STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 19, 2014

Shilole ana Malele, akipika filamu mpya

http://vibe.co.tz/wp-content/uploads/2014/09/shilole.jpgMUIMBAJI nyota nchini aliye pia muigizaji filamu, Zuwena Mohamed 'Shilole' ameachia kazi yake mpya iitwayo 'Malele' wakati akijiandaa kutengeneza filamu iitwayo 'Shilole In Dar'.
Shilole  a.k.a Shishii Beibii' aliyekuwa akisumbua na 'ngoma' yake iitwayo 'Namchukua' ameiachia kazi hiyo mpya majuzi na tayari imeanza kusumbua hewani.
Msanii huyo alidokeza kuwa wimbo huo ameandikiwa na mkali kutoka Nyumba ya Vipaji (THT) Barnaba Boy na umetengenezwa katika studio za mtayarishaji Nahreel.
"Baada ya kutamba na nyimbo kadhaa nyuma, safari hii nakuja na Malele, pia nilitaka kuwadokeza mashabiki wangu pamoja na kuwa kimya katika masuala ya filamu, lakini kuna kazi natarajia kuanza kuirekodi itafahamika kama 'Shilole In Dar'," alisema Shilole.
Shilole alisema filamu hiyo itarekodiwa Igunga mjini Tabora na jijini Dar es Salaam ikirejea simulizi juu maisha yake kutoka kwao Tabora mpaka kuja kutikisa jijini Dar.
Msanii huyo ni mmoja ya waimbaji wa kike wanaofanya vizuri nchini baada ya kufaishwa na nyimbo kama 'Lawama', 'Dume Dada', 'Paka wa Baa', 'Chuna Buzi', 'Nakomaa na Jiji' na 'Namchukua'.

No comments:

Post a Comment