STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 19, 2014

Falcao anogewa OT, awang'ang'ania Mashetani Wekundu

http://static.guim.co.uk/sys-images/Football/Pix/pictures/2014/10/5/1412513205570/Radamel-Falcao-celebrates-012.jpg
Falcao akishangalia moja ya mabao yake
MSHAMBULIAJI nyota wa Colombia anayeichezea Manchester United kwa mkopo, Radamel Falcao amesisitiza kwamba anataka kubaki Manchester United lakini anafahamu kwamba anapaswa kukomaa ili apate nafasi zaidi ya kucheza katika kikosi cha Louis van Gaal.
Dili la kulipa euro milioni 56 kwa Monaco ili kubadili uhamisho wake wa mkopo uwe wa kudumu tayari umeafikiwa, ingawa Man U wanalo chaguo la kusubiri hadi mwisho wa msimu kuona kama wanaridhishwa na uzima na kiwango cha strika huyo kabla ya kukamilisha uhamisho.
Falcao amecheza mechi nane tu za Ligi kuu ya England msimu huu kutokana na maumivu ya 'kiazi' cha mguu na mshambuliaji huyo amesema hatma yake bado haijaamuliwa.
"Kwa upande wangu, ndiyo, nataka kubaki, lakini lazima nichanganue hali iliyopo," alisema Falcao.
"Nitaona kama nitachezeshwa zaidi na kuona maamuzi yatakayochukuliwa na bodi. Lakini kwa upande wangu, nataka kubaki.
"Naona kwamba timu tayari inanihitaji. Kila ninapopata fursa ya kuingia uwanjani najaribu kufanya kilichobora kwa ajili ya kocha na kuisaidia timu.
"Kila mcheza soka anataka kuchezeshwa, hakuna anayekuwa na furaha asipocheza, anapokaa benchini, lakini kila ninapopewa fursa, iwe kwa dakika tano, 10, 20 au 90, najituma niwezavyo."

No comments:

Post a Comment