STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 19, 2014

Diamond nouma! Alipa nusu mshahara wa Boban ili akipigie Friends

Diamond Platnumz aliyejitolea kulipa mshahara wa Boban katika klabu ya Friends Rangers
Boban anayemtia wazimu Diamond kwa umahiri wake uwanjani
MSHINDI wa tuzo saba za Kili Music-2014 na tatu za CHAOMVA-2014, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ameonyesha namna gani yeye ni mtu wa kujichanganya ndani ya jamii baada ya kudaiwa kukubali kulipa nusu ya mshahara anaolipwa kiungo mshambuliaji anayemhusudu, Haruna Moshi 'Boban' aliyetua Friends Rangers.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya klabu hiyo ni kwamba Diamond amekubali kutoa fedha hizo ili tu Boban mchezaji anayemzimia kupita maelezo akipige timu hiyo iliyopo Ligi Daraja la Kwanza na ambayo ipo katika nafasi nzuri katika kinmyang'anyiro cha kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2015-2016.
"Diamond amekubali kulipa nusu ya mshahara wa Boban, na mwingine katoka theluthi ya mshahara huyo na kilichobaki kitalipwa na uongozi wa klabu ya Friends ambayo inapiga kupanda Ligi kuu," mtoa habari huyo aliidokeza MICHARAZO.
Kiwango cha mshahara cha mchezaji huyo ndani ya klabu hiyo
MICHARAZO inayo, ila kwa kuwa ni suala la mtu binafsi imeamua kuuweka kapuni, na kiwango atakapochotoa Diamond pia inafahamu na kile kingine cha mdau wa klabu hiyo ni Sh. 300,000 na huku uongozi ukiwa na jukumu jepesi la kumaliza mzigo kamili.
Nyota huyo wa zamani wa Simba na Taifa Stars aliyekuwa hana timu tangu alipoachwa na Coastal Union mwsihoni mwa msimu uliopita amejiunga na timu hiyo sambamba na wakali wengine kama Amir Maftaha kuonyesha namna gani klabu hiyo imepania kucheza ligi kuu msimu ujao.


No comments:

Post a Comment