STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 19, 2014

438,960 wachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, wasome hapa!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhsA3WpuEiX5vgwlBeYwyweMxrRst1WhE1EBR9om6MzVWSAtwVet0MqxiJ2KITd92xBvuKloWWP9h5wMJ_7v8SNjmR5yKyRM-8oxfPUsROsLNefXsdD0WMm5onXGNHnWxKRsqP406tMVF4c/s1600/c3.jpg
Naibu Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Kassim Majaliwa.
JUMLA ya wanafunzi 438,960 kati ya 451,392 ya waliofanya mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza.
Naibu Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mhe. Kassim Majaliwa  ametoa taarifa ya serikali kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015.
Akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa ofisi za  TAMISEMI, jijini Dar, Majaliwa alisema;

“Wanafunzi 438, 960 kati ya 451,392 waliofaulu mtihani wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika  shule za serikali katika awamu ya kwanza.”
Akaongeza: “Idadi hiyo ni sawa na asilimia 97.23 ya wanafunzi waliofaulu mtihani na kwa matokeo hayo yanayonesha kuwa na alama ya juu kabisa kwa wavulana ilikuwa 243 na kwa wasichana 240 kati ya alama 250.”
Aidha, naibu huyo amewaagiza wazazi, walezi, wadau wa elimu na halmashauri zote kukamilisha majengo na kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment