STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, July 17, 2013

Kivuli cha van Persie chamtesa Rooney United

Wayne Rooney
IMEBAINIKA kwamba 'kivuli' cha Robin van Persie kilichomfunika mshambuliaji nyota wa Manchester United, Wayne Rooney, ndicho kinachomfanya mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England atake kuondoka klabuni hapo japo klabu yake imedai hauzwi.
Kwa mujibu wa duru za soka nchini England zinasema, Rooney amekuwa akiumia kucheza kama chaguo la pili ndani ya United katika safu ya ushambuliaji nyuma ya Mholanzi huyo aliyeibuka Mfungaji Bora wa EPL ikiwa ni msimu wake wa kwanza tangu atue Old Trafford akitokea Arsenal mwaka uliopita.
Chanzo cha karibu cha mchezaji huyo kimenukuliwa kikisema kuwa, Rooney 'amechukia na kuchanganyikiwa' baada ya kocha mkuu wa timu hiyo David Moyes kueleza wazi bado ataendelea kumuamini van Persie kama ailivyokuwa kwa mtangulizi wake.
Mchezaji huyo anayelipwa pauni 250,000 kwa wiki anaamini enzi zake baada ya miaka tisa ndani ya OT iliyomsajili kwa kitita cha pauni Milioni 26 akitokea Everton, ambapo tangu atue United ameifungia mabao 198 mpaka sasa.
Rooney amekuwa akiwinda na klabu mbalimbali baada ya kubainika hana amani OT licha ya klabu yake kusisistiza kuwa mchezaji huyo HAUZWI.

No comments:

Post a Comment