STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, July 1, 2014

Young Hassanal kumbe ni Mr Pendwapendwa

Muimbaji Hassani Ally
MUIMBAJI nyota wa muziki wa taarab wa kundi la Kings Modern, Ally Hassan 'Young Hassanal' anajiandaa kuingiza sokoni albamu yake binafsi ya 'Nyongo Mkalia Ini', huku akiendelea kutamba na wimbo mpya wa 'Mr Pendwapendwa'.
Wimbo huo upo kwenye albamu ijayo ya kundi lake la King Modern inayoandaliwa kabla ya kuja kuachiwa baadaye.
Akizungumza na MICHARAZO, muimbaji huyo alisema kuwa albamu yake aliyoizindua Machi mwaka huu itaingia sokoni wakati wowote kuanzia sasa ili mashabiki wake waipate.
"Naada ya uzinduzi uliofana kwa sasa nipo hatua za mwisho kabla kuingiza sokoni albamu yangu ya 'Nyongo Mkalia Ini'," alisema.
Young Hassanal aliongeza, wakati akijiandaa kuingiza sokoni albamu hiyo, kundi lake la Kings lipo katika maandalizi ya mwisho kukamilisha albamu yao mpya itakayokuwa na nyimbo tano.
"Albamu hiyo tayari inatambaulishwa hewani na wimbo nilioimba wa 'Mr Pendwapendwa' ambao unafanya vyema kwenye vituo vya redio," alisema.No comments:

Post a Comment