Edinson Cavani |
MSHAMBULIAJI nyota wa Uruguay aliyekuwa akiwinda na timu za Real Madrid, Manchester City na Chelsea, Edinson Cavani, ameamua kuuma jongoo kwa meno kwa kuzitosa timu hizo na kutua PSG ya Ufaransa kwa donge nono la karibu Euro Milioni 64 (Sh Milioni 126) kwa mkataba wa miaka mitano.
Dau lililomhamisha nyota huyo toka Napoli mpaka Ufaransa imemfanya avunje rekodi ya dau la uhamisho nchini humo lilililokuwa likishikiliwa na Radamel Falcao alipohamia Monaco hivi karibuni akitokea Atletico Madrid ya Hispamia aliyesajiliwa kwa donge nono la Euro Milioni 60.
Mchezaji huyo alifanikisha usajili wake huo kwa mabingwa hao wa Ligue 1 jana na kumfanya auange na mchezaji mwenzake wa zamani wa Napoli, Ezequiel Lavezzi.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay amefunga magoli zaidi ya 20 kwa kila msimu katika misimu mitatu iliyopita ya Serie A, Ligi Kuu ya Italia na kuisaidia Napoli kumaliza kwenye nafasi ya pili msimu wa 2012-13, hivyo kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kuanzia hatua ya makundi.
Juzi, rais wa klabu hiyo De Laurentiis alinukuliwa kwamba kama PSG isingetangaza dau hilo isingekuwa tayari kumuachia mshambuliaji huyo ambaye aling'ara kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo PSG ilifika Robo Fainali.
No comments:
Post a Comment