STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 19, 2013

Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa atiwa mbaroni kisa...!





 mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akiwasili  eneo la vurugu kabla  ya kuanza kwa  vurugu  hizo
 Mbunge Msigwa akiondoka  eneo la mashine  tatu 
 Machinga  wakisukuma gari ya  mbunge Msigwa 
 Polisi  wakimfuatilia  mbunge Msigwa kwa  nyuma baada ya  kufika eneo hilo  bila kufanya biashara kama alivyoahidi
Polisi  wakianza  kufukuza  wananchi  eneo hilo


 Polisi  wakipita  eneo la Mashine  tatu asubuhi 
 Abiria  na  wapiga  debe  stendi kuu  wakinawa maji baada ya  kupigwa mabomu na kumwagiwa maji ya kuwasha  na askari  wa FFU leo




 Hali  ikiendelea  kuwa  tete  kwa machinga  kufunga barabara  kuu  ya  Iringa  Dodoma na ile ya mashine  tatu
Ni Machafuko  Iringa  hivi  leo








Warembo Miss Tabata 2013 kutembelea Mbuga ya Mikumi

Miss Tabata wakiwa kwenye pozi ya picha ya pamoja



WAREMBO watakaoshiriki kinyang'anyiro cha shindano la Miss Tabata 2013 watatembelea mbuga ya  wanyama ya Mikumi wikiendi ijayo.

Mratibu wa shindano hilo Godfrey Kalinga mapema leo kuwa, lengo la ziara hiyo ni kukuza utalii wa ndani. Alisema kuwa warembo hao pia watapata fursa ya kujua vivutio vilivyomo kwenye mbuga hiyo iliyoko mkoani Morogoro.

“Hii siyo mara yetu ya kwanza kuwapeleka warembo wetu mbugani. Tumekuwa tukifanya kila mwaka,” alisema Kalinga.

Kapinga alisema kuwa ziara hiyo imedhaminiwa na CXC Africa.



Shindano la kumsaka Miss Tabata  litafanyika Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.

Wadhamini wa shindano hilo ni Nipashe, Redds, Dodoma Wine, Nipashe, Vayle Springs, Multichoice, Fredito Entertainment, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.

Warembo watakaoshiriki kwenye shindano hilo linaloandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts ni Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Upendo Dickson Lema (22), Hidaya David Mwenda (22), Aneth Ndumbalo (19),  Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Musa Kitereja (19),  Rehema Kihinja (20),  Pasilida Mandali (21), Brath Chambia (23), Joaniter Kabunga (21), Recho Mushi (20),Caroline Sadiki (20) na  Suzan Daniel (18).



Warembo watano watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.

Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.

Simba na Yanga zaingiza Mil, 500, zenyewe zazoa Mil. 250

Simba na Yanga zilipoumana jana uwanja wa Taifa
Na Boniface Wambura
PAMBANO la watani wa jadi Simba na Yanga la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 limeingiza sh. 500,390,000.

Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati kile cha sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh. 123,515,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ya Ligi sh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,910,819.44 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,708,415.12.

Golden Bush Veterani yaendeleza ubabe Dar

Wakali wa soka la maveterani Dar, Golden Bush
GOLDEN Bush Veterani, maarufu kama 'Wakali wa Soka la Maveterani Dar' kama kawa asubuhi ya leo wameendelea kuzinyanyasa timu za wazee jijini humo baada ya kuwanyuka Ukonga Veterani kwa mabao 2-0.
Timu hiyo ilipata ushindi katika michezo ya Bonanza iliyofanyika kwenye viwanja wa Staki Shari, Ukonga ambapo wakali hao waliwacharaza wapinzani wao hao.
Mabao ya Di Natale na 'kisiki' wa zamani wa Moro Utd na Yanga, Yahya Issa yalitosha kuizamisha Ukonga Veterani na kuwafanya Golden Bush kurejea maskani mwao wakichekaaa kwa ushindi huo.
Msemaji wa klabu hiyo, Onesmo Waziri 'Ticotico' alisema licha ya ushindi huo bado hakufurahishwa kwa vile walipania kutoa kipigo zaidi ya hicho.
Ticotico alisema wamekuwa na mazoea ya kuzigonga timu pinzani mabao kuanzia manne hiyo ushindi wa 2-0 wanaona kama hawakutenda haki kwa Ukonga.

Saturday, May 18, 2013

Wanawake Mbeya wamcharukia Mchumba wa Dk Slaa kwa kumkashifu Mama Salma Kikwete


UMOJA wa wanawake  wa chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya(UWT) umemshukia Bi.Josephine Mushumbusi ambaye ni mchumba Katibu Mkuu wa chama cha
Demokrasia na maendeleo CHADEMA kufuatia kauli za udhalilishaji dhidiya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.



