Mwqenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe |
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema haitambui
kuondolewa kwa kipengele cha ukomo wa uongozi uliofanywa na Chadema bila
kufuata idhini ya mkutano mkuu wa chama hicho.
Mwaka
2006, Katiba ya Chadema ilifanya marekebisho yaliyoruhusu wanachama
kugombea uongozi bila ukomo wakati awali, waliruhusiwa kugombea kwa
vipindi viwili vya miaka mitano.
Barua
ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwenda kwa Katibu
Mkuu wa Chadema, inasema kipengele hicho katika Ibara ya 6.3.2 (C)
kiliondolewa kwenye katiba bila idhini na mkutano mkuu wa chama hicho.
Mutungi alisema baada ya
kupitia muhtasari wa kikao cha mkutano mkuu wa mwaka 2006 suala la
kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi halikuonyesha kujadiliwa katika
mkutano huo.
Hata hivyo, akizungumza kwa simu jana, Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema kipengele hicho kiliondolewa kwa
vikao vya chama ambavyo ni wilaya na mkoa.
“Mjadala
kuhusu ukomo wa uongozi ulishamalizika na haujadiliwi tena,
ulishapitishwa na vikao halali vya chama, mkutano mkuu ulipitisha yale
yaliyoamuliwa na vikao vya chini,” alisema Dk Slaa.
Hata hivyo, Jaji Mutungi alisema: “Chadema wamefanya mabadiliko bila kufuata katiba”
Alishauri
waitishe mkutano rasmi na halali kwa mujibu wa katiba ya chama hicho
ili waweze kurekebisha kasoro zilizopo.
Alisema kama chama hicho
hakitarekebisha kasoro hiyo, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haiwezi
kuitambua ibara hiyo.
Alisema ingawa hoja hiyo iliwasilishwa na
aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ambaye
sasa si mwanachama wake, bado hoja hiyo ni muhimu na inahitaji kufanyiwa
kazi.
“Ni
vizuri mkaifanyia kazi hoja hiyo bila kujali kwamba aliyeiwasilisha si
mwanachama tena wa Chadema,” alisema katika barua hiyo.
Credit:Info is Hot
No comments:
Post a Comment