Tegete akiwa na kocha Marcio Maximo, mshambuliaji huyo leo amewapa raha wanayanga |
Azam waliotibuliwa rekodi yao ya kutofungwa katika ligi ya tangu msimu uliopita |
Simba wameshindwa kupata ushindi katika mechi zao tano baada ya leo kulazimishwa sare ya 1-1 jijini Mbeya |
Yanga ambayo ilisimamishwa na watani zao Simba kwa kutoka suluhu mechi iliyopita waliwafundisha soka Stand United kwenye uwanja wao kwa mabao ya Jaja aliyetangulia kufunga dakika ya 13 kabla ya Tegete kufunga mawili akitokea benchi na kuwadhihirisha mashabiki wa kandanda uwezo wa kufunga anao.
Nyota huyo wa zamani wa Taifa Stars alifunga bao la kwanza dakika ya 77 kabla ya kuongeza jingine dakika ya 90 na kumpa raha Maximo aliyekuwa akicheza pambano la pili ugenini baada ya lile la Mtibwa Sugar na kucharazwa mabao 2-0.
Katika pambano jingine lililochezwa Chamazi, mabingwa watetezi walitibuliwa rekodi yao ya kucheza mechi mfululizo bila kufungwa baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu.
Kipigo hicho kimehitimisha rekodi ya Azam ambayo ilikuwa haijaonja kipigo tangu msimu uliopita ikiwa imecheza mechi 38 ikigawa maumivu kwa wenzake.
Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na Samuel Kamutu dakika ya 45 na kuiacha Azam wakisaliwa na pointi 10 baada ya mechi tano.
Nayo Simba ilikuwa ikiongoza kwa muda mrefu bao 1-0 dhidi ya Prisons wamejikuta wakiendeleza mdudu wa sare baada ya kutoka 1-1 kufuatia wenyeji kuchomoa bao jioni na kuifanya Simba kupata droo ya tano mfululizo katika ligi hiyo.
Simba ilianza kuandika bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Emmanuel Okwi kabla ya wenyeji kuchomoa dakika ya 90 kupitia kwa Hamis Mahingo mmoja wa viungo mahiri kwa sasa nchini.
Ruvu Shooting ikiwa nyumbani uwanja wa Mabatini imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Morogoro.
Kutoka Bukoba, wenyeji Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya 1-1 na Coastal Union. Wenyeji walianza kupta bao dakika ya 70 kupitia kwa Salum Kanoni ambaye hata hivyo hakumaliza pambano ilo kwa kupewa kadi nyekundu kabla ya Coastal Union kusawazisha kupitia kwa Rama Salim
No comments:
Post a Comment