STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 4, 2015

CHAMIJATA WAALIKWA CHINA, DIWANI AWAPA BAO

[DSC08287+[800x600].JPG]
Mwenyekiti wa CHAMIJATA, Mohammed Kazingumbe
CHAMA cha Michezo ya Jadi Tanzania (Chamijata) kimesema kimepata mwaliko kushiriki mashindano ya kurusha mishale ambayo yatafanyika nchini China kuanzia Machi 28 hadi 20 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chamijata Tanzania Mohammed Kazingumbe wakati akizungumza na jijini Dar katika ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam.
Alisema Chamijata imekuwaikipata mialiko mara kwa mara katika nchi za China na Korea Kusini hivyo kwa mwaka huu mwaliko wa kwanza ni kutoka China na mialiko mingine ipo ambayo ni kwenda Korea Kusini mwezi Septemba.
Mwenyekiti huyo alisema kwa sasa wanahangaika kutafuta wafadhili ili waweze kupeleka timu na viongozi wa Chamijata wakati huo ukifika.
"Tumepata mwaliko wa kwenda China katika mashindano ya kurusha mishale ambayo yatafanyika Machi 28 hadi 30 hivyo jithada na mikakati yetu ni kuhakikisha kuwa tunashiriki," alisema Kazingumbe.
Kazingumbe alisema Chamijata ina imejipanga vilivyo ili kuhakikisha kuwa michezo ya jadi inarejea katika hadhi yake ya awali ambapo amewaomba wadau kuwasaidia kufanikisha hilo.
Mwenyekiti huyo alisema Chamijata katika kuhakikisha kuwa inakuza mchezo huo itatumia kitabu ambacho wamekiandika chenye maelezo kwakina kuhusu mchezo wa bao.
Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Msongola Angelina Malembeka ametoa msaada wa mabao matatu kwa Chama cha Michezo ya Jadi Tanzania (Chamijata) ikiwa ni jitihada zake za kuendeleza mchezo huo.
Malembeka ambaye pia ni Katibu wa Madiwani wa Manispaa ya Ilala alikabidhi mabao hayo jana katika ofisi za Chamijata zilizipo Temeke jijini Dar es Salaam.
Alisema ameamua kutoa msaada huo kwa Chamijata kutokana na kuona kwa muda mrefu mchezo huo umeshindwa kuvuma hivyo kwa kuanzia mabao hayo yatawasaidia.
Diwani huyo alisema pia katika kuendeleza mchezo huo amegawa mabao katika mitaa tisa ya Kata yake lengo likiwa ni kuendeleza mchezo huo kuanzia Mitaa hadi ngazi ya Taifa.
"Jamani naomba mpokee mabao haya ila naahidi kuendelea kuwasaidia pale msaada utakapo hitajika kwani mimi ni mdau  wa michezo hasa michezo ya jadi," alisema Malembeka.
Malembeka alisema iwapo michezo ya jadi itapewa kipaumbele ni dhahiri kuwa jamii itadumisha tamaduni zake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chamijata Gamaliel Mhanga alimshukuru Diwani huyo kwa msaada wa mabao hayo ambapo aliwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia chama hicho.
Mhanga alisema Chamijata imejipanga kutekeleza mipango yake mbalimbali ya kuboresha na kuendeleza michezo ya jadi kwa kushirikiana na wadau kama Diwani Malembeka.

No comments:

Post a Comment