STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 19, 2014

Tanzania yapaa FIFA, Rwanda yaibwaga Uganda

http://4.bp.blogspot.com/-tipzDvnfDgU/U8wqo38F7wI/AAAAAAAA9y8/aluV53LA9y4/s400/IMG_2184.jpgNCHI ya Tanzania imepanda kwa nafasi saba kwenye viwango vya Shirikisho la Soka duniani, FIFA, vilivyotangazwa huku Rwanda ikiwa nchi iliyopanda kwa nafasi nyingi zaidi mwezi huu ikiibwaga Uganda waliokuwa wakiongoza katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa muda mrefu iliyoporomoka.
Katika Ukanda wa Cecafa, Rwanda ndiyo inayoongoza kutokana na kupanda kwa nafasi 22 hivyo kushika nafasi ya 68 Fifa wakati Tanzania ikishika nafasi ya 105 kwa sasa.
Uganda inashika nafasi ya pili Cecafa baada ya kupanda kwa nafasi mbili huku kwa upande wa Fifa ikiwa ni ya 76, wakati Sudan ni ya 110, Kenya (111), Ethiopia (116), Burundi (116), Sudan Kusini (189), Eritrea (202), Somalia (1204) na Djibouti ni ya 206.
Algeria ndiyo inayoongoza katika 10 bora kwa upande wa Afrika huku kidunia ikishika nafasi ya 18, ikifuatiwa na Tunisia ambayo ni 22, Ivory Coast (28), Senegal (35), Ghana (37), Guinea (39), Cape Verde (40), Cameroon (42), Nigeria (43) na Zambia ikiwa ya 46.
Hakuna mabadiliko yoyote kwa timu zilizoingia 10 bora ya viwango hivyo kidunia kwani ni zile zile za mwezi uliopita zikiongozwa na Ujerumani ambayo ilitwaa Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu.
Nafasi ya pili inashikwa na Argentina ikifuatiwa na Colombia, Ubelgiji, Uholanzi, Brazil, Ureno, Ufaransa, Hispania na Uruguay.
Italia ipo nafasi ya 11 ikifuatiwa na Switzerland     wakati England ambayo Ligi Kuu yake ina wapenzi wengi barani Afrika, ikishika nafasi ya 13 katika viwango hivyo ambavyo hutolewa kila mwezi.

No comments:

Post a Comment