NYOTA wa Ivory Coast anayechezea klabu ya Chelsea Didier Drogba
anatarajiwa kutangaza kustaafu kuichezea klabu hiyo mara baada ya
kumalizika kwa msimu huu akiwa amerejea Chelsea akitokea Galatasaray ya
Uturuki .Drogba ambaye kwa Chelsea anahesabika kama gwiji ametengenezewa nafasi ya kubaki ndani ya klabu hiyo mara atakapostaafu ambapo ataendelea kuwepo chini ya kocha Mreno Jose Mourinho .
Drogba anatarajiwa kukaa kwenye benchi la Chelsea akiwa mmoja wa makocha wasaidizi wa Mourinho jukumu ambalo nyota huyu wa Afrika ameafiki kulichukua baada ya kukubali kuwa hawezi kuendelea kucheza katika kiwango cha juu .

Drogba amepanga kustaafu mwishoni mwa msimu huu .
Atakapostaafu Didier Drogba atakuwa msaidizi wa Jose Mourinho kwenye benchi la ufundi.
No comments:
Post a Comment