STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 4, 2015

New Family Group yaiomba serikali kudhibiti panya Road

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYt0VvknsAULCfXKblhX-k4MAqyoupcdtUtit8OCIsc5iad7xmCsz-Gdc5Tv6VcadL4wW6tpyDwCYkiHdNfytf3FXuXJ3WBuPq1ghcDLkP3-nf84TGXfrDG7o5SL2ZYf93aK0UwLJHqSpS/s1600/panya+Road.jpg
baadhi ya wanaodaiwa kuwa viongozi wa kundi la OPanya Road waliponaswa hivi karibuni
Mwandishi Maalum
KITUO cha New Familiy Group (NGFG) cha Mwasonga Temeke jijini Dar es Salaam kimeomba Serikali kushirikina na kituo hicho ili kuweza kuwahifadhi vijana ambao wanaonekana kuleta hofu katika Jiji wanaotambulika kwa jina la 'Panya rodi' ili waweze kulelewa kituo hapo.
Ombi hilo linakuja ikiwa ni siku moja vijana hao kutajwa kuwa wameibuka katika Wilaya ya Kinondoni na Ilala na kufanya matokio ambayo yanahatarisha amani kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa NHFG Omari Kombe alisema kikundi hicho ambacho kinaundwa na vijana wengi wa mitaani kutoka mikoani kipo kwa muda mrefu lakini udhibiti wake umekuwa wa kusuasua.
Kombe alisema wamekuwa wakiwasiliana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto pamoja na Jeshi la Polisi kupitia dawati la Jinsia ili kwa pamoja waweze kupata muafaka wa tatizo hilo ila mwitiko kwa upande wa Serikali umekuwa duni.
"Unajua kwa muda mrefu vijana hawa wamekuwa wakifanya matukio mbalimbali ya uhalifu na hili la jana ni endelevu lakini njia ambayo inaweza kuwa ni suluhisho ni kuhakikisha kuwa kunakuwepo na eneo ambalo linaweza kuwapatia mafunzo ya ufundi, ujasiriliamali na mengine ambayo yatakuwa na tija nao," alisema Kombe.
Kombe alisema NHFG ipo tayari kushirikiana na Serikali kwa kutoa eneo ambalo litajengwa kituo kikubwa mbapo watapata mafunzo hali ambayo inaweza kuleta amani kwa jamii.
Mwenyekiti huyo alisema NHFG ina eneo la heka 10 hivyo iwapo Serikali itaona ni jambo la msingi kujenga wao wapo tayari kushirikiana kwa maslahi ya vijana hao na nchi kwa ujumla.
Alisema iwapo vijana hao watashindwa kudhibitiwa kwa sasa ni ishara tosha kuwa nchi inatengeneza majambazi kwa miaka ijayo ambayo yatakuwa na uzoefu wa kutosha.
Kombe alisema vijana hao wameanza kutumiwa na kundi lingine la Mbwa Mwitu ambalo nalo limekuwa likiibuka kila mara katika maeneo  mbalimbali ya mji.
Alitoa rai kwa wananchi kuhakikisha kuwa wanashirikiana na Serikali hasa Jeshi la Polisi ili kuhakikisha kuwa matatizo hayo ya uwepo wa panga rodi na mbwa mwitu yanaisha.

No comments:

Post a Comment