Na Suleiman Msuya
WIZARA ya
Maliasili na Utalii kupitia Idara ya
Wanyamapori imesema zaidi ya tembo 475 wameuwawa na majangili kwa kipindi cha
mwaka 2012/13 ambapo watuhumiwa 1215 walikamatwa kwa makosa mbalimbali.
Mkurugenzi wa
Wanyamapori, Profesa Alexander Songoro pamoja na watuhumiwa hao pia jumla ya
bunduki 85 na risasi 215 za aina mbalimbali zilikamwata na kesi 670
zilifunguliwa katika mahakama za hapa nchini, ambapo kesi 272 zimekamilika kwa
washitakiwa 247 kulipa faini ya jumla ya
Sh175,002,420 na washitakiwa 71 kupewa adhabu ya vifungo vya jumla ya
miaka 99.
Alisema kesi 398
zenye jumla ya washitakiwa 897 bado zinaendelea katika mahakama mbalimbali
nchini ambapo wanaamini kuwa zitakamilika hivi karibuni.
"Kimsingi
ndugu zangu wanahabari hali ya ujangili ni kubwa sana kwani kwa kipindi cha
mwaka jana zaidi ya tembo 475 waliuuwawa hali ambayo inahitaji juhudi zaidi
ziongezeke ili kukabiliana na hali hiyo," alisema Profesa Songoro.
Alisema vita dhidi
ya ujangili ni ngumu hasa ukizingatia kuwa baadhi ya watanzania wanaamini kuwa
jukumu la kulinga wanyamapori ni la Serikali pekee hasa maofisa wanyama pori
jambo ambalo ni dhana potofu.
Songoro alisema ni
vema Watanzania wakatunza wanyamapori kwa kutambua kuwa asilimia 90 ya utalii
hapa nchini unategemea wanyamapori kwa watalii wengi kutmbelea maeneo yenye
wanyamapori.
Alisema utalii wa
wanyamapori ndio umebeba uchumi wa Taifa kwa kutoa huduma mbalimbali kama vile
madawa, vitabu na kujenga maabara na huduma zingine za kijamii.
Kaimu Mkurugenzi wa
Msaidizi Kitengo cha Kuzuia Ujangili, John Muya alisema migogoro inayotokea
katika maeneo ya hifadhi za wanayamapori inatokana ongezeko la binadamu na wanyama jambo ambalo linachangia kuwepo kwa mwingiliano
wa makazi .
Alisema binadamu
wamekuwa wakiingia na kuweka makazi katika maeneo ambayo wanyama wapo jambo
ambalo wakati mwingine linachangia vifo vya wananchi bila sababu za msingi.
Pia alisema ufinyu
wa watumishi katika mapori yenye kuhifadhi wanyamapori ni moja ya sababu nyingine
ya kukosekana kwa udhibiti wa wanyamapori ambao wanaingia katika makazi ya
watu.
Muya alisema
kuongezeka kwa ujangili wa nchini
kunachangiwa na Watanzania wenyewe ambapo kuna wenye fikra potofu juu ya
baadhi ya maeneo ya wanyama wanaouwawa ambapo tembo anaongoza.
jaman tuwe makin sana na hawa wanaojitokeza kujifannya wana dawa za ukimwi ili tusihje tukaibiwa hela zetu jaman
ReplyDelete