STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 10, 2016

Vikosi kamili vitakavyochuana Ufaransa katika Euro 2016 hivi hapa

http://www.sportsmirchi.com/wp-content/uploads/2015/10/UEFA-Euro-2016-Qualified-teams-List.jpg 
PARIS, Ufaransa
TIMU 24 za taifa barani Ulaya zitakazoshindana katika fainali za mwaka huu za Euro 2016 zimetangaza vikosi vyao vya mwisho vya wachezaji 23 vya mwisho vitakavyoshiriki mashindano hayo nchini Ufaransa, ambayo yataanza leo Juni 10 hadi Julai 10 mwaka huu.
 
ALBANIA (Kundi A)
(wachezaji 23 kikosi cha mwisho) 
Makipa: Etrit Berisha (Lazio), Alban Hoxha (Partizani), Orges Shehi (Skenderbeu).

Mabeki: Elseid Hysaj (Napoli), Lorik Cana (Nantes), Arlind Ajeti (Frosinone), Mergim Mavraj (Koeln), Naser Aliji (Basel), Ansi Agolli (Karabag), Frederik Veseli (Lugano).
Viungo: Ermir Lenjani (Nantes), Andi Lila (Giannina), Migjen Basha (Como), Ledian Memushaj (Pescara), Burim Kukeli (Zurich), Taulant Xhaka (Basel), Ergys Kace (Paok), Amir Abrashi (Freiburg), Odise Roshi (Rijeka).

Washambuliaji: Bekim Balaj (Rijeka), Sokol Cikalleshi (Medipol Basaksehir), Armando Sadiku (Vaduz), Shkelzen Gashi (Colorado Rapids).

AUSTRIA(Kundi F)
 
Makipa: Robert Almer (Austria Vienna), Heinz Lindner (Eintracht Frankfurt), Ramazan Ozcan (Ingolstadt).

Mabeki: Aleksandar Dragovic (Dinamo Kiev), Christian Fuchs (Leicester City), Gyorgy Garics (Darmstadt), Martin Hinteregger (Borussia Monchengladbach), Florian Klein (Stuttgart), Sebastian Prodl (Watford), Markus Suttner (Ingolstadt), Kevin Wimmer (Tottenham Hotspur).

Viungo: David Alaba (Bayern Munich), Marko Arnautovic (Stoke City), Julian Baumgartlinger (Mainz), Martin Harnik (Stuttgart), Stefan Ilsanker (Leipzig), Jakob Jantscher (Luzern), Zlatko Junuzovic (Werder Bremen), Marcel Sabitzer (Leipzig), Alessandro Schopf (Schalke).

Washambuliaji: Lukas Hinterseer (Ingolstadt), Rubin Okotie (1860 Munich), Marc Janko (Basel).

UBELGIJI(Kundi E)

Makipa: Thibaut Courtois (Chelsea), Jean-Francois Gillet (Mechelen), Simon Mignolet (Liverpool).

Mabeki: Toby Alderweireld (Tottenham), Jason Denayer (Galatasaray), Bjorn Engels (Club Bruges), Nicolas Lombaerts (Zenit), Jordan Lukaku (Oostende), Thomas Meunier (Club Bruges), Thomas Vermaelen (Barcelona), Jan Vertonghen (Tottenham).

Viungo: Moussa Dembele (Tottenham), Marouane Fellaini (Manchester United), Radja Nainggolan (Roma), Axel Witsel (Zenit St Petersburg).

Washambuliaji: Michy Batshuayi (Marseille), Christian Benteke (Liverpool), Yannick Carrasco (Atletico Madrid), Kevin De Bruyne (Manchester City), Eden Hazard (Chelsea), Romelu Lukaku (Everton), Dries Mertens (Napoli), Divock Origi (Liverpool).

CROATIA(Kundi D)
Makipa: Danijel Subasic (Monaco), Lovre Kalinic (Hajduk Split), Ivan Vargic (Rijeka).

Mabeki: Vedran Corluka (Lokomotiv Moscow), Darijo Srna (Shakhtar Donetsk), Domagoj Vida (Dynamo Kiev), Sime Vrsaljko (Sassuolo), Gordon Schildenfeld (Dinamo Zagreb), Ivan Strinic (Napoli), Tin Jedvaj (Bayer Leverkusen)
.
Viungo: Luka Modric (Real Madrid), Ivan Rakitic (Barcelona), Mateo Kovacic (Real Madrid), Marcelo Brozovic (Inter Milan), Milan Badelj (Fiorentina), Ivan Perisic (Inter Milan), Marko Rog (Dinamo Zagreb), Ante Coric (Dinamo Zagreb).



Washambuliaji: Mario Mandzukic (Juventus), Nikola Kalinic (Fiorentina), Marko Pjaca (Dinamo Zagreb), Duje Cop (Dinamo Zagreb), Andrej Kramaric (Leicester).

JAMHURI YA CZECH (Kundi D)
  
Makipa: Petr Cech (Arsenal), Tomas Vaclik (Basle), Tomas Koubek (Slovan Liberec).

Mabeki: Theodor Gebre Selassie (Werder Bremen), Roman Hubnik (Viktoria Pilsen), Pavel Kaderabek (Hoffenheim), Michal Kadlec (Fenerbahce), David Limbersky (Viktoria Pilsen), Daniel Pudil (Sheffield Wednesday), Marek Suchy (Basle), Tomas Sivok (Bursaspor).

