STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, July 17, 2013

Golden Bush Fc yaonja kipigo Ligi Kinondoni

Kikosi cha Golden Bush Fc
TIMU ya soka ya Golden Bush Fc inayoshiriki Ligi Daraja la Nne Wilaya ya Kinondoni kwa mara ya kwanza jana imeonja machungu ya vipigo baada ya kukubali kulazwa bao 1-0 na Kijitonyama Fc.
Hicho ni kipigo cha kwanza kwa timu hiyo inayocheza ligi hiyo kwa mara ya kwanza na uongozi wa timu hiyo umesema ni changamoto kwao kujipanga vyema kwa mechi ijayo dhidi ya Shein Rangers.
Kabla ya hapo Golden Bush inayonolewa na makocha Shija Katina na Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio' ilikuwa imeshinda mechi nne na kuongoza kundi lao linalotumia uwanja wa Itihad.
Hata hivyo huenda timu hiyo imeteleza baada ya ligi hiyo kusimama kwa muda mrefu na kuipunguzia kasi  timu hiyo ambayo hivi karibuni ilifanikiwa kumvutia wakala wa soka wa kimataifa toka Msumbiji, Ashraf ambaye alitangaza kumchukua mchezaji mmoja wa klabu hiyo ili kwenda kucheza soka la kulipwa nchini mwake.
IKwa mujibu wa uongozi wa klabu hiyo watarekebisha makosa yaliyojitokeza katika mechi yao ya jana ili kuweza kufanya vyema kwa mechi zao zilizosalia ambapo inahitaji kushinda mechi tatu ili kujihakikisha kusonga mbele kwenye ligi hiyo kuwania kupanda Daraja la Tatu.

No comments:

Post a Comment