Jonas Nkya, mtoto wa Waziri wa Afya wa zamani nchini Dk Lucy Nkya ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM-Moro |
MAPEMA leo kwenye mitandao mingi kulikuwa na taarifa zinahusiana na tukio la kurushiana risasi baina ya
aliyekuwa Naibu Waziri wa zamani wa Afya na Mbunge wa Morogoro Kusini
Mashariki Dk. Lucy Nkya na mtoto wake ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa
Vijana wa CCM Morogoro Jonas Nkya.
Waziri wa zamani wa Afya Dk Lucy Nkya ambaye ni Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki |
Tukio hilo ambalo limetokea leo Morogoro
baina ya wanafamilia hao, limehusishwa na ugomvi wa kifamilia jambo
ambalo limeamsha hisia tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari
Morogoro, Jonas Nkya amekanusha taarifa za kurushiana risasi na kueleza
kuwa tukio hilo ni tukio la bahati mbaya baada ya bunduki yake kudondoka
na kupelekea risasi mbili kufyatuka.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo, Jonas
amesema, “.. silaha inakaa kiunoni, nakwenda kwenye gari nashuka pale
ofisini pisto hii imeanguka imejipiga risasi mbili nje ya ofisi. Sasa
nadhani majirani wakaogopa sijui mi sielewi, lakini kuna watu wanaishi
pale. Sasa ndio ikafika hapo wakaja Polisi of course na nini..
tumejaribu kuwaeleza.. ndio hicho kilichotokea. Lakini mimi sijui.. wala
sikujua kama mama yangu yuko ndani kwa sababu pale ofisini nimekwenda
kufuata gari .”–Jonas
“.. Na ndio maana nasema kama mkipata
muda na nyie mnaweza kwenda kumuuliza yule mama je tumegombana.. je kuna
kitu kama hicho.. hiyo ndio habari iko hivyo.. hakuna ukweli kwenye
hilo..”–Jonas
No comments:
Post a Comment