Vijana wa Golden Bush wakiwa mazoezini na kocha wao Shija Katina (kushoto) wakipeana mikakati ya kusaka ushindi katika Ligi daraja la Nne wanayoicheza kwa mara ya kwanza |
BAADA ya wiki iliyopita kutibuiliwa rekodi yake ya ushindi mfululizo kwa kulazwa na Kijitonyama, timu ya Golden Bush Fc jana ilizinduka katika Ligi Daraja la Nne wilayani Kinondoni kwa kufanya 'mauaji' ya kutisha dhidi ya Shein Rangers kwa kuinyuka mabao 4-1.
Pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam lilishuhudia vijana wa Golden Bush inayonolewa na kocha Shija Katina na Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio' wakicharuka tangu mwanzo wa mchezo ili kurejesha heshima yake katiika lig hiyo.
Vijana hao walipata mabao yao yaliyotosha kuwafanya wafikishe pointi 15 katika kundi lake baada ya kucheza mechi 6 yalitumbukizwa kimiani na aliyekuwa nyota wa mchezo, Adilu aliyefunga mawili, Said na Kenan.
Timu hiyo inatarajiwa kushuka tena dimbani siku ya alhamis, ambapo uongozi wa timu hiyo umesema vijana wao watashuka wakiwa na lengo moja tu la kuendeleza vipigo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya pili na hatimaye kuipanda Ligi Daraja la Tatu.
No comments:
Post a Comment