Viungo: Vladimir Darida (Hertha Berlin), Borek Dockal (Sparta Prague), Jiri Skalak (Brighton) Daniel Kolar (Viktoria Pilsen), Ladislav Krejci (Sparta Prague), David Pavelka (Kasimpasa), Jaroslav Plasil (Bordeaux), Tomas Rosicky (Arsenal), Josef Sural (Sparta Prague).

Washambuliaji: David Lafata (Sparta Prague), Tomas Necid (Burkaspor), Milan Skoda (Slavia Prague).

ENGLAND (Kundi B)
   
Makipa: Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Manchester City), Tom Heaton (Burnley).

Mabeki: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Danny Rose (Tottenham), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham).

Midfielders: Dele Alli (Tottenham), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Jack Wilshere (Arsenal).

Washambuliaji: Harry Kane (Tottenham), Marcus Rashford (Manchester United), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Jamie Vardy (Leicester)

UFARANSA (Kundi A)
  
Makipa: Benoit Costil (Rennes), Hugo Lloris (Tottenham), Steve Mandanda (Marseille).

Mabeki: Lucas Digne (Roma), Patrice Evra (Juventus), Christophe Jallet (Lyon), Laurent Koscielny (Arsenal), Eliaquim Mangala (Manchester City), Samuel Umtiti (Lyon), Bacary Sagna (Manchester City), Adil Rami (Sevilla).

Viungo: Yohan Cabaye (Crystal Palace), Morgan Scheiderlin (Manchester United), N'Golo Kante (Leicester), Blaise Matuidi (Paris Saint-Germain), Paul Pogba (Juventus), Moussa Sissoko (Newcastle).

Washambuliaji: Kingsley Coman (Bayern Munich), Andre-Pierre Gignac (Tigres), Olivier Giroud (Arsenal), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Anthony Martial (Manchester United), Dimitri Payet (West Ham).

UJERUMANI(Kundi C)
  
Makipa: Manuel Neuer (Bayern Munich), Marc-Andre ter Stegen (Barcelona), Bernd Leno (Leverkusen)

Mabeki: Jerome Boateng (Bayern Munich), Jonas Hector (Cologne), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Benedikt Howedes (Schalke), Shkodran Mustafi (Valencia), Emre Can (Liverpool), Antonio Rudiger (Roma)

Viungo: Sami Khedira (Juventus), Toni Kroos (Real Madrid), Mesut Ozil (Arsenal), Julian Draxler (Wolfsburg), Bastian Schweinsteiger (Manchester United), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Julian Weigl (Borussia Dortmund), Leroy Sane (Schalke)

Washambuliaji: Lukas Podolski (Galatasaray), Thomas Muller (Bayern Munich), Mario Gomez (Besiktas), Mario Gotze (Bayern Munich), Andre Schurrle (Wolfsburg)

HUNGARY(Kundi F)

Makipa: Gabor Kiraly (Haladas), Denes Dibusz (Ferencvaros), Peter Gulacsi (Leipzig)

Mabeki: Attila Fiola (Puskas Academy), Barnabas Bese (MTK Budapest), Richard Guzmics (Wisla Krakow), Roland Juhasz (Videoton), Adam Lang (Videoton), Tamas Kadar (Lech Poznan), Mihaly Korhut (Debrecen)

Viungo: Adam Pinter (Ferencvaros), Gergo Lovrencsics (Lech Poznan), Akos Elek (Diosgyor), Zoltan Gera (Ferencvaros), Adam Nagy (Ferencvaros), Laszlo Kleinheisler (Werden Bremen), Zoltan Stieber (Nuremberg)

Washambuliaji: Balazs Dzsudzsak (Bursaspor), Adam Szalai (Hannover), Krisztian Nemeth (Al Gharafa), Nemanja Nikolics (Legia Warsaw), Tamas Priskin (Slovan Bratislava), Daniel Bode (Ferencvaros)

ICELAND (Kundi F)
  
Makipa: Hannes Halldorsson (Bodo/Glimt), Ogmundur Kristinsson (Hammarby), Ingvar Jonsson (Sandefjord).

Mabeki: Ari Skulason (OB), Hordur Magnusson (Cesena), Hjortur Hermannsson (PSV Eindhoven), Ragnar Sigurdsson (Krasnodar), Kari Arnason (Malmo), Sverrir Ingi Ingason (Lokeren), Birkir Sævarsson (Hammarby), Haukur Heidar Hauksson (AIK).

Viungo: Emil Hallfredsson (Udinese), Gylfi Sigurdsson (Swansea), Aron Gunnarsson (Cardiff), Theodor Elmar Bjarnason (AGF), Arnor Ingvi Traustason (Norrkoping), Birkir Bjarnason (Basel), Johann Gudmundsson (Charlton), Eidur Gudjohnsen (Molde), Runar Mar Sigurjonsson (Sundsvall).

Washambuliaji: Kolbeinn Sigthorsson (Nantes), Alfred Finnbogason (Augsburg), Jon Dadi Bodvarsson (Kaiserslautern).

ITALIA (Kundi E)

Makipa: Gianluigi Buffon (Juventus), Federico Marchetti (Lazio), Salvatore Sirigu (Paris Saint-Germain)

Mabeki: Andrea Barzagli (Juventus), Leonardo Bonucci (Juventus), Giorgio Chiellini (Juventus), Angelo Ogbonna (West Ham), Matteo Darmian (Manchester United), Mattia De Sciglio (Milan)

Viungo: Daniele De Rossi (Roma), Alessandro Florenzi (Roma), Emanuele Giaccherini (Bologna), Thiago Motta (Paris Saint-Germain), Marco Parolo (Lazio), Stefano Sturaro (Juventus), Antonio Candreva (Lazio)

Washambuliaji: Eder (Inter), Ciro Immobile (Torino), Lorenzo Insigne (Napoli), Graziano Pelle (Southampton), Simone Zaza (Juventus), Federico Bernardeschi (Fiorentina), Stephan El Shaarawy (Roma)

IRELAND KASKAZINI(Kundi C)
 
Makipa: Alan Mannus (St Johnstone), Michael McGovern (Hamilton Academical), Roy Carroll (Linfield).

