STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 19, 2014

Angel di Maria amfunika Lionel Messi kwao Argentina

http://media.themalaysianinsider.com/assets/uploads/articles/lionel-messi-reuters-062214.jpg.JPGKIUNGO wa Manchester United, Angel Di Maria amewapiku Lionel Messi na Sergio Aguero na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Argentina anayecheza soka nje ya nchi.
Di Maria (26), alikuwa miongoni mwa kikosi cha Argentina kilichofurukuata na kufika fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil, wakati pia alikuwa silaha muhimu kwa klabu yake ya zamani ya Real Madrid wakati ikiutwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya 10 (La Decima) msimu uliopita.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa 'The Albiceleste', ambaye pia ametwaa Kombe la Mfalme (Copa del Rey) na UEFA Super Cup akiwa na Madrid 2014, amekuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya usajili Uingereza  baada ya Agosti kuijunga na United kwa paundi milioni 59.7.
Di Maria amefunga mabao matatu kwenye mechi 11 tangu ajiunge na Mashetani Wekundu (Red Devils) hao, ingawa ametupwa nje mechi tatu kutoka na kuwa majeruhi.
Hiii ni mara ya kwanza kwa Messi kushindwa kutwaa tuzo hiyo ya 'Olimpia de Plata' tangu 2006, licha ya mchezaji huyo wa Barcelona kufunga mabao 56 kwa klabu na nchi yake mwaka huu na kutwaa tuzo ya Mpira wa Dhahabu kwa nchi yake kutokana na kuwa mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Dunia.
Aguero pia amefurahia kuvutia mwaka huu baada ya kuisaidia Manchester City kutwaa ubingwa wa England msimu uliopita wakati pia kwa sasa akiongoza kwa ufungaji akiwa na mabao 14 msimu huu.
Kadhalika, Lucas Pratto wa Velez Sarsfield ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ndani wa Argentina.

No comments:

Post a Comment