|
Benzema akifunga bao la tatu la Real Madrid |
|
Neymar akishangilia bao lake la mapema kabla ya Real Madrid kuwageuzia kibao |
|
Ronaldo akifunga penati yake |
|
Real wakishangilia bao la pili lililofungwa na Pepe |
|
Piga Keleleeee Pepe akishangilia bao lake |
|
Benzema akipongezwa na Ronaldo kwa bao lake la tatu |
|
Messi akimpongeza Neymar kwa bao la mapema lililokuwa la kufutia machozi kwao |
|
Messi hoi mbele ya Ronaldo |
REAL Madrid wakiwa uwanja wa nyumbani wa Santiago Bernabeu wameizamisha wapinzani wao wa jadi, Barcelona iliyoshuka dimbani kwa mara ya kwanza wakiwa na nyota wao Luis Suarez kwa mabao 3-1 katika pambano la La Liga.
Barcelona walianza kwa mkwara kwa kuandika bao la kuongoza katika dakika ya nne kupitia kwa Neymar akimalizia kazi nzuri ya Suarez aliyekuwa akicheza kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya Hispania akitokea kifungoni.
Hata hivyo Cristiano Ronaldo aliendeleza rekodi yake ya kufunga mabao katika ligi hiyo kwa kufunga bao la kusawazisha katika dakika ya 35 kwa mkwaju wa penati na kufikisha bao la 16 katika mechi 9 za ligi hiyo.
Mabao mengine ya Real Madrid yalifungwa na Pepe katika dakika ya 50 kwa kichwa akimalizia mpira uliopigwa na Tom Kroos kabla ya Karim Benzema kuongeza bao la tatu lililowanyong;onyesha Barcelona na kuvunja rekodi yao ya kutopoteza katika ligi ya msimu huu.
Benzema alifunga bao hilo katika dakika ya 61 akimalizia kazi nzuri ya James Rodriguez na kuwapa Real Madrid ushindi uliowafanya wafikishe jumla ya pointi21 na kushika nafasi ya pili wakitofautiana pointi moja na Barcelona wenye pointi 22.
No comments:
Post a Comment