Mabeki: Craig Cathcart (Watford), Jonathan Evans (West Bromwich Albion), Gareth McAuley (West Bromwich Albion), Luke McCullough (Doncaster Rovers), Conor McLaughlin (Fleetwood Town), Lee Hodson (MK Dons), Aaron Hughes (Free agent), Patrick McNair (Manchester United), Chris Baird (Derby County).

Viungo: Steven Davis (Southampton), Oliver Norwood, (Reading), Corry Evans, (Blackburn Rovers), Shane Ferguson (Millwall), Stuart Dallas (Leeds United), Niall McGinn (Aberdeen), Jamie Ward (Nottingham Forest).

Washambuliaji: Kyle Lafferty (Norwich City), Conor Washington (Queens Park Rangers), Josh Magennis (Kilmarnock), Will Grigg (Wigan Athletic).

POLAND (Kundi C)
  
Makipa: Lukasz Fabianski (Swansea City), Wojciech Szczesny (Roma), Artur Boruc (Bournemouth)

Mabeki: Thiago Cionek (Palermo), Kamil Glik (Torino), Artur Jedrzejczyk (Legia Warsaw), Michal Pazdan (Legia Warsaw), Lukasz Piszczek (Borussia Dortmund), Bartosz Salamon (Cagliari), Jakub Wawrzyniak (Lechia Gdansk)

Viungo: Jakub Blaszczykowski (Fiorentina), Kamil Grosicki (Rennes), Tomasz Jodlowiec (Legia Warsaw), Bartosz Kapustka (Cracovia), Grzegorz Krychowiak (Sevilla), Karol Linetty (Lech Poznan), Krzysztof Maczynski (Wisla), Slawomir Peszko (Lechia Gdansk), Filip Starzynski (Zaglebie Lubin), Piotr Zielinski (Empoli).

Washambuliaji: Arkadiusz Milik (Ajax), Robert Lewandowski (Bayern Munich), Mariusz Stepinski (Ruch Chorzow) 

URENO(Kundi F)

Makipa: Rui Patricio (Sporting Lisbon), Anthony Lopes (Lyon), Eduardo (Dinamo Zagreb).

Mabeki: Vieirinha (Wolfsburg), Cedric Soares (Southampton), Pepe (Real Madrid), Ricardo Carvalho (Monaco), Bruno Alves (Fenerbahce), Jose Fonte (Southampton), Eliseu (Benfica), Raphael Guerreiro (Lorient).

Viungo: William Carvalho (Sporting Lisbon), Danilo Pereira (Porto), Joao Moutinho (Monaco), Renato Sanches (Benfica), Adrien Silva (Sporting Lisbon), Andre Gomes (Valencia), Joao Mario (Sporting Lisbon).

Washambuliaji: Rafa Silva (Braga), Ricardo Quaresma (Besiktas), Nani (Fenerbahce), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Eder (Lille)

JAMHURI YA IRELAND (Kundi E)
    
Makipa: Shay Given (Stoke), Darren Randolph (West Ham), Keiren Westwood (Sheffield Wednesday).

Mabeki: Seamus Coleman (Everton), Cyrus Christie (Derby), Ciaran Clark (Aston Villa), Richard Keogh (Derby), John O'Shea (Sunderland), Shane Duffy (Blackburn), Stephen Ward (Burnley).

Viungo: Aiden McGeady (Sheffield Wednesday), James McClean (West Brom), Glenn Whelan (Stoke), James McCarthy (Everton), Jeff Hendrick (Derby), David Meyler (Hull), Stephen Quinn (Reading), Wes Hoolahan (Norwich), Robbie Brady (Norwich), Jonathan Walters (Stoke).

Washambuliaji: Robbie Keane (LA Galaxy), Shane Long (Southampton), Daryl Murphy (Ipswich).

ROMANIA(Kundi A)
    
Makipa: Ciprian Tatarusanu (Fiorentina), Costel Pantilimon (Watford), Silviu Lung (Astra Giurgiu).

Mabeki: Cristian Sapunaru (Pandurii Targu Jiu), Alexandru Matel (Dinamo Zagreb), Vlad Chiriches (Napoli), Valerica Gaman (Astra Giurgiu), Cosmin Moti (Ludogorets), Dragos Grigore (Al-Sailiya), Razvan Rat (Rayo Vallecano), Steliano Filip (Dinamo Bucharest).

Viungo: Mihai Pintilii (Steaua Bucharest), Ovidiu Hoban (Hapoel Beer Sheva), Andrei Prepelita (Ludogorets), Adrian Popa (Steaua Bucharest), Gabriel Torje (Osmanlispor), Alexandru Chipciu (Steaua Bucharest), Nicolae Stanciu (Steaua Bucharest), Lucian Sanmartean (al-Ittihad).

Washambuliaji: Claudiu Keseru (Ludogorets), Bogdan Stancu (Genclerbirligi), Florin Andone (Cordoba), Denis Alibec (Astra Giurgiu).

URUSI
  
Makipa: Igor Akinfeev (CSKA Moscow), Guilherme (Lokomotiv Moscow), Yuri Lodygin (Zenit St. Petersburg).

