutoka kwangu," alitamba Aisha Bui.
Nyota huyo aliyecheza filamu mbalimbali ikiwamo ya Saturday Morning, Better Days, Not Without My Son, Continous Love, Revenge of Love, Mirathi, Pain of Love, Crazy Love na The Second Wife, alisema ndani ya filamu hiyo mpya inasimulia kisa cha mfanyabiashara wa dawa za kulevya ambaye anamlazimisha askari Polisi kumsaidia kupitisha mzigo wake.
Hata hivyo kazi haiwi rahisi na kuibua kashkash kwa binti wa askari huyo Myrine nafasi iliyochezwa na Aisha kufanywa kama chambo.
"Ni simulizi linalosisimua na kutia simanzi na bahati nzuri walioiigiza kuanzia mimi mwenyewe, Gabo, Mzee Chilo na wengine tumeitendea haki," alisema Aisha.

KIVUMBI AFRIKA AS VITA vs TP MAZEMBE NI SHIIIDA!

http://ptblog.pesatimes.com/wp-content/uploads/2014/04/mazembe.jpg
TP Mazembe
https://lh5.googleusercontent.com/-WVEVQ9rwWPA/T4sgtVuUV_I/AAAAAAAASJ0/i37zP2UN0W0/IMG_0282.jpg?imgmax=800
AS VITA
KIVUMBI za mechi za kuhitimisha hatua ya makudni kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika kinatarajiwa kutimka vumbi leo kwa klabu nane zitakazposhuka dimbani kumalizia viporo vyao kabla ya kuruhusu kuanza kwa mechi za nusu fainali za michuano hiyo mikubwa.
Vita Club itakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani kupepetana na 'ndugu' zao TP Mazembe kuwania uongozi wa kundi A wa Ligi ya Mabingwa Afrika, huku timu za Esperance ya Tunisia ikiialika Al Ahly Benghazi wa Libya mjini Tunis katika mechi nyingine kamambe.
Katika michuano ya Kombe la Shirikisho AC Leopard ya Congo itaialika ASEC Memosa ya Ivory Coast, huku Real Bamako ya Mali itaialika Coton Sports ya Cameroon katika pambano jingine la kukata na mundu la michuano hiyo.
Pambano la la mahasimu DR Congo As Vita dhidi ya Mazembe ndizo zinazosubiriwa kwa hamu na amshabiki kutokana na upinzani wao na wengi kutaka kuona kama Vita italipa kisasi kw akipigo ilichopewa na TP Mazembe katika mechi yao ya mkondo wa kwanza.
Pia Vita imekuwa nyonge kwa wapinzani wao hata kwenye Ligi Kuu ya DR Congo, hivyo mechi yao leo licha ya kutaka ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kwanza ya kundi hilo, lakini pia kulinda heshima yao dhidi ya mahasimu wao wanaotamba na nyota wa Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

Hivi Ndivyo Tanzania XI iliyotota kwa Real Madrid Legends





Neymar majanga Barcelona, La Liga yaanza kwa kishindo

http://taroudantnews.com/fichiersTrdnt/uploads/naymar1.jpgKLABU ya Barcelona imepata pigo kubwa kuelekea katika mchezo wao wa ufunguzi wa La Liga dhidi ya Elche utakaochezwa leo Jumapili kutokana na taarifa za kukosekana kwa Neymar katika mchezo huo wa Camp Nou kutokana na majeruhi.
Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, ndio kwanza alikuwa ameruhusiwa kucheza na madaktari wa timu hiyo baada ya kupona majeruhi ya mgongo aliyopata katika Kombe la Dunia lakini sasa anakabiliwa na majeruhi mengine. 
Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, imedai kuwa Neymar alikuwa akilalamika maumivu katika kifundo chake cha mguu wa kushoto na baada ya vipimo imegundulika kuwa ana matatizo ambayo yatachukua muda kidogo kupona. 
Taarifa hiyo imeendelea kudai kuwa kurejea mazoezini kwa mchezaji huyo kutategemea kumalizika kwa maumivu hayo hivyo ni wazi hatakuwepo katika mchezo wa leo. 
Neymar alicheza mechi 26 za La Liga msimu uliopita na kufunga mabao saba lakini msimu huu unaonekana tayari ameuanza vibaya kwa maumivu.
Kipute cha ligi hiyo ya Hispania kilianza usiku wa jana kwa kushuhudiwa Malaga wakitamba nyumbani kwa kuitandika Athletico Club bao 1-0, Sevilla ikilazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Valencia, huku Granada ikivuna ushindi nyumbani dhidi ya Deportivo la Coruna kwa kuilaza mabao 2-1 na Almeria na Espanyol wakitishana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Meya Silaa awatoa hofu wakazi wa Ilala

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjoC3Qa3K4vPRbqDFp0Auh_DWoHWp32YREGTNW2jwGLbie2fDvO1DMCFbA5u3pttAhdiBXgmRqxUvbS2HcEmn0s1XhZER_ZkcsKbCthuIS4iznJ89oaD5DiaNomDGsbz9d05cwyDaQhDt0/s1600/Jerry+Silaa.jpg
NA SULEIMAN MSUYA
WAKATI kukiwa na hali ya sintofahamu juu ya ubomoji wa mzumnguko wa uliopo katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi Kariakoo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Meya wa Manispaa hiyo Jerry Slaa amesema ubomoaji huo unalenga kupisha ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi.
Meya huyo alibainisha hilo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.
Alisema Mradi wa mabasi yaendao kasi unahusu barabara ya Morogoro, Kawawa na Msimbazi hivyo Manispaa inapaswa kuondoa ili kupisha ujenzi huo.
“Unajua Serikali ipo katika mkakati wa kuboresha miundombinu hivyo eneo lile la mzunguko wa Msimbazi linahusika hivyo tunapswa kuuondoa ili ujenzi uendelee”, alisema.
Slaa alisema pamoja na kuondoa mzunguko huo Manispaa inaendelea kutafuta eneo ambalo watauhamishia ili kuendelea kuonekana katika  Manispaa hiyo na jiji kwa ujumla.
Meya huyo Manispaa ya Ilala aliwataka wananchi wa Ilala na maeneo mengine ya Dar es Salaam wasiwe na hofu juu ya kinachoondelea kwani ni katika harakati za kuboresha jiji.
Akizungumzia juu ya changamoto ambazo zinaikabili Manispaa ya Ilala alisema ni suala la kuondoa uchafu katika makazi ya watu ambapo kata 16 kati ya 26 za manispaa hiyo bado hazijapata mzabuni wa kukusanya taka.
Slaa alisema Manispaa ipo katika mkakati wa kuzisaidia Kata zilizobakia magari ya kubeba taka ambapo kwa kuanzia watatoa magari tisa kwa vikundi ambavyo vipo katika kata.
“Changamoto zipo nyingi ila hii ya taka inatuumiza vichwa sasa hivyo tumefikiria ili kuondoa taratibu za wananchi kuweka taka barabarani tumeamua kuvipatia vikundi katika Kata magari ili wafanye kazi hiyo ya kukusanya moja kwa moja wenyewe”, alisema.
Pia alisema manispaa hiyo inakabiliwa na changamoto ya bajeti inayotosha, watumishi wachache ambapo pia walio wengi wanaelimu ndogo ambayo haindani na kasi ya mahitaji ya jamii.
Alisema juhudi za manispaa hiyo ni kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma zilizo na vigezo na kwa wakati ili wawe ni sehmu ya maendeo ya manspaa yao.