STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, July 17, 2013

Msiba mwingine katika tasnia ya muziki Tanzania

MCHARAZAJI wa gitaa la besi wa zamani wa kundi la Jahazi Modern taarab, Juma 'Mgunda' (Jino Moja), amefariki dunia mchana wa leo baada ya kuugua ghafla.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanamuziki wenzake, Ramadhani Kisolo, ni kwamba Jino Moja aliyekuwa akipigia makundi ya mtaani baada ya kutemwa na Jahazi, alifariki saa 7 mchana na bado haijafahamika atazikwa lini kwa sababu ndugu na jamaa bado walikuwa wakipanga mipango ya mazishi yake.
Taarifa zaidi za msiba wa mwanamuziki huyo aliyekuwa akitajwa sana katika nyimbo za kundi la Jahazi tutazidi kuwaletea

No comments:

Post a Comment