Mabeki: Alexei Berezutsky (CSKA Moscow), Vasily Berezutsky (CSKA Moscow), Sergei Ignashevich (CSKA Moscow), Dmitry Kombarov (Spartak Moscow), Roman Neustadter (Schalke), Georgy Shchennikov (CSKA Moscow), Roman Shishkin (Lokomotiv Moscow), Igor Smolnikov (Zenit St Petersburg).

Viungo: Igor Denisov (Dynamo Moscow), Denis Glushakov (Spartak Moscow), Alexander Golovin (CSKA Moscow), Oleg Ivanov (Terek Grozny), Pavel Mamaev (Krasnodar), Alexander Samedov (Lokomotiv Moscow), Oleg Shatov (Zenit St Petersburg), Roman Shirokov (CSKA Moscow), Dmitri Torbinski (Krasnodar).

Washambuliaji: Artyom Dzyuba (Zenit St Petersburg), Alexander Kokorin (Zenit St Petersburg), Fyodor Smolov (Krasnodar).

SLOVAKIA(Kundi B)
 
Makipa: Matus Kozacik (Viktoria Plzen), Jan Mucha (Slovan Bratislava), Jan Novota (Rapid Vienna).

Mabeki: Peter Pekarik (Hertha Berlin), Milan Skriniar (Sampdoria), Martin Skrtel (Liverpool), Norbert Gyomber (Roma), Jan Durica (Lokomotiv Moscow), Kornel Salata (Slovan Bratislava), Tomas Hubocan (Dynamo Moscow), Dusan Svento (Cologne).

Viungo: Viktor Pecovsky (Zilina), Robert Mak (PAOK Thessaloniki), Juraj Kucka (AC Milan), Patrik Hrosovsky (Viktoria Plzen), Jan Gregus (Jablonec), Marek Hamsik (Napoli), Ondrej Duda (Legia Warsaw), Miroslav Stoch (Bursaspor), Vladimir Weiss (Al Gharafa).

Washambuliaji: Michal Duris (Viktoria Plzen), Adam Nemec (Willem II), Stanislav Sestak (Ferencvaros).

HISPANIA
 
Makipa: Iker Casillas (Porto), David de Gea (Manchester United), Sergio Rico (Sevilla).

Mabeki: Sergio Ramos (Real Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Hector Bellerin (Arsenal), Jordi Alba (Barcelona), Marc Bartra (Barcelona), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Mikel San Jose (Athletic Bilbao), Juanfran (Atletico Madrid).

Viungo: Bruno (Villarreal), Sergio Busquets (Barcelona), Koke (Atletico Madrid), Thiago (Bayern Munich), Andres Iniesta (Barcelona), David Silva (Manchester City), Pedro (Chelsea), Cesc Fabregas (Chelsea).

Washambuliaji: Aritz Aduriz (Athletic Bilbao), Nolito (Celta Vigo), Alvaro Morata (Juventus), Lucas Vasquez (Real Madrid).

SWEDEN (Kundi E)
  
Makipa: Andreas Isaksson (Kasimpasa), Robin Olsen (Copenhagen), Patrik Carlgren (AIK).

Mabeki: Ludwig Augustinsson (Copenhagen), Erik Johansson (Copenhagen), Pontus Jansson (Torino), Victor Lindelof (Benfica) Andreas Granqvist (Krasnodar), Mikael Lustig (Celtic), Martin Olsson (Norwich).

Viungo: Jimmy Durmaz (Olympiakos), Albin Ekdal (Hamburg), Oscar Hiljemark (Palermo), Sebastian Larsson (Sunderland), Pontus Wernbloom (CSKA Moscow), Erkan Zengin (Trabzonspor), Oscar Lewicki (Malmo), Emil Forsberg (Leipzig), Kim Kallstrom (Grasshoppers).

Washambuliaji: Marcus Berg (Panathinaikos), John Guidetti (Celta Vigo), Zlatan Ibrahimovic (Paris), Emir Kujovic (Norrkoping).

USWISI(Kundi A)
      
Makipa: Yann Sommer (Borussia Monchengladbach), Roman Buerki (Borussia Dortmund), Marwin Hitz (Augsburg)

Mabeki: Stephan Lichtsteiner (Juventus), Nico Elvedi (Borussia Monchengladbach), Michael Lang (Basle), Johan Djourou (Hamburg), Steve von Bergen (Young Boys), Fabian Schaer (Hoffenheim), Francois Moubandje (Toulouse), Ricardo Rodriguez (Wolfsburg)

Viungo: Valon Behrami (Watford), Blerim Dzemaili (Genoa), Gelson Fernandes (Rennes), Fabian Frei (Mainz), Granit Xhaka (Arsenal), Xherdan Shaqiri (Stoke), Denis Zakaria (Young Boys)

Washambuliaji: Breel Embolo (Basle), Haris Seferovic (Eintracht Frankfurt), Admir Mehmedi (Bayer Leverkusen), Eren Derdiyok (Kasimpasa), Shani Tarashaj (Everton). 

