STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 25, 2014

Ndanda yazamishwa tena nyumbani, Mgambo wawapigisha kwata

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgSvHwYqtPQMuzPoWUu4QCWVjjgvVwLySqdBYExhW-LxDkl-tjqI3X__y-_vwNzmO6A72piQEbxsK79AqJ8vub5o2bTvjx1VL8FqSFT_-uMryVYDTOmZZVv18G_WiMV4YrQE_D_be0p_aWy/s1600/20140913_160438.jpg
Ndanda FC iliyopigwa tena nyumbani
TIMU ya soka ya Ndanda Fc ikicheza bila ya kocha aliyeipandisha daraja, Dennis KItambi imeendelea kutoa 'takrima' nyumbani baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Mgambo JKT kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara.
Pambano hilo ni la pili kwa Ndanda kulala nyumbani baada ya awali kulazwa mabao 3-1 na Ruvu Shooting na kusababishwa kutimuliwa kwa Kitambi aliyeoonekana pengine ni kikwazo cha timu hiyo kufanya vema.
Bao lililoizamisha Ndanda ikiwa na koicha mpya Hamim Mawazo liliwekwa kimiani dakika ya tatu tu ya mchezo kupitia Ali Nasoro Idd.
Katika mchezo mingine Ruvu Shooting imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Moro katika pambano lililochezwa uwanja wa Mabatini, Mlandizi Pwani.
Bao pekee la mchezo huo liliwekwa kimiani na Zubeiry Dabi dakika ya 68 na kuifanya Ruvu kushinda kwa mara ya pili mfululizo na kufikisha pointi 7.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kwa pambano moja tu kati ya Mbeya City itakayoikaribisha Mtibwa Sugar kwenye dimba la Sokoine, jijini Mbeya.
Timu hizo zitakutana huku Mtibwa ikiwa kileleni mwa msimamo ikilingana pointi na timu za Yanga, Azam wakati Mbeya ikiwa na pointi tano baada ya mchezo uliopitwa kuzimwa nyumbani 1-0 na Azam fc.

No comments:

Post a Comment