Hatua hiyo inatokana  na kauli za kiudhalilishaji zilizotolewa mwishoni mwa wiki na mchumba huyo wa Katibu Mkuu wa Chadema kuwa mama Kikwete ameshindwa kumshauri   Rais ambaye ni mume wake  kuiongoza nchi vizuri.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Mbeya Bi.Priscilla Mbwaga wakati  akitoa Tamko   kwa waandishi wa habari juu ya Matusi ya wazi yaliyotolewa na Bi.Mushumbusi   kwa Mke wa Rais katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Wilayani Mbozi Kata ya Vwawa Mkoani hapa.

Bi.Mbwaga alisema kuwa katika mikutano yake ya Hadhara Bi.Mushumbusi alidai kuwa  mama Salma Kikwete  ameshindwa kumshauri  mume wake kuingoza nchi na kuacha Twiga wakiwa wanakunjwa na kuondoka na kwamba yeye akiwa Ikulu hataacha kumshauri mume wake Dkt.Slaa katika masuala ya kuingoza Nchi

 
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kama umoja huo wanalaani  vikali lugha chafu na za kichochezi zinazopandikizwa  chuki miongoni mwa jamii ya watanzania .

Alisema kuwa kama umoja wa wanawake  wanalaani matusi hayo na kwamba umoja huo  ulifuatilia  mikutano  hiyo na kugundua kuwa ilikuwa imetawaliwa  na  matusi badala ya kutoa sera  kwa wananchi kuwa wanataka kufanya nini.

“Sisi kama umoja wa wanawake  Mkoa tunaeleza umma  ambao una imani na  kuwa katika utamaduni   na maadili  yao hawapendi  na wala hawajazoea kusikia matusi  katika  jamii yao hivyo wakiangalie vizuri na kwa  makini Chadema  kuwa  cha hicho kina  watu  wa maadili gani , mahali  pote  siku zote  na miaka  yote  ni matusi,kuongea uongo, uzushi  na kashfa wasimamapo majukwaani “alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha Bi.Mbwaga alisema kuwa wanawake wa mkoa wa Mbeya  wanadhani kuwa kauli ambazo zimetolewa na  Mushumbusi ni  ni za kuwadhalilisha wanawake wote wa Tanzania  kwani Mama Salma ni Kiongozi wa juu pamoja
na Mushumbusi .


“Tunamshangaa sana  Mushumnbusi anaposimama majukwaani na kutoa kashfa nzito za namna hii ni  kama nani kwa wanawake  wa Tanzania 'alihoji Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoani hapa (CCM),Bw.Amani Kajuna  alisema  kauli aliyotoa Dkt.slaa kuwa Rais Kikwete  ana Udini ni ulaghai  mkubwa  ambao anaufanya kwa wananchi  na kuendelea kuiweka nchi katika mazingira magumu .

“Kama vijana  tunatambua kuwa  Rais Kikwete ni kiongozi wa watanzania, na kwamba hana sifa ya Udini hii ajenda inaanzishwa kisiasa ili kujipatia umaarufu wa bure wa kudhani kuwa ndiyo njia ya kuwapeleka ikulu  mwaka 2015 jambo ambalo halitawezekana ,maana  watanzania hawataweza kukubali" alisema Mwenyekiti huyo.


Hata hivyo Bw.Kajuna aliendelea kusema kuwa Dkt. Slaa amekuwa akimtuhumu  Rais Kikwete kuwa  ni FREEMASON , “hebu tumuulize huyu mtu amekutana lini na Rais kwenye iman hiyo” na kwamba katika uongozi wake watanzania  wameona miradi mikubwa  ya maendeleo ya nchi yetu kwa ukuaji wa wa pato la Taifa.
 
CHANZO:MPEKUZI HURU

Hivi Ndivyo Yanga walivyoitambia Simba Taifa

Beki wa Simba, Musa Mudde (kushoto) akichuana na mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo. 
Beki wa Simba, Shamte Ramadhani akimtoka mshambuliji wa Yanga, Simon Msuva
Nahodha wa Yanga, Nidir Haroub 'Canavaro' akiwa amenyanyua kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara pamoja na wachezaji wenzake.
Shabiki wa Yanga akipelekwa kupewa huduma ya kwanza baada ya kuzimia wakati mchezo ukiendelea.
Kikosi cha Simba.
Makocha wa yanga wakipanga mikakati ya Ushindi.
Timu zikiingia uwanjani.
Timu zikisalimiana.
Kocha wa Simba, Patrick Liewig
Kocha wa Yanga, Ernst Brandts
Beki wa Simba, Shomari Kapombe akimtoka mshambuliji wa Yanga, Simon Msuva
Msanii Juma Nature akitumbuiza wakati wa mchezo huo. 
Mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa Yanga. 
Mashabiki wa Yanga.
 Raha ya ushindi.
 Kocha wa Yanga, Ernst Brandts akiwa amebebwa na wachezaji wake.
 Kiduku
KARIBU JANGWANI NGASA
Mashabiki wa Yanga wakiwa wamembeba mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa mara baada ya mpira kumalizika, ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika klabu yao. 