UTURUKI(Kundi D)
      
Makipa: Volkan Babacan (Medipol Basaksehir), Onur Recep Kivrak (Trabzonspor), Harun Tekin (Bursaspor)

Mabeki: Gokhan Gonul (Fenerbahce), Sener Ozbayrakli (Bursaspor), Semih Kaya (Galatasaray), Ahmet Calik (Genclerbirligi), Hakan Balta (Galatasaray), Caner Erkin (Fenerbahce), Ismail Koybasi (Besiktas)

Viungo: Mehmet Topal (Fenerbahce), Selcuk Inan (Galatasaray), Ozan Tufan (Fenerbahce), Oguzhan Ozyakup (Besiktas), Hakan Calhanoglu (Bayer Leverkusen), Nuri Sahin (Borussia Dortmund), Arda Turan (Barcelona), Olcay Sahan (Besiktas), Volkan Sen (Fenerbahce), Emre Mor (Nordsjaelland)

Washambuliaji: Burak Yilmaz (Beijing Guoan), Cenk Tosun (Besiktas), Yunus Malli (Mainz)

UKRAINE (Kundi C)
(wachezaji 23 kikosi cha mwisho) 
Makipa: Andriy Pyatov (Shakhtar), Denys Boyko (Besiktas), Mykyta Shevchenko (Zorya)

Mabeki: Evhen Khacheridi (Dynamo Kiev), Bohdan Butko (Amkar), Artem Fedetskyi (Dnipro), Oleksandr Karavaev (Zorya), Oleksandr Kucher (Shakhtar), Yaroslav Rakytskyi (Shakhtar), Vyacheslav Shevchuk (Shakhtar)

Viungo: Serhiy Rybalka (Dynamo Kiev), Denys Garmash (Dynamo Kiev), Serhiy Sydorchuk (Dynamo Kiev), Andriy Yarmolenko (Dynamo Kiev), Evhen Konoplyanka (Sevilla), Ruslan Rotan (Dnipro), Taras Stepanenko (Shakhtar), Viktor Kovalenko (Shakhtar), Anatolyi Tumoschuk (Kairat), Oleksandr Zinchenko (UFA)

Washambuliaji: Roman Zozylya (Dnipro), Pylyp Budkivskyi (Zorya), Evhen Seleznyov (Shakhtar) 

WALES (Kundi B)
  
Makipa: Wayne Hennessey (Crystal Palace), Danny Ward (Liverpool), Owain Fon Williams (Inverness).

Mabeki: Ben Davies (Tottenham), Neil Taylor (Swansea), Chris Gunter (Reading), Ashley Williams (Swansea), James Chester (West Brom), Ashley Richards (Fulham), James Collins (West Ham).

Viungo: Aaron Ramsey (Arsenal), Joe Ledley (Crystal Palace), David Vaughan (Nottingham Forest), Joe Allen (Liverpool), David Cotterill (Birmingham), Jonathan Williams (Crystal Palace), George Williams (Fulham), Andy King (Leicester), Dave Edwards (Wolves).

Washambuliaji: Hal Robson-Kanu (Reading), Sam Vokes (Burnley), Simon Church (Nottingham Forest), Gareth Bale (Real Madrid).

HIVI NDIVYO UEFA EURO CUP 2016 ITAKAVYOPIGWA UFARANSA

https://s3.eu-central-1.amazonaws.com/panadeuro/assets/fb_image-25449d6e90be250b3d2921a7e0e0ac87.png
UNAWEZA kujua kuwa leo Ijumaa usiku ndio vumbi la fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya 'UEFA Euro 2016 litaanza kutimka nchini Ufaransa, lakini huenda hujui makundi na wala rariba nzima ya michuano hiyo ilivyo.
MICHARAZO MITUPU inakuletea kwa ufupi makundi ya michuano hiyo ya Ulaya ambayo ni ya pili kwa ukubwa baada ya Fainali za Kombe la Dunia, ratiba na jinsi siku 30 zitakazotumika kwa timu 24 kuonyeshana kazi hadi mchezo wa fainali wa
kupatikana kwa bingwa wa mwaka huu mnamo Julai 10, ebu chungulia;


