STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 19, 2014

Makubwa yaibuka kifo cha Ebosse, yadaiwa alipigwa

http://i.ytimg.com/vi/nRgfnT26dgY/hqdefault.jpg
Ebosse siku alipokuwa akiipigiania roho yake

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/79828000/jpg/_79828541_ebosse.jpg
Ebosse enzi za uhai wake akiwajibika uwanjani

IMEFAHAMIKA kuwa nyota wa kimataifa wa Cameroon, Albert Ebosse aliyefariki uwanjani wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Algeria kuwa alipigwa na siyo kama alishambuliwa na kitu chenye nchi kali dimbani.
Vipimo vipya vya uchunguzi vimedai kuwa mchezaji huyo aliyekuwa akiichezea JS Kabylie alifariki kwa kupigwa na sio kupigwa na kitu chenye ncha kali kama ilivyodaiwa hapo awali. 
Mshambuliaji huyo aliyekuwa na umri wa miaka 24 alifariki dunia Agosti mwaka huu baada ya timu yake kufungwa katika mchezo wa soka. 
Matokeo ya uchunguzi uliofanywa na mamlaka za Algeria ulibaini kuwa mchezaji huy alifariki dunia kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani. 
Lakini vipimo vipya vilivyofanyika kwa ombi la wanafamilia vimedai kuwa kifo cha Ebosse kimetokana na kushambuliwa kwa kupigwa ikihisiwa kuwa katika chumba cha kubadilishia nguo. 
Ripoti hiyo ya Andre Moune inadai kuwa Ebosse alijeruhiwa maeneo kadhaa katika mwili wake huku kukiwa na dalili za kupambana wakati akishambuliwa. Familia ya mchezaji huyo imesema itafikisha ushahidi huo mpya kwa Shirikisho la Soka la Cameroon sambamba na Shirikisho la Soka la Afrika kwa ajili ya hatua zaidi.

No comments:

Post a Comment