STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 25, 2014

Southampton yaendeleza rekodi England, West Brom chupuchupu

Sadio Mane, Southampton
Southampton wakishangilia bao lao leo
Mile Jedinak scored his second penalty of the season to give Crystal Palace a 2-0 half-time lead at West Bromwich Albion
West Brom walipokuwa wakiadhibiwa kabla ya kuchomoa mwishoni
BAO pekee lililofungwa na Msenegal Sadio Mane katika dakika ya 33 limeiwezesha Southmpton kupata ushindi mwembemba dhidi ya Stoke City na kuendeleza rekodi ya kutofungika nyumbani.
Ushindi huo umeifanya Southampton kufikisha pointi 19 na kukwea hadi nafasi ya pili wakiwaengua mabingwa watetezi Manchester Citry waliocharazwa mabao 2-1 katika mechi ya mapema leo Jumamosi na kupunguza pengo la pointi kati yao na vinara Chelsea wanaoongoza kwa pointi 22 na wakitarajiwa kushuka kesho kuumana na Mashetani Wekundu uwanja wa Old Trafford.Katika mechi nyingine za Ligi Kuu ya England, West Bromwich Albion wakiwa nyumbani walichomoa kipigo toka kwa Cryastal Palace kwa kulazimisha sare ya mabao 2-2.
Wenyeji walisubiri hadi dakika ya 90 kuchomoa bao kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Saido Berahino ambapo kabla ya hapo Victor Anichebe alifunga bao la kwanza dakika ya 51 na kufanya matokeo kuwa 2-1.
Wageni walipata mabao yao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa  Hangeland aliyefunga dakika ya 16 kabla ya Jedinak kuongeza la pili sekunde chache kabla ya mapumziko kwa mkwaju wa penati na kuwapa Stoke uongozi wa 2-0 wakati wa mapumziko.

No comments:

Post a Comment