STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, July 17, 2013

Dude ndiye 'Yahaya' wa Lady Jaydee

Na Elizabeth John
MSANII wa filamu za bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ anatarajia kucheza kama ‘Yahaya’ katika video ya wimbo huo, ulioimbwa na mwanadada Judith Wambura ‘Lady Jaydee’.
Mwanadada huyo ameanza kushuti video ya wimbo huo juzi katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Lady Jaydee alisema anawashukuru mashabiki wake kwa kumpokea vizuri katika tasnia ya muziki ukiwa ni pamoja na mapokezi ya ngoma hiyo.
“Kiukweli sikutegemea kama Watanzania wananikubali kupita kiasi kama walivyonionesha katika wimbo huu wa ‘Yahaya’, naomba wakae mkao wa kula kupokea video yake ambapo Dude atacheza kama Yahaya,” alisema.
Alisema anawaomba watanzania waendelee kumpa sapoti katika kazi zake zinazofuata ikiwa ni pamoja na kukaa mkao wa kula kwaajili ya video ya wimbo huo ambao unafanya vizuri kwasasa katika vituo mbalimbali vya redio.

No comments:

Post a Comment