MAKUNDI YALIVYO:
KUNDI AUfaransa
Uswisi
Romania
Albania   

KUNDI B

England   
Urusi
Slovakia
Wales   

KUNDI C

Ujerumani
Poland
Ukraine
Ireland ya Kaskazini

KUNDI D

Hispania
Croatia   
Jamhuri ya Czech
Uturuki

KUNDI E

Ubelgiji
Italia
Sweden   
Jamhuri ya Ireland   


KUNDI F

Ureno
Austria   
Hungary   
Iceland   


RATIBA ILIVYO
KUNDI A
Juni 10, 2016
Ufaransa v Romania- St-Denis

Juni 11, 2016

Albania v Uswisi- Lens

Juni 15, 2016

Romania v Uswisi- Paris
Ufaransa v Albania- Marseille

Juni 19, 2016

Romania v Albania-  Lyon
Uswisi v Ufaransa- Lille

KUNDI B
Juni 11, 2016

Wales v Slovakia- Bordeaux
England v Urusi- Marseille

Juni 15, 2916

Urusi v Slovakia- Lille
England v Wales- Lens

Juni 20, 2016

Urusi v Wales- Toulouse
Slovakia v England- St-Etienne

Kundi C
Juni 12, 2016

Poland v Ireland ya Kaskazini- Nice
Ujerumani v  Ukraine- Lille

Juni 16, 2016

Ukraine vIreland ya Kaskazini- Lyon
Ujerumani v Poland - St-Denis

Juni 21, 2016

Ukraine v Poland- Marseille
Ireland ya Kaskazini v Ujerumani- Paris

Kundi D
Juni 12, 2016

Uturuki v Croatia- Paris

Juni 13, 2016

Hispania v Jamhuri ya Czech- Toulouse

Juni 17, 2016

Jamhuri ya Czech v Croatia-  St-Etienne
Hispania  v Uturuki- Nice

Juni 21, 2016

Jamhuri ya Czech v Uturuki- Lens
Croatia v Hispania- Bordeaux

Kundi E
Juni 13, 2016

Jamhuri ya Ireland v Sweden- St-Denis
Ubelgiji v Italia- Lyon

Juni 17, 2016

Italia v Sweden- Toulouse
Ubelgiji v Jamhuri ya Ireland- Bordeaux

Juni 22, 2016Italia v Jamhuri ya Ireland- Lille
Sweden v Ubelgiji- Nice

Kundi F
Juni 14, 2016Austria v Hungary- Bordeaux
Ureno  v Iceland- St-Etienne

Juni 18, 2016Iceland v Hungary- Marseille
Ureno v Austria- Paris

Juni 22, 2016Iceland v Austria- St-Denis
Hungary v Ureno- Lyon

Mtoano 16 BoraJuni 25, 2016:Mechi 1: Mshindi wa Pili Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi C- St-Etienne
Mechi 2: Mshindi Kundi D vMshindi wa Tatu B/E/F- Lens
Mechi 3: Mshindi Kundi B v Mshindi wa Tatu A/C/D- Paris

Juni 26, 2016:
Mechi 4: Mshindi Kundi F v Mshindi wa Pili Kundi E- Toulouse
Mechi 5: Mshindi Kundi C v Mshindi wa Tatu A/B/F - Lille

 

Juni 27, 2016:Mechi 6: Mshindi Kundi E v Mshindi wa Pili Kundi D- St-Denis
Mechi 7: Mshindi Kundi A v Mshindi wa Tatu C/D/E- Lyon
Mechi 8: Mshindi wa Pili Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi F- Nice


Robo Fainali:Juni 30, 2016
RF1-Mshindi Mechi 1 v Mshindi Mechi 2- Marseille
 

Julai 01, 2016
RF2-Mshindi Mechi 3 v Mshindi Mechi 4-  Lille

Julai 2, 2016
RF3-Mshindi Mechi 5 v Mshindi Mechi 4- Bordeaux
Julai 3, 2016
RF4-Mshindi Mechi 7 v Mshindi Mechi 8- St-Denis
Nusu Fainali:

Julai 6, 2016
NF1-Mshindi QF1 v Mshindi QF2- Lyon
Julai 7, 2016
NF2-Mshindi QF3 v Mshindi QF4- Marseille
Fainali:
Julai 10, 2016
Mshindi NF1 v Mshindi NF2- St-Denis

Hizi ndizo rekodi za Mbeya City msimu wa 2015-2016

IMG_7987
Kikosi cha Mbeya City cha msimu uliopita
NA DISMAS TENI, MBEYA CITY
BAADA ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara  2015/16  na Mbeya City fc kumaliza ikiwa kwenye nafasi ya 8 baada ya kuweka kibindoni jumla ya Pointi 35,  kufuatia  mabao  32  ya kufunga na kufungwa 34 kwenye michezo 30 ya msimu mzima.
Hapa chini ni rekodi kadhaa kutoka benchi la ufundi zimetoka  na kati ya hizo baadhi  zinaonyesha kuwa, magolikipa watatu wa kikosi cha kwanza, Juma Kaseja, Haningtony Kalyesubula na Geoffrey Mwalyego  waliokuwa wakisimama langoni  kwa kupishana kwenye michezo tofauti wamewajibika kwa asilimia 33.33 katika ushindi, sare na hata kupoteza mchezo katika mechi zote 30 za msimu.
Katika rekodi hizo zinaonyesha,  Juma  Kaseja  alicheza michezo 17 na kuruhusu kufungwa mabao 20, Haningtony Kalyesubula alicheza michezo 13 na kufungwa mabao 14 wakati Geoffrey Mwalyego yeye hakupata nafasi ya kucheza mchezo hata mmoja.
Wakati Mlinzi Hassan Mwasapili akiweka rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi kikosini kuliko mchezaji yoyote kwa kucheza mechi 28 na kukosa 2  pia kufunga mabao 2  katika mechi zote 30, Mlinzi wa kati Haruna Shamte amemaliza akiwa na rekodi ya kupata kadi nyingi zaidi kuliko mchezaji yoyote akiwa na  jumla ya kadi 8, kati ya hizo 6 zikiwa za njano na 2 nyekundu.
Kiungo Rafael Daud ndiye kinara wa mabao kikosini akimaliza msimu kwa kufunga mabao 6,na kuifikia rekodi ya Mwegane Yeya aliyoiweka 2013/14,  ingawa  pia  ukurasa wake ukionyesha kuwa alipata kadi 2 za njano.
Mlinzi na kiungo Aboubakary Shaaban akiweka rekodi ya kucheza ligi kuu akiwa na umri mdogo zaidi kuliko wachezaji wote wa City, akicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Coastal Union jijini Tanga akiwa na umri wa miaka 17 na siku 129.
David Kabole alicheza mechi 1 na kufunga bao 1 hii ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu ambao City ilipata ushindi wa 3-0 lakini baada ya hapo hakuonekana tena dimbani  hii ni baada ya kiwango chake kuporomoka kwa kasi na kujikuta akitolewa kwa mkopo kwenda Fc Kimondo na kumpisha Salvatory Nkulula  aliyeingia kikosini na kufanikiwa kucheza  mechi 6 akifunga mabao 4.
Rekodi pia  zinaonyesha 2015/16 ndiyo msimu  pekee ambao City imekuwa chini ya makocha watatu, ikianza na Juma Mwambusi  aliyeondoka  baadae, na nafasi yake kushikwa na Abdul Mingange  ambaye  alidumu kikosini kwa miezi 3, kufuatia matatizo ya kifamilia Mingane  aliachia nafasi hiyo na kumpisha kocha wa sasa Kinnah Phiri.
Licha ya kushinda 4-0 dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo wa duru ya pili April 4 kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa, ushindi mkubwa wa City msimu huu ulikuwa ni ule wa bao 5-1 dhidi ya Toto Africans katika mechi ya kukata nashoka iliyopigwa jijini Mbeya, huku kipiko kikali kikiwa ni kile cha mabao 4-1 ilichokipa kutoka kwa Ndanda Fc huko Nangwanda Sijaona.
Katika nyota walisajiliwa wakati wa dirisha dogo Haruna Moshi  ameonekan kung’ara zaidi akifanikiwa kumaliza msimu akiwa amefunga mabao 3, sambamba na Ramadhani Chombo,Abdalah Juma na Ditram Nchimbi  waliofunga 2 kila mmoja ingawa Abdalah Juma hakumudu kuitumikia timu kwa kiwango kutokana na majereha ya mara kwa mara.
2015/16 ndiyo msimu pekee ambao City imeshinda mechi mbili pekee ugenini, 2-1 dhidi ya JKT Ruvu, Karume Dar na 1-0 dhidi ya Mgambo JKT, Mkwakwani, Tanga,  huku pia ikivuna pointi 3 za sare ugenini  dhidi ya Toto Africans, Coastal Union na Mwadui Fc.