Mashabiki wa yanga.
Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuifunga Simba 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa  jijini Dar es Salaam
Kipa wa Simba, Juma Kaseja akijaribu bila mafanikio kuokoa mpira wa kichwa uliopigwa na mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu katika mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

KARIBU NYUMBANI
Mashabiki wa Yanga wakiwa wamembeba mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa mara baada ya mpira kumalizika, ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika klabu yao. 
Refa wa mechi ya Simba na Yanga, Nartin Saanya akiwa chini baada ya kugongwa kwa bahati mbaya na mchezaji wa Yanga, Didir Kavumbagu.
Refa, Martin Saanya akipata matibabu.
 
PICHA ZOTE NA FRANCIS DANDE WA HABARI MSETO

Majina ya wanavyuo walionaswa wakijiuza haya hapa



Wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha Dar es salaam [UDSM],Chuo cha elimu ya biashara [CBE]na chuo cha mamlaka ya Elimu na ufundi  stadi [VETA],Dar es salaam ,wamefikishwa katika mahakama ya jiji samora wakidaiwa kufanya biashara ya kuuza mili yao.

Washitakiwa hao waliokamatwa  katika eneo la kona Baa Ambiance Sinza wilayani kinondoni ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo na wote walifikishwa mahakamani hapo.

Kesi hiyo ilikuwa chini ya hakimu Willian Mtaki ambapo muendesha mashitaka,bwana John Kijumbe,alisema wasichana hao walikamatwa katika mazingira tofautitofauti.

Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye miaka 21 CBE mkazi wa upanga,Morin Masatu miaka 19 UDSM,mkazi wa kinondoni na mwanafunzi wa VETA aliyefahamika kwa jina moja la Khadija.

“Nilikwenda pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita nikaichukue ndipo askari wa jiji wakanikamata,”Alisema Khadija akijitetea.

Kwa mujibu wa bw. Kijumbe washitakiwa  hao wamekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili au kulipa faini ya kulipa sh. 200,000.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena mei 28 mwaka huu,ambapo washitakiwa wote walipelekwa Segerea.

Wakati huohuo, jeshi la Polisi mkoa wa kinondoni , limewakamata watuhumiwa 716 waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili kati yao wanaume 38 na wanawake 678.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, alisema watu hao walikamatwa kwenye msako uliodumu kwa miezi sita kwenye maeneo mbalimbali ya Kinondoni.

Maeneo hayo ni baa, kumbi za starehe, madanguro, sehemu za wazi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, na makaburini ambapo kati ya wanaume waliokamatwa wengine ni mashoga pamoja na wateja wa machagudoa.

“Msako huo ulifanyika Maisha   Club, Coco Beach, Barabara ya Tunisia , Travertine Hotel, Tandale Uwanja wa Fisi, Ambiance Club, Shekilango pamoja na Mwinanyamala” Alisema

Kamanda Kenyela aliongeza kuwa , jeshi hilo pia limewakamata raia 12 kutoka nchini Ethiopia walioingia nchini bila kibali kati ya Mei 2 na 6, mwaka huu katika eneo la Kimara Mwisho na Tegeta Kibaoni.

Alisema kukamatwa kwao kulitokana na taarifa walizozipata kutoka kwa raia wema waliowaona maeneo.


Credit:Mpekuzi Huru

Mbunge Chadema aanguka ghafla Bungeni


Mhe. Taratibu Abama
MBUNGE wa Viti Maalum, pichani Mwanamrisho Taratibu Abama (Chadema), ameanguka  bungeni, baada ya kujisikia vibaya.

Mbunge huyo alianza kujisikia vibaya, hali iliyomfanya kuketi katika viti vilivyo karibu na zahanati ya Bunge.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia walisema mbunge huyo alipata huduma ya kwanza katika zahanati hiyo kwa zaidi ya saa mbili kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya  Rufaa ya Mkoa ya Dodoma.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya hospitali hiyo, zinasema mbunge huyo alilazwa wodi namba 18.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk. Zainab Chaula, alithibitisha kupokelewa kwa mbunge huyo.
“Ni kweli yupo hapa  na hali yake inaendelea vizuri sasa ,”alisema.