Rama Salim (kushoto) na Emmanuel Okwi ambao wameendelea kufunga mabao katika Ligi Kuu na kumbeep Didier Kavumbagu |
Rama alifunga bao la kusawazisha la Coastal na kumfanya kushika nafasi ya pili akilingana na Ally Shomar wa Mtibwa wakiwa na mabao matatu, moja pungufu dhidi ya manne ya Kavumbagu.
Kadhalika Jerry Tegete ameanza na moto baada ya magoli yake mawili aliyofunga leo Shinyanga yamemfanya kuingia kwenye orodha ya wanaowania Kiatu cha Dhahabu.
Mshambuliaji huyo ameungana na wachezaji wengine saba kushika nafasi ya tatu sambamba na Emmanuel Okwi aliyefunga jioni ya leo dhidi ya Prisons-Mbeya.
Wakati katika mbio za ufungaji bora ikiwa hivyo, Mtibwa itakayoshuka dimbani kesho ugenini ikiwa ni kati ya timu mbili ambazo hazijaonja machungu ya kipigo sambamba na Simba, itaumana na Mbeya City baada ya kurejea kileleni kutokana na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Awali Azam waliwatangulia kwa faida ya herufi A wakiwa wamelingana kila kitu kabla ya leo kutibuliwa na JKT Ruvu waliowafumua bao 1-0 uwanja wa Chamazi na kushuka had nafasi ya pili licha ya timu kuwa na pointi 10 sawa na Yanga ambayo imerejea nafasi ya tatu.
Hata hivyo Mtibwa ina nafasi nzuri kwa vile ina mchezo mmoja mkononi kulinganisha na wenzake waliocheza mechi tano kila moja dhidi ya nne za Mtibwa.
Matokeo mengine ya ligi hiyo jioni ya leo imebadilisha msimamo maeneo ya kati na mkiani baada ya Mgambo kujinasua mkiani kwa kushinda 1-0 dhidi ya Ndanda na kufikisha pointi sita zilizowapeleka hadi nafasi ya nane wakilingana na Kagera Sugar waliolazimishwa sare ya 1-1 na Coastal.
Nazo timu za maafande wa JKT, Ruvu Shooting na JKT Ruvu zimefanikiwa kupanda hadi kwenye nafasi ya tano na sita kwa kufikisha pointi 7 baada ya kupata ushindi wa pili mfululizo timu zote hizo zikiwa zinalingana kwa kila kitu isipokuwa wakitenganishwa kwa herufi zao za mwanzo, JKT wakiitangulia Ruvu.
Unaweza kuuchungulia msimamo wa ligi hiyo na orodha ya wafungaji kujionea mwenyewe.
MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
P W D L F A GD Pts
01. Mtibwa Sugar 04 03 01 00 06 01 05 10
02. Azam 05 03 01 01 06 02 04 10
03. Yanga 05 03 01 01 07 04 03 10
04. Coastal Union 05 02 02 01 07 05 02 08
05. JKT Ruvu 05 02 01 02 04 05 -1 07
06. Ruvu Shooting 05 02 01 02 04 05 -1 07
07. Kagera Sugar 05 01 03 01 04 03 01 06
08. Mgambo JKT 05 02 00 03 02 04 -2 06
09. Prisons 05 01 02 02 05 05 00 05
10. Simba 05 00 05 00 05 05 00 05
11. Mbeya City 04 01 02 01 01 01 00 05
12. Stand Utd 05 01 02 02 03 08 -5 05
13. Ndanda Fc 05 01 00 04 07 10 -3 03
14. Polisi Moro 05 00 03 02 03 06 -3 03
Wafungaji Bora:
4- Didier Kavumbagu(Azam)
3- Ally Shomari (Mtibwa), Rama Salum (Coastal)
2- Shaaban Kisiga, Emmanuel Okwi (Simba), Nassor Kapama (Ndanda), Ame Ally (Mtibwa), Rashid Mandawa, Salum Kanoni (Kagera), Aggrey Morris (Azam), Jabir Aziz (JKT Ruvu), Jerry Tegete (Yanga)
No comments:
Post a Comment