Kumekucha UEFA Euro Cup 2016! Nani kucheka?

https://i.ytimg.com/vi/cpdvLwDjjms/maxresdefault.jpg
PAZIA la michuano ya Fainali za Kombe la Ulaya 'UEFA Euro 2016' linafunguliwa rasmi leo kwa pambano moja tu la wenyeji Ufaransa dhidi ya Romania.
Pambano hilo linaashiria kuanza kwa vita ya kuwania taji la michuano hiyo ambalo kwa misimu miwili mfululizo limekuwa likishikiliwa na Hispania waliotwaa katika fainali za mwaka 2008 na 2012.
Ufaransa waliowahi kunyakua mara mbili taji hilo mwaka 1984 wakiwa wenyeji na 2000 nchini Ubelgiji/ Uholanzi ikiwa imetoka kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1998 wakiwa pia wenyeji, inapewa nafasi kubwa ya kufanya kweli safari hii wakiwa kama wenyeji, lakini ni kutokana na kuwa na kikosi kinachoundwa na wachezaji mahiri na wajanja wa soka.
Hii ni mara ya tatu kwa nchi hiyo kuandaa fainali hizo baada ya ile ya kwanza mwaka 1960 na 1984, ambako kucheza kwenye viwanja vyake vya nyumbani na mashabiki watakaowatia nguvu na uimara wa kikosi chake ni dhahiri wakilikosa taji Ufaransa itabidi wajutue kwelikweli.
Pambano hili litakalopigwa majira ya saa 4;00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, litatanguliwa na mashamsham ya uzinduzi kabla ya wanaume 22 kuonyeshana kazi kwenye dimba la Stade de France, Saint-Denis likihukumiwa na Mwamuzi Viktor Kassai kutoka Hungary.
pambano hilo la Kundi A linatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kutokana na mafanikio makubwa ya vijana wa Ufaransa katika klabu zao kwenye Ligi Kuu tofauti za Ulaya akiwamo Paul Pogba ambaye kwa sasa amekuwa gumzo kutokana na kuwindwa na klabu kubwa duniani baada ya kutwaa mataji manne mfululizo ya Ligi ya Ufaransa.
Hata hivyo kama wenyeji wanapaswa kuwa makini dhidi ya Romania wanaoumana nao leo na hata washiriki wengine wa kundi hilo zikiwamo Uswisi na Albania.
Kipute cha michuano hiyo kitaendelea kesho Jumamosi kwa mechi tatu, moja ikiwa ya kundi A kati ya Uswisi na Albania itakayopigwa mapema saa 10 jioni na mbili za Kundi B.
Mechi hizo zitazikitanisha Wales dhidi ya Slovakia majira ya saa 1 jioni kabla ya England kuvaana na Russia saa 4 usiku, mechi zinazosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani wakiwamo wa Tanzania.

Ratiba ilivyo kwa leo na kesho ikiwamo ile ya Kombe la Copa America ni hivi;
Leo Ijumaa
8:30 Usiku– Uruguay v Venezuela -Copa
11:00 Alfajiri– Mexico v Jamaica- Copa
4:00 Usiku– France vs. Romania-Uero

Kesho Jumamosi
8:00 Usiku– Chile v Bolivia-Copa
10:30 Alfajiri– Argentina v Panama-Copa
10:00 Jioni– Albania v Switzerland-Euro
1:00 Usiku– Wales    v. Slovakia-Euro
4:00 Usiku– England v Russia-Euro

Thursday, June 9, 2016

Liverpool yaingia vitani kumwania Jamie Vardy

https://metrouk2.files.wordpress.com/2015/04/football-leicester-citys-jamie-vardy-celebrates-after-scoring-their-first-goal.jpg
Jamie Vardy
LIVERPOOL ipo tayari kuingia kwenye vita ya kumwania straika wa Mabingwa wa England, Jamie Vardy.
Kwa mujibu wa Daily Star, The Kop imekuwa ikimwania mkali huyo wa mabao mwenye umri wa miaka 29 kwa misimu miwili sasa.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, tayari ndani ya kikosi chake kina wanaume wa shoka katika safu yake ya ushambuliaji ikiongozwa na Daniel Sturridge, Divock Origi, Christian Benteke na Danny Ings.
Hata hivyo inaelezwa kuwa Vijogoo hao wa Anfield wapo tayari kumuuza mmoja wa mastraika hao, huku Benteke akihusishwa zaidi ili kumpisha Vardy, kwa vile ni kama hayupo kwenye mipango ya Kocha Klopp.
Klabu ya Arsenal imekuwa nayo ikimsaka straika huyo, ila mwenyewe amedaiwa hajaamua lolote kwa sasa mpaka baada ya michuano ya fainali za Euro 2016 inayoanza kesho Ijumaa huko Ufaransa akiiwakilisha nchi yake ya England.

Luke Shaw amtumia ujumbe Mourinho tayari kwa kazi OT

http://static.independent.co.uk/s3fs-public/thumbnails/image/2014/10/28/08/Luke-Shaw-2.jpgYUPO tayari kwa kazi, asikuambie mtu. Beki mahiri  wa pembeni wa Manchester United, Luke Shaw amemtumia ujumbe Kocha wake mpya, Jose Mourinho akisema kwamba yupo fiti kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.
Nyota huyo aliyeshindwa kuitumia Mashetani Wekundu kwa msimu mzima kutokana na kuvunjia mguu mara mbili wakati akiipigania klabu yake katika Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven, alitumia akaunti yake ya instagram kumfikishia ujumbe kocha wake.
"Nipo tayari" alisema Shaw.
Siku baada ya siku naendelea vema na nazidi kuimarika," aliongeza beki huyo wa zamani wa klabu ya Southampton.

Maskini Agger! Aamua kutundika daluga bila kupenda

http://i1.manchestereveningnews.co.uk/incoming/article660491.ece/ALTERNATES/s615/C_71_article_1584808_image_list_image_list_item_0_image.jpgHANA namna. Maumivu ambayo yamekuwa yakimuandama mara kwa mara nyota wa zamani wa Liverpool, Daniel Agger yamemfanya atundike daluga. Agger ametangaza kustaafu soka akiwa  ndio kwanza ana umri wa miaka 31 tu. Beki huyo amekuwa akisumbuliwa kwa kipindi kirefu cha soka lake la majeruhi aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuelezea uamuzi wake huo. Agger aliandika katika twitter akiwashukuru wale wote waliomuunga mkono katika kipindi chote na kuongeza japo ni uamuzi mgumu, lakini anadhani ni sahihi kwa afya yake.
Beki huyo wa kimataifa wa Denmark aliyeondoka Liverpool mwaka 2014 baada ya kuitumikia kwa miaka nane na kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Brondby, amewahi kuichezea nchi hiyo mechi 75. Mkali huyo ameingia katika orodha ya nyota waliowahi kustaafu soka mapema kabla ya wakati wao kwa sababu mbalimbali ikiwamo majeruhi yasiyoisha.

Ronaldo, Messi hawashikiki kwa mkwanja mnene duniani

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgY8PvBrWzFoQIsf0lo44zBa1a5LOgQGVqaoJ90UrwDJJgXi6t_8HUQACiYEVoOsmc7yvAiWq9bU1MxejhpuojP57RhYySRr985IDkhFY-SDoKpnHzRkpsJcPrNdqi1JLmYe4aRX5wQzxo/s1600/lionel_messi_vs_cristiano_ronaldo.jpgWANANUKA pesa. Labda ubishe tu, lakini imefichuliwa kuwa nyota wanaochuana kwa sasa duniani, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndio wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani.
Kwa mujibu wa Jarida maarufu la Forbes la Marekani limewataja nyota hao kuwa vinara duniani kwa kuvuta mkwanja wa maana wakiwazidi wanamichezo wengine.
Nyota wa Real Madrid, Ronaldo ndiye anayeongoza orodha hiyo kwa kukunja kitita cha Pauni Milioni 60.9 katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, huku nyota wa Barcelona Messi akijikusanyia kiasi cha Pauni Milioni 56.3.
Mkali wa mchezo wa Gofu, Tiger Woods na bondia Floyd Mayweather ndio waliokuwa wakitawala orodha hizo kwa muongo mmoja uliopita, lakini Woods akiandamwa na majeruhi na kushuka kiwango na Mayweather akiwa amestaafu Ronaldo na Messi wamepanda na kuongoza orodha hiyo kilaini.
Ronaldo anakuwa mwanamichezo wa pili kutoka katika timu baada ya nguli wa mpira wa kikapu Michael Jordan kuongoza orodha hizo toka jarida hilo lilipoanza kukokotoa vipato vya nyota vya wanamichezo mbalimbali mwaka 1990.
Nyota wengine waliopo katika orodha hiyo ni nyota wa mpira wa kikapu Lebron James anayeshika nafasi ya tatu kwa kuingiza Pauni Milioni 53.4, nyota wa tenisi Roger Federer anashika nafasi ya nne akiingiza Pauni Milioni 46.9 na mkali mwingine wa Kikapu, Kevin Durant anakamilisha Tano Bora kwa kuingiza Pauni Milioni 38.6.
Mastraika matata kwa kufumania nyavu Neymar, Zlatan Ibrahimovic na Gareth Bale ndio wachezaji soka wengine pekee waliopo katika orodha hiyo wakiwa katika nafasi ya 21, 22 na 25 kwa kuingiza kiasi cha Pauni Milioni 25.8, 25.7 na 24.7.