STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 19, 2014

Zola D King sasa kuja na kipindi cha runinga

http://3.bp.blogspot.com/-XpkM1hU5p-w/UQiyEQPyyzI/AAAAAAAAEUM/IbEOVC5n9U4/s1600/Zola+D2.JPG
Zola D King katika pozi

Zola D KIng baada ya kupiga tizi
MWANAHIPHOP  David Michael 'Zola D King' anajiandaa kurusha kipindi maalum cha mazoezi kitakachokuwa kikirushwa na kituo kimoja cha runinga nchini, kikiwa na lengo la kutaka kuwahamaisha watu kufanya mazoezi hata bila kwenda kwenye vituo vya mazoezi (gym).
Akizungumza na MICHARAZO, Zola D aliyeachia wimbo wake mpya wa 'I Don't Care' alisema kipindi hicho kwa matangazo ya awali tayari kimeshatengenezwa na kitakuwa kikirekodiwa kila siku ili kuwapa watazamaji mbinu mpya za kujenga mwili na kuuweka vema kiafya bila kupiga nondo (kunyanyua chuma).
"Katika harakati za kuisaidia jamii kujenga utamaduni wa kupenda kufanya mazoezi kwa afya zao, Zola D kupitia kampuni yake ya Under Films inatarajia kuanza kurusha hewani kipindi maalum cha mazoezi, hiki ni tofauti na vile vilivyozoeleka," alisema.
Alisema kipindi hicho kitawarahisishia watazamaji na watu wengine wanaopenda kufanya mazoezi kujifanyia kokote walipo bila kusubiri kwenda 'gym' au maeneo maalum la kufanyia mazoezi na kwa gharama rahisi.
"Nadhani kabla ya mwisho wa mwezi huu kitaanza kuruka hewani," alisema mkali huyo aliyewahi kutamba na nyimbo kama 'Moto wa Tipper', 'Jana Sio Leo' na 'Msela Sana'.

No comments:

Post a Comment