MABINGWA wa zamani wa kandanda nchini Yanga imeendelea kujipanga na mikakati ya kurudisha ubingwa walionyang'anywa na Azam msimu uliopouta kwa kumsainisha kiungo mshambuliaji kutoka Brazil.
Kiungo huyo Andrey Marcel Ferreira Coutinho raia wa Brazil jana alisaini mkataba wa miwili kuitumikia timu ya Young Africans (Yanga) kwa
ajili ya michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na
mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Katibu mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema usajili wa
mchezaji Coutinho ni sehem ya muendelezo wa maandalizi ya msimu mpya wa
Ligi Kuu na kama ilivyokawaida wao mambo yao ni kimyakimya.
Coutinho ambaye alizaliwa tarehe 12 Januari 1990 amekulia kwenye mji
wa Berem ambapo alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Paysandu
Sports Club kabla ya kwenda nchini Asia katika nchi ya Myanmar katika
klabu ya Rukhapura United.
Mpaka anajiunga na klabu ya Young Africans Andrey Coutinho alikuwa
akichezea timu ya Castanhal EC iliyopo kwenye Ligi Daraja la pili ambao
aliweza kuichezea kwa michezo yote ya mzunguko wa pili mwaka 2014.
Katika hatua nyingine kikosi cha Young Africans kinatarajia kuendelea
na mazoezi kesho chini ya kocha Marcio Maximo katika ufuke wa Coco
Beach ikiwa ni siku yake ya kwanza kuanza kazi baada ya leo kuwa na
mkutano wa ndani na wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi.
No comments:
